Kwa Jinsi Rais Magufuli alivyotangaza mambo ambayo Mkapa alifanya naona kila kitu cha maana leo yeye ndio alianzisha

Kwa Jinsi Rais Magufuli alivyotangaza mambo ambayo Mkapa alifanya naona kila kitu cha maana leo yeye ndio alianzisha

Aisee!!
Unasema Nyerere hakuacha nae hakuacha alama kubwa???
Nikusaidie tu hata JK amecha mambo mengi mazuri na makubwa. Ingia makataba na mitandaoni utaona.
Nyerere hana mfano wa hao wote, yeye tunaweza kujaza kabati la vitabu tukiandika mazuri na makubwa aliyofanya Nyerere na yangali hai hadi sasa.

Pengine sasa hivi wewe au ukoo wenu msingemiliki ardhi na wengi wetu hapa wasingesoma bila Nyerere.
Kifupi kila unachokiona hapa Tanzania katika msingi wake kina mkono wa Nyerere.
Achana nae huyooh, anadhan huo uhuru anaopata leo ulitokana na juhudi za nan? Mpuuze tyuuuh
 
Yeye si ndio kila siku anasema hamna kilicho fanyika kwenye awamu zilizopita?
 
Nimesikiliza mambo ambayo Rais Magufuli anayasema kuhusu Mkapa binafsi naona Mkapa ni shujaa mkubwa mno wa Taifa hili maana alianzisha mambo muhimu mno mpaka sasa na sisi ambao wengi hatujui tulijua hayo yalianzishwa na Mwl. Nyerere au Mzee Mwinyi kumbe ni Mkapa, pia naona yale maubabe aliyokuwa anayafanya kumbe ilkua ni kwa nia njema kabisa.

Angalia jinsi alivyokuwa ana coordinate uchumi pia naskia alivyoingia madarakani hakuna CHAKULA kiliongezeka bei, binafsi sijui aliemfata madarakani Mzee Kikwete pamoja na kusafiri sana sijui makubwa ya maana aliyoyafanya hapa nchini ni nini hapo ndo napopata akili ya kuwa Rais Magufuli kumbe ameanzia pale alipoishia Mkapa.

Sasa naamini kwa maneno aliyoongea ya sifa tele kwa Mkapa akipita uchaguzi huu tutegemee wananchi kutokuwa na PESA mifukoni hasa wale wasiokuwa na ajira rasmi au shughuli rasmi ya kuingiza kipato na badala yake lazima apige Miradi mikubwa zaidi itakayoacha alama KUBWA kuwa hii iliasisiwa au kufanywa na Magufuli.
Mkapa alikuwa siyo mpendwa sifa kama huyu
 
We jamaa sijui una kipaji cha chuki nadhani unaishi pangoni pia.
Mkuu Mimi ninaakili zangu I can see,I can analyse things,sipelekwi pelekwi kwa propoganda uchwara Kama unavyopelekeshwa wewe.
 
Ni mengi sana lakini kama kweli wewe uoni ya nini nisumbuke kukutajia. Kumbuka huyu ana miaka mitano amejenga Barabara za viwango kuliko kipindi kingine chote, amehamisha serikali, amejenga Ubungo interchange,amejenge Tazara flay-over, daraja la Salender refu kuliko yote africa mashariki na kati kwa baharini, daraja kwa busisi refu kuliko yote kwenye maziwa africa, Bwawa la nyerere ameanzisha Tarura nk nk.
Mkuu we acha tu ukiyaandika hapa ni mlolongo lakini nina uhakika ukienda kila wilaya kwa sasa lazima uone kitu tofauti kabisa na itabidi tuanze kuvitaja kwa makundi maana kimoja kimoja itakuwani matumizi mabaya ya rasilimali muda.
 
mimi naona kama vile vitu vyote vinafanyika kutokana na ilani ya chama,sidhani kama kuna haja ya kubishana nani kafanya zaidi, nafikiri ndivyo wanavyopokezana vijiti. wangekua wanatoka vyama tofauti hapo mabishano yana ulazima kuwepo, sidhani kama magufuli mwenyewe ashasema jk au bwm hawakuwahi fanya kitu, ila huwa anafanya kulingana na mwongozo na mapendekezo ya chama na mahitaji wa wananchi.
Mtoa hoja hauko serious. Yaani hujawahi kusikia JPM kwenye hotuba zake akiponda watangulizi wake?
 
