Kwa Jinsi Rais Magufuli alivyotangaza mambo ambayo Mkapa alifanya naona kila kitu cha maana leo yeye ndio alianzisha

Kwa Jinsi Rais Magufuli alivyotangaza mambo ambayo Mkapa alifanya naona kila kitu cha maana leo yeye ndio alianzisha

Kama ulivyokuwa hujui mazuri ya BWM, hivyohivyo hujui mazuri ya JK. Ukiambiwa utasema wooow!, Kumbe naye alifanya makubwa pia

JK naye ana makubwa mengi kaifanyia nchi hii, nayo yakisemwa ni mengi tu, labda wewe huna taarifa

Lakini leo ni siku ya BWM hatuna haja ya kuongelea marais wengine
Naamin hapa tunakumbushana mema na makubwa ya Mkapa kiuchumi naamini kuanzia Nyerere Mwinyi hata Kikwete hawajaacha alama KUBWA Kama Mkapa aliyoacha.
 
hivi kama leo hii ikitokea huyu wa sasa atwaliwe (Mungu apishie mbali though), jee ni kitu gani hasa cha maana (landmark) atakumbukwa kwacho?

kumbuka hivi hapa chini ni vya JK:

- Kigamboni (Nyerere) bridge
- JNIA terminal 3
- flyovers (TAZARA, Ubungo & Kurasini)
- DART
- TZ kuingia uchumi wa kati (JK kachangia $480B, Mkapa $330B, JPM $100B)
- tarmac road network mikoani & wilayani
- UDOM
- Medical infrastructure (Mloganzila, JKCI)

Muacheni Kikwete ale mema ya kustaafu, aliyo ya fanya kwa Taifa hili yanajulikana likiwemo la kumkata rafiki yake wa haja.

Leo na yeye msibani kaongozana na Hussein wake angalau.
 
Nafkir JPM kaanzia alipoishia Mkapa Ila aisee Mkapa ndo kama alianzisha NCHI upya hongera kwa Mkapa ngoja tuone ya JPM na atakae mfata

Wewe kijana, Maraisi waliopita walikuwa hawapendi misifa misifa. Walikuwa wakitenda mambo yao hawataki promo
Ukitafuta mazuri ya kila rais utayaona

Ila Mkapa ndiye msingi wa mifumo mingi tuliyo nayo sasa, JK pamoja na kuanzisha taasisi nyingine, lakini alijenga juu ya misingi ya taasisi za Mkapa na kuzipatia nyenzo mbalimbali ikiwemo bajeti na staffing kwa kuajiri sana.
 
Subiri kikwete nae akitangulia mbele za haki (God forbid) utakuja kuanzisha uzi mnono km huu. Maana hapa naona unasema ya kikwete huyajui.

Utayajua tu akiaga dunia kama ambavyo leo hii ndio umeyajua ya Mkapa baada ya kuaga dunia. Sijui nimetumia lugha nyepesi hapa au?
Ni kweli kila mtu anamema yake kwa nyakati zake ila kwangu mie naona Mkapa amefiti kwa nyakati kabla ya muda wake pia kwenye muda wake na hata baada yake hasa kiuchumi kwa wengine sioni Magufuli hatuwezi kumpima kwenye mizani hii mpaka amalize yake kumi.
 
Mleta mada unauliza kikwete alifanya nini kwani hukuwa unaziona barabara alizojenga? Acha chuki na huyo mzee, hata Magufuli huwa anamsifu sana kwa barabara na madaraja.
 
Kikwete miaka kumi yake ndio uchumi wote ulipoharibika hata wakati wa mkpa foreign reserve ilikua kubwa mkapa alifuta madeni karibia yote ,jk alikopa hata cha maana hakufanya akamaliza pesa zote, ufisadi dili zikawa nyingi, kikwete ndio iliua uchumi wa nchi
Magufuli ndo anaua uchumi,fikiri vizuri utapata majibu
 
Kikwete miaka kumi yake ndio uchumi wote ulipoharibika hata wakati wa mkpa foreign reserve ilikua kubwa mkapa alifuta madeni karibia yote ,jk alikopa hata cha maana hakufanya akamaliza pesa zote, ufisadi dili zikawa nyingi, kikwete ndio iliua uchumi wa nchi
Hata mie hili naliona Kikwete alisafiri nje Sana lakini alituacha tumechoka vibaya mno kichumi
 
Nafkir JPM kaanzia alipoishia Mkapa Ila aisee Mkapa ndo kama alianzisha NCHI upya hongera kwa Mkapa ngoja tuone ya JPM na atakae mfata

Unajua UDOM, Mwendokasi Dar, Shule za Kata, Hospitali ya Mloganzila, Daraja la Malagarasi, Daraja la Kigamboni, Umeme Kinyerezi 2, Hospitali ya Benjamin william Mkapa iliyojengwa chuo kikuu cha UDOM, Mtandao wa barabara nchi nzima, Jakaya Kikwete Health Institute, uwanja wa Ndege terminal 3, Mradi wa Gesi Mtwara hadi Dar, Mradi wa Maji Ruvu Juu hadi Dar kupitia Bunju, Vivuko kedekede, Ukarabati viwanja vya ndege, Kuongeza udahili wanafunzi wa vyuo vikuu, Daraja la Kilombero, Ajira za kumwaga, Demokrasia pana na mengine mengi tu

Hapo unaona JK hakufanya kitu?
 
mleta mada unauliza kikwete alifanya nini kwani hukuwa unaziona barabara alizojenga ? acha chuki na huyo mzee,hata magufuli huwa anamsifu sana kwa barabara na madaraja
Namaanisha kuanzisha Jambo lake binafsi la kukuza uchumi nasio muendelezo angalia mashirika mengi ya serikali yalifia kwa Kikwete alafu njoo mchukue Mkapa alafu muweke kwenye mizani hyo hyo ilimpimia Kikwete alafu lete majibu
 
Kikwete miaka kumi yake ndio uchumi wote ulipoharibika hata wakati wa mkpa foreign reserve ilikua kubwa mkapa alifuta madeni karibia yote ,jk alikopa hata cha maana hakufanya akamaliza pesa zote, ufisadi dili zikawa nyingi, Kikwete ndio iliua uchumi wa nchi
Awamu hii tuliyonayo sasa hivi, kwa miaka mitano tuu shughuli tumeiona kuhusu uchumi.
 
Akuna kitu kilikua kina tesa watanzania kama kodi ya kichwa na kodi ya baiskeli Nakumbuka ilikua watu wanajificha mapolini kukimbia kodi ya kichwa
 
Namaanisha kuanzisha Jambo lake binafsi la kukuza uchumi nasio muendelezo angalia mashirika mengi ya serikali yalifia kwa Kikwete alafu njoo mchukue Mkapa alafu muweke kwenye mizani hyo hyo ilimpimia Kikwete alafu lete majibu
Hata ujenzi wa barabara ni jambo lake binafsi la kukuza uchumi, ungesema toka mwanzo sasa kama unataka aanzishe mashirika, lakini hiyo haiwezekani kila Rais akija aanzishe mashirika yatakuwa mengi sasa na yakose maana.
 
hivi kama leo hii ikitokea huyu wa sasa atwaliwe (Mungu apishie mbali though), jee ni kitu gani hasa cha maana (landmark) atakumbukwa kwacho?

kumbuka hivi hapa chini ni vya JK:

- Kigamboni (Nyerere) bridge
- JNIA terminal 3
- flyovers (TAZARA, Ubungo & Kurasini)
- DART
- TZ kuingia uchumi wa kati (JK kachangia $480B, Mkapa $330B, JPM $100B)
- tarmac road network mikoani & wilayani
- UDOM
- Medical infrastructure (Mloganzila, JKCI)
Watakwambia SGR, STEGOLAZ, TANZANITE BRIJI, VIWANDA, UCHUMI WA KATI TUMEFIKA MAPEMA, NIDHAMU KAZINI.
 
Unajua UDOM, Mwendokasi Dar, Shule za Kata, Hospitali ya Mloganzila, Daraja la Malagarasi, Daraja la Kigamboni, Umeme Kinyerezi 2, Hospitali ya Benjamin william Mkapa iliyojengwa chuo kikuu cha UDOM, Mtandao wa barabara nchi nzima, Jakaya Kikwete Health Institute, uwanja wa Ndege terminal 3, Mradi wa Gesi Mtwara hadi Dar, Mradi wa Maji Ruvu Juu hadi Dar kupitia Bunju, Vivuko kedekede, Ukarabati viwanja vya ndege, Kuongeza udahili wanafunzi wa vyuo vikuu, Daraja la Kilombero, Ajira za kumwaga, Demokrasia pana na mengine mengi tu

Hapo unaona JK hakufanya kitu?
Nyerere bridge, Malagarasi bridge, mabibo hostel, makazi ya JWTZ nchi nzima.
 
Akuna kitu kilikua kina tesa watanzania kama kodi ya kichwa na kodi ya baiskeli Nakumbuka ilikua watu wanajificha mapolini kukimbia kodi ya kichwa
Vitu kama hivo ndio vilifanya Tz ichelewe kuendelea,mimi ninapenda sana kutazama picha,video za miaka ya zamani,ukitazama maisha walioishi wazaire,waganda,wakenya na wasouth alafu tazama picha za watanzania utaona watanzania wengi waliishi maisha ya dhiki hata hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000, lakini videos na picha za wacongo wa kawaida kabisa za miaka ya 70 utaona walivovaa mavazi mazuri na kuishi nyumba nzuri. Haya mambo ya kina Diamond kubadili magari kila siku waliyafanya kina JB mpiana miaka ya 90 huko.
 
aldeo,

Nilikuja kuanzisha uzi kama huu. Mara nakuta umeuweka hapa tayari! Mungu wetu ni mkubwa na mwema. Leo ukweli umejulikana. Watoto wa siku hizi waliaminishwa na walamba viatu (ikiwemo TBC) kuwa kila kitu kimefanyika awamu ya 5! Uongo mtupu. Marais wengine wana mchango wao pia. Tuache sifa za uongo jamani. Tuombe kura bila ya kupanda kwenye mabega ya wengine. Siyo ustaarabu kabisa.

Lakini ukisikiliza tofauti ya indicators za uchumi kabla na baada ya 1995 utajiuliza Mzee Mwinyi alikuwa analipeleka wapi taifa. Na hata hivyo kuna watu walitaka aongezewe vipindi vya kutawala. Bahati nzuri Nyerere alikuwa hai akawatalia.
 
Mkuu magufuli anafanya propoganda tu hana lolote,Mkapa aliamini katika mifumo,huyu magu anaamini katika one man show,kikwete alijenga barabara nyingi na kuacha mifumo ifanye kazi zake, huyu magufuli yeye Kila kitu anataka afanye yeye
Ukimpima Magufuli kwenye mizani sawa ambayo tumempimia Nyerere Mwinyi Mkapa na Kikwete itakuwa sio sawa tusubiri Magufuli amalize yake kumi ndo tuje tumpime pia kuna kipindi inabidi ufanye Jambo kulingana na nyakati husika sa hii one man show huenda inamsaidia sana kuliko ile ya kuacha system ifanye kila kitu kipindi cha Kikwete labda ndo mana JK alichelewa kufika kabla hajafika but BWM ni Bora mno kwa aliyoyafanya.
 
Back
Top Bottom