Kwa Jinsi Rais Magufuli alivyotangaza mambo ambayo Mkapa alifanya naona kila kitu cha maana leo yeye ndio alianzisha

Kwa Jinsi Rais Magufuli alivyotangaza mambo ambayo Mkapa alifanya naona kila kitu cha maana leo yeye ndio alianzisha

Street Hustler

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
2,175
Reaction score
4,299
Nimesikiliza mambo ambayo Rais Magufuli anayasema kuhusu Mkapa binafsi naona Mkapa ni shujaa mkubwa mno wa Taifa hili maana alianzisha mambo muhimu mno mpaka sasa na sisi ambao wengi hatujui tulijua hayo yalianzishwa na Mwl. Nyerere au Mzee Mwinyi kumbe ni Mkapa, pia naona yale maubabe aliyokuwa anayafanya kumbe ilkua ni kwa nia njema kabisa.

Angalia jinsi alivyokuwa ana coordinate uchumi pia naskia alivyoingia madarakani hakuna CHAKULA kiliongezeka bei, binafsi sijui aliemfata madarakani Mzee Kikwete pamoja na kusafiri sana sijui makubwa ya maana aliyoyafanya hapa nchini ni nini hapo ndo napopata akili ya kuwa Rais Magufuli kumbe ameanzia pale alipoishia Mkapa.

Sasa naamini kwa maneno aliyoongea ya sifa tele kwa Mkapa akipita uchaguzi huu tutegemee wananchi kutokuwa na PESA mifukoni hasa wale wasiokuwa na ajira rasmi au shughuli rasmi ya kuingiza kipato na badala yake lazima apige Miradi mikubwa zaidi itakayoacha alama KUBWA kuwa hii iliasisiwa au kufanywa na Magufuli.
 
Kikwete miaka kumi yake ndio uchumi wote ulipoharibika hata wakati wa mkpa foreign reserve ilikua kubwa mkapa alifuta madeni karibia yote, JK alikopa hata cha maana hakufanya akamaliza pesa zote, ufisadi dili zikawa nyingi, Kikwete ndio iliua uchumi wa nchi.
 
aldeo,

Hivi kama leo hii ikitokea huyu wa sasa atwaliwe (Mungu apishie mbali though), jee ni kitu gani hasa cha maana (landmark) atakumbukwa kwacho?

Kumbuka hivi hapa chini ni vya JK:

- Kigamboni (Nyerere) bridge
- JNIA terminal 3
- flyovers (TAZARA, Ubungo & Kurasini)
- DART
- TZ kuingia uchumi wa kati (JK kachangia $480B, Mkapa $330B, JPM $100B)
- tarmac road network mikoani & wilayani
- UDOM
- Medical infrastructure (Mloganzila, JKCI)
 
aldeo,

Kama ulivyokuwa hujui mazuri ya BWM, hivyohivyo hujui mazuri ya JK. Ukiambiwa utasema wooow! Kumbe naye alifanya makubwa pia.

JK naye ana makubwa mengi kaifanyia nchi hii, nayo yakisemwa ni mengi tu, labda wewe huna taarifa.

Lakini leo ni siku ya BWM hatuna haja ya kuongelea marais wengine.
 
aldeo,

Subiri Kikwete nae akitangulia mbele za haki (God forbid) utakuja kuanzisha uzi mnono km huu. Maana hapa naona unasema ya Kikwete huyajui.

Utayajua tu akiaga dunia kama ambavyo leo hii ndio umeyajua ya Mkapa baada ya kuaga dunia.
Sijui nimetumia lugha nyepesi hapa au!?
 
aldeo,

Mkuu Magufuli anafanya propoganda tu hana lolote,Mkapa aliamini katika mifumo,huyu magu anaamini katika one man show, Kikwete alijenga barabara nyingi na kuacha mifumo ifanye kazi zake,huyu magufuli yeye kila kitu anataka afanye yeye.
 
Back
Top Bottom