Kwa Jinsi Rais Magufuli alivyotangaza mambo ambayo Mkapa alifanya naona kila kitu cha maana leo yeye ndio alianzisha

Achana nae huyooh, anadhan huo uhuru anaopata leo ulitokana na juhudi za nan? Mpuuze tyuuuh
 
Yeye si ndio kila siku anasema hamna kilicho fanyika kwenye awamu zilizopita?
 
Huyu hata akimaliza miaka 30 hakuna Cha maana anachoweza kufanya,vitu hufanywa kwa mipango na si maguvu,
We jamaa sijui una kipaji cha chuki nadhani unaishi pangoni pia.
 
Mkapa alikuwa siyo mpendwa sifa kama huyu
 
We jamaa sijui una kipaji cha chuki nadhani unaishi pangoni pia.
Mkuu Mimi ninaakili zangu I can see,I can analyse things,sipelekwi pelekwi kwa propoganda uchwara Kama unavyopelekeshwa wewe.
 
Mkuu we acha tu ukiyaandika hapa ni mlolongo lakini nina uhakika ukienda kila wilaya kwa sasa lazima uone kitu tofauti kabisa na itabidi tuanze kuvitaja kwa makundi maana kimoja kimoja itakuwani matumizi mabaya ya rasilimali muda.
 
Mtoa hoja hauko serious. Yaani hujawahi kusikia JPM kwenye hotuba zake akiponda watangulizi wake?
 
Ni kweli uliyosema. Ila Magufuri anaweza haya:-
1. Ni mropokaji kwa kuwa anapoongea hajali kadamnasi imayomsikia. Matusi ya nguoni ndiyo lugha yake ya kawaida.

2. Hapendi upinzani kwa kuwa akiruhusu atashindwa asubuhi. Ndiyo maana katumia hela ya Serikali kuwanunua wabunge wa Kinondoni, Siha na Bahati.

3. Anapenda rushwa na ufisadi ndiyo maana hataki kufanya kazi na CAG aliye nyooka.

4. Ni mwizi wa mali ya umma ndiyo maana kamuweka Katibu Mkuu Hazina ambaye ni mpwa wake. Kwa miaka 4 tayari Tsh 2.4 Trillion hazijulikani zilipo

5. Ni mpenda ukabila kwa kuwa sehemu nyeti zote amejaza ndugu na watu wa Kanda ya ziwa Angalia IGP, DPP, AG, KM-KM-Hazina, RC DSM, Waziri Nishati, CAG mpya, Waziri Viwanda, Jaji Mkuu nk

6. Ni mtu wa kufuja mali ya umma. Angalia ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato na uanzishaji wa mbuga ya Burigi -Chato

7. Amezuia shughuli za vyama vya siasa wakati CCM inafanya mkutano kila mahali. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2000 na Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 zinatambua shughuli za vyama vingi.

8. Hataki watu wajieleze kwa uhuru kadri ya katiba, na amevibana vyombo vya habari. Kwa mfano Eric Kabendera ameanzishiwa shitaka la kutakatisha fedha wakati kiukweli ni maoni yake kwenye gazeti la The Economist

9. Anachukia wenye vyeti feki lakini kamuacha Bashite aendelee kuwa RC DSM wakati naye ana cheti feki. Hata PhD yake yasadikiwa amekopi kwa supervisor wake ambaye kamteua kuwa Katibu Mkuu wa Wizara mojawapo.

10. Ameruhusu kikundi cha wasiojulikana kiteke watu, kuwatesa na wengine kuwaua kama Ben Saanane, Azory Gwanda. Na majeruhi kwa Tundu Lissu

11. Analitawala Bunge kwa remote control. Bunge haiwezi kuhoji chochote kilichofanywa na Serikali.

12. Mahakama nayo iko mfukoni mwake
 
They have eyes but pretend not to see. According to them all good things in this country have been done by either Nyerere, Mkapa and they are going to say Magufuli. Mwinyi, Kikwete and the like seem to do nothing for them, you know why? Because they are not of their caliber.

Sent from my TECNO CA6 using JamiiForums mobile app
 
Nafkir JPM kaanzia alipoishia Mkapa Ila aisee Mkapa ndo kama alianzisha NCHI upya hongera kwa Mkapa ngoja tuone ya JPM na atakae mfata.
Jk kafanya mengi nae pia ila leo ni siku ya Mkapa
 
Wanajamvi salaam

Mpaka Mkapa anafariki mimi nilikuwa naamini viongozi waliopita hawakuwa wamefanya kitu. Niliamini maneno ya viongozi wa awamu ya tano kuwa Marais waliopita hakuna walichofanya zaidi ya ufisadi tu.

Niliamini na kuaminishwa kuwa katika awamu hii ndiyo tumepata mkombozi wa kweli ambaye tunaambiwa watu kama yeye hawazaliwi mara kwa mara anstahili kuongezewa muda wa kuongoza.

Baada ya kifo cha Mkapa ndiyo nimejua kwamba kumbe kuna kiongozi aliyepita anaitwa Mkapa naye alifanya mambo makubwa na hakuongezewa muda.

Kwa maneno yake mwenyewe Rais Magufuli amemwita Mkapa Rais wa wanyonge.

Kumbe Mkapa pia alijenga madaraja na mabarabara,

Kumbe alijenga uwanja mkubwa wa mpira,

Alijenga majengo ya kisasa ya bunge Dodoma,

Kumbe naye alikuwa mpinga ufisadi akaanzisha hadi TAKUKURU,

Kumbe naye alikuwa ametilia mkazo makusanyo ya mapato akaanzisha TRA

Akaanzisha VETA,
Akaanzisha bodi ya mikopo watoto wasomeshwe kwa mikopo,

Akaanzisha MMEM na MMES, MKURABITA

Alianzisha mfumo wa ruzuku kwa vyama vya siasa,

Alisaidia nchi ikasamehewa deni la taifa USD bilioni 3

Alianzisha TCU, NECTA na MEMKWA
Nk nk nk nk

Leo ndiyo nimejua kumbe waliopita nao walifanya kitu tofauti na tunavyoaminishwa, kumbe walifanya vitu vingi na hawakuomba kuongezewa muda.
Kumbe viongozi wazuri walikuwepo na wataendelea kuwepo.

Hakika nilipotoka, tuliaminishwa sivyo, tulidanganywa. Kifo cha mzee Mkapa kimefichua mengi mazuri ya waliopita ambayo yalikuwa hayasemwi
 

Attachments

  • Screenshot_2020-07-29-10-50-03.jpeg
    73.5 KB · Views: 2
alafu kesho atasahau yote aliyosema,atasema yeye ndiye pekee ameleta maendeleo,usimuamini yule
 
Jamani Magufuli bado yake tano mingine ndo tumpime kwenye mizani hii tunaowapimia wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…