Nimesikiliza mambo ambayo Rais Magufuli anayasema kuhusu Mkapa binafsi naona Mkapa ni shujaa mkubwa mno wa Taifa hili maana alianzisha mambo muhimu mno mpaka sasa na sisi ambao wengi hatujui tulijua hayo yalianzishwa na Mwl. Nyerere au Mzee Mwinyi kumbe ni Mkapa, pia naona yale maubabe aliyokuwa anayafanya kumbe ilkua ni kwa nia njema kabisa.
Angalia jinsi alivyokuwa ana coordinate uchumi pia naskia alivyoingia madarakani hakuna CHAKULA kiliongezeka bei, binafsi sijui aliemfata madarakani Mzee Kikwete pamoja na kusafiri sana sijui makubwa ya maana aliyoyafanya hapa nchini ni nini hapo ndo napopata akili ya kuwa Rais Magufuli kumbe ameanzia pale alipoishia Mkapa.
Sasa naamini kwa maneno aliyoongea ya sifa tele kwa Mkapa akipita uchaguzi huu tutegemee wananchi kutokuwa na PESA mifukoni hasa wale wasiokuwa na ajira rasmi au shughuli rasmi ya kuingiza kipato na badala yake lazima apige Miradi mikubwa zaidi itakayoacha alama KUBWA kuwa hii iliasisiwa au kufanywa na Magufuli.
Ni kweli uliyosema. Ila Magufuri anaweza haya:-
1. Ni mropokaji kwa kuwa anapoongea hajali kadamnasi imayomsikia. Matusi ya nguoni ndiyo lugha yake ya kawaida.
2. Hapendi upinzani kwa kuwa akiruhusu atashindwa asubuhi. Ndiyo maana katumia hela ya Serikali kuwanunua wabunge wa Kinondoni, Siha na Bahati.
3. Anapenda rushwa na ufisadi ndiyo maana hataki kufanya kazi na CAG aliye nyooka.
4. Ni mwizi wa mali ya umma ndiyo maana kamuweka Katibu Mkuu Hazina ambaye ni mpwa wake. Kwa miaka 4 tayari Tsh 2.4 Trillion hazijulikani zilipo
5. Ni mpenda ukabila kwa kuwa sehemu nyeti zote amejaza ndugu na watu wa Kanda ya ziwa Angalia IGP, DPP, AG, KM-KM-Hazina, RC DSM, Waziri Nishati, CAG mpya, Waziri Viwanda, Jaji Mkuu nk
6. Ni mtu wa kufuja mali ya umma. Angalia ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato na uanzishaji wa mbuga ya Burigi -Chato
7. Amezuia shughuli za vyama vya siasa wakati CCM inafanya mkutano kila mahali. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2000 na Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 zinatambua shughuli za vyama vingi.
8. Hataki watu wajieleze kwa uhuru kadri ya katiba, na amevibana vyombo vya habari. Kwa mfano Eric Kabendera ameanzishiwa shitaka la kutakatisha fedha wakati kiukweli ni maoni yake kwenye gazeti la The Economist
9. Anachukia wenye vyeti feki lakini kamuacha Bashite aendelee kuwa RC DSM wakati naye ana cheti feki. Hata PhD yake yasadikiwa amekopi kwa supervisor wake ambaye kamteua kuwa Katibu Mkuu wa Wizara mojawapo.
10. Ameruhusu kikundi cha wasiojulikana kiteke watu, kuwatesa na wengine kuwaua kama Ben Saanane, Azory Gwanda. Na majeruhi kwa Tundu Lissu
11. Analitawala Bunge kwa remote control. Bunge haiwezi kuhoji chochote kilichofanywa na Serikali.
12. Mahakama nayo iko mfukoni mwake