Nimesikiliza mambo ambayo Rais Magufuli anayasema kuhusu Mkapa binafsi naona Mkapa ni shujaa mkubwa mno wa Taifa hili maana alianzisha mambo muhimu mno mpaka sasa na sisi ambao wengi hatujui tulijua hayo yalianzishwa na Mwl. Nyerere au Mzee Mwinyi kumbe ni Mkapa, pia naona yale maubabe aliyokuwa anayafanya kumbe ilkua ni kwa nia njema kabisa.

Angalia jinsi alivyokuwa ana coordinate uchumi pia naskia alivyoingia madarakani hakuna CHAKULA kiliongezeka bei, binafsi sijui aliemfata madarakani Mzee Kikwete pamoja na kusafiri sana sijui makubwa ya maana aliyoyafanya hapa nchini ni nini hapo ndo napopata akili ya kuwa Rais Magufuli kumbe ameanzia pale alipoishia Mkapa.

Sasa naamini kwa maneno aliyoongea ya sifa tele kwa Mkapa akipita uchaguzi huu tutegemee wananchi kutokuwa na PESA mifukoni hasa wale wasiokuwa na ajira rasmi au shughuli rasmi ya kuingiza kipato na badala yake lazima apige Miradi mikubwa zaidi itakayoacha alama KUBWA kuwa hii iliasisiwa au kufanywa na Magufuli.
Ni kweli uliyosema. Ila Magufuri anaweza haya:-
1. Ni mropokaji kwa kuwa anapoongea hajali kadamnasi imayomsikia. Matusi ya nguoni ndiyo lugha yake ya kawaida.

2. Hapendi upinzani kwa kuwa akiruhusu atashindwa asubuhi. Ndiyo maana katumia hela ya Serikali kuwanunua wabunge wa Kinondoni, Siha na Bahati.

3. Anapenda rushwa na ufisadi ndiyo maana hataki kufanya kazi na CAG aliye nyooka.

4. Ni mwizi wa mali ya umma ndiyo maana kamuweka Katibu Mkuu Hazina ambaye ni mpwa wake. Kwa miaka 4 tayari Tsh 2.4 Trillion hazijulikani zilipo

5. Ni mpenda ukabila kwa kuwa sehemu nyeti zote amejaza ndugu na watu wa Kanda ya ziwa Angalia IGP, DPP, AG, KM-KM-Hazina, RC DSM, Waziri Nishati, CAG mpya, Waziri Viwanda, Jaji Mkuu nk

6. Ni mtu wa kufuja mali ya umma. Angalia ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato na uanzishaji wa mbuga ya Burigi -Chato

7. Amezuia shughuli za vyama vya siasa wakati CCM inafanya mkutano kila mahali. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2000 na Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 zinatambua shughuli za vyama vingi.

8. Hataki watu wajieleze kwa uhuru kadri ya katiba, na amevibana vyombo vya habari. Kwa mfano Eric Kabendera ameanzishiwa shitaka la kutakatisha fedha wakati kiukweli ni maoni yake kwenye gazeti la The Economist

9. Anachukia wenye vyeti feki lakini kamuacha Bashite aendelee kuwa RC DSM wakati naye ana cheti feki. Hata PhD yake yasadikiwa amekopi kwa supervisor wake ambaye kamteua kuwa Katibu Mkuu wa Wizara mojawapo.

10. Ameruhusu kikundi cha wasiojulikana kiteke watu, kuwatesa na wengine kuwaua kama Ben Saanane, Azory Gwanda. Na majeruhi kwa Tundu Lissu

11. Analitawala Bunge kwa remote control. Bunge haiwezi kuhoji chochote kilichofanywa na Serikali.

12. Mahakama nayo iko mfukoni mwake
 
Labda mnaona aibu kumsema Mwalimu, lakini uchumi wa nchi hii ulikuwa umekufa kabisa mwaka 1985

Hivi wewe una habari kuwa mwaka 1985 Mwinyi alichukua nchi uchumi ukiwa unakua kwa NEGATIVE rate (Ulikuwa ukikua kwa -3%).

Hujui kuwa Mwinyi Kachukua hii nchi wakati tukifuata Uchumi wa Kijamaa ambao ulishafeli duniani, na Mwinyi kwa ujasiri akaamua kufanya reforms kwa kuanzisha soko huria!

Hujui kuwa TRA ilianzishwa kisheria na Mwinyi mwaka 1995 kabla ya mkapa kufanya Staffing mwaka 1996

Hujui ni Mwinyi ndiye aliyerudisha vyama vingi?

Hujui Barabara kwa mfano ya Dar Arusha ilijengwa kwa lami kipindi cha Mwinyi?

Ukiwa huna maono unaweza kumlaumu Mwinyi, lakini wakati Mwinyi anachukua nchi hii ilikuwa ni almost failed state, watu ni masikini choka mbaya!
They have eyes but pretend not to see. According to them all good things in this country have been done by either Nyerere, Mkapa and they are going to say Magufuli. Mwinyi, Kikwete and the like seem to do nothing for them, you know why? Because they are not of their caliber.

Sent from my TECNO CA6 using JamiiForums mobile app
 
Nafkir JPM kaanzia alipoishia Mkapa Ila aisee Mkapa ndo kama alianzisha NCHI upya hongera kwa Mkapa ngoja tuone ya JPM na atakae mfata.
Jk kafanya mengi nae pia ila leo ni siku ya Mkapa
 
Wanajamvi salaam

Mpaka Mkapa anafariki mimi nilikuwa naamini viongozi waliopita hawakuwa wamefanya kitu. Niliamini maneno ya viongozi wa awamu ya tano kuwa Marais waliopita hakuna walichofanya zaidi ya ufisadi tu.

Niliamini na kuaminishwa kuwa katika awamu hii ndiyo tumepata mkombozi wa kweli ambaye tunaambiwa watu kama yeye hawazaliwi mara kwa mara anstahili kuongezewa muda wa kuongoza.

Baada ya kifo cha Mkapa ndiyo nimejua kwamba kumbe kuna kiongozi aliyepita anaitwa Mkapa naye alifanya mambo makubwa na hakuongezewa muda.

Kwa maneno yake mwenyewe Rais Magufuli amemwita Mkapa Rais wa wanyonge.

Kumbe Mkapa pia alijenga madaraja na mabarabara,

Kumbe alijenga uwanja mkubwa wa mpira,

Alijenga majengo ya kisasa ya bunge Dodoma,

Kumbe naye alikuwa mpinga ufisadi akaanzisha hadi TAKUKURU,

Kumbe naye alikuwa ametilia mkazo makusanyo ya mapato akaanzisha TRA

Akaanzisha VETA,
Akaanzisha bodi ya mikopo watoto wasomeshwe kwa mikopo,

Akaanzisha MMEM na MMES, MKURABITA

Alianzisha mfumo wa ruzuku kwa vyama vya siasa,

Alisaidia nchi ikasamehewa deni la taifa USD bilioni 3

Alianzisha TCU, NECTA na MEMKWA
Nk nk nk nk

Leo ndiyo nimejua kumbe waliopita nao walifanya kitu tofauti na tunavyoaminishwa, kumbe walifanya vitu vingi na hawakuomba kuongezewa muda.
Kumbe viