#COVID19 Kwa jinsi kirusi cha Corona cha India kinavyosambaa sasa Afrika, nikiambiwa hakijafika Tanzania nitashangaa

#COVID19 Kwa jinsi kirusi cha Corona cha India kinavyosambaa sasa Afrika, nikiambiwa hakijafika Tanzania nitashangaa

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Tafadhali Mamlaka husika chukueni Tahadhari haraka kwani tayari Kirusi hatari na Kipya cha Corona kilichopo nchini India kimeanza Kusambaa Kwetu barani Afrika.

Mpaka sasa Kirusi hiko kimefika nchi za Nigeria, Algeria, Congo Brazaville, Kenya, Uganda, Morocco na Afrika Kusini kwa mujibu wa Kipindi kizuri cha Nipashe cha Radio One asubuhi ya leo.

Kuna Mtu (nimemsahau) alitudanganya kuwa Tanzania tupo salama na tusiogope huku akisema Corona haipo Tanzania hivyo namuomba Rais Samia nae asitudanganye na ikiwezeka hatua Kali za Kudhibiti zianze Kuchukuliwa sasa.

Yaani kiwe Kenya na Uganda (kwa Majirani zetu) halafu Tanzania kisiwepo? Kikiwa hakipo najitolea Kuogelea Baharini kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar.
 
Msitutishe hiyo corona iko wapi?

Kila siku corona this corona that wakati si tunaishi fresh; tumejaa masokoni, tumejaa kwenye daladala nyie mmejifungia kwenye magari na barakoa lakin hakuna maajabu yoyote, wala hospital hazijajaa wala hakuna mizoga inayookotwa barabarani.
 
Msitutishe hiyo corona iko wapi?

Kila siku corona this corona that wakati si tunaishi fresh; tumejaa masokoni, tumejaa kwenye daladala, nyie mmejifungia kwenye magari na barakoa lakin hakuna maajabu yoyote, wala hospital hazijajaa wala hakuna mizoga inayookotwa barabarani.
Kutoa Tahadhari ni Kosa sana?
 
B1617 kilianzia south Africa, nature ya kirusi hiki hakipendi kabisa watu weupe. Ha ha ha jokes.
 
Vaa Barakoa, epuka mikusanyiko na nawa mikono na maji tirirka.
 
Kutoa Tahadhari ni Kosa sana?
Tahadhari gani unatoa?

Eti tahadhari...

Eti kirusi cha india, unajua hata ku-isolate virus lab au hata basics za public health hasa epidemiology au una bwabwaja tu kisa umeona kirus cha India kwa Millard Ayo na azam tv!

Hebu kaa kwa kutulia usubiri mwez uonekane ukale biriani na kuimba kaswida, hizo ndo level zako achana na hizi zingine unajidhalilisha
 
nimeona india unaweza kuchoka yani watu wanakula kula kuni mpaka kuni zimekwisha kwa sababu vifo ni vingi kupelekea kuelemewa
Tusafirishe kuni to India mzee wangu, hizo ndo fursa ..si unajua kufa kufaana
 
Tafadhali Mamlaka husika chukueni Tahadhari haraka kwani tayari Kirusi hatari na Kipya cha Corona kilichopo nchini India kimeanza Kusambaa Kwetu barani Afrika.

Mpaka sasa Kirusi hiko kimefika nchi za Nigeria, Algeria, Congo Brazaville, Kenya, Uganda, Morocco na Afrika Kusini kwa mujibu wa Kipindi kizuri cha Nipashe cha Radio One asubuhi ya leo.

Kuna Mtu ( nimemsahau ) alitudanganya kuwa Tanzania tupo salama na tusiogope huku akisema Corona haipo Tanzania hivyo namuomba Mamie nae asitudanganye na ikiwezeka hatua Kali za Kudhibiti zianze Kuchukuliwa sasa.

Yaani kiwe Kenya na Uganda ( kwa Majirani zetu ) halafu Tanzania kisiwepo? Kikiwa hakipo najitolea Kuogelea Baharini kutoka Dar es Salaam hadi Zanzibar.
Zenziba hapo sisi tunaenda na baiskeli kila siku kufuata halua na karafu
 
Kutoa Tahadhari ni Kosa sana?
Hasira za nini. Wewe vaa barokoa mwenyewe, weka distance wewe na familia yako ikiwezekana jifungieni ndani kabisa, acha watanzania wanao amua kutafuta ridhiki nje waendelee

NB
Ukiona inafaa pia wapigie simu na ndugu zako wavae barakoa na wasiende sokoni pia. Siyo kuleta hoja za kijinga hapa.
 
Tahadhari gani unatoa?

Eti tahadhari...

Eti kirusi cha india, unajua hata ku-isolate virus lab au hata basics za public health hasa epidemiology au una bwabwaja tu kisa umeona kirus cha India kwa Millard Ayo na azam tv!

Hebu kaa kwa kutulia usubiri mwez uonekane ukale biriani na kuimba kaswida, hizo ndo level zako achana na hizi zingine unajidhalilisha
Hopeless.....!!
 
Back
Top Bottom