Labda mnaona aibu kumsema Mwalimu, lakini uchumi wa nchi hii ulikuwa umekufa kabisa mwaka 1985
Hivi wewe una habari kuwa mwaka 1985 Mwinyi alichukua nchi uchumi ukiwa unakua kwa NEGATIVE rate (Ulikuwa ukikua kwa -3).
Hujui kuwa Mwinyi Kachukua hii nchi wakati tukifuata Uchumi wa Kijamaa ambao ulishafeli duniani, na Mwinyi kwa ujasiri akaamua kufanya reforms kwa kuanzisha soko huria!
Hujui kuwa TRA ilianzishwa kisheria na Mwinyi mwaka 1995 kabla ya mkapa kufanya Staffing mwaka 1996
Hujui ni Mwinyi ndiye aliyerudisha vyama vingi?
Hujui Barabara kwa mfano ya Dar Arusha ilijengwa kwa lami kipindi cha Mwinyi?
Ukiwa huna maono unaweza kumlaumu Mwinyi, lakini wakati Mwinyi anachukua nchi hii ilikuwa ni almost failed state, watu ni masikini choka mbaya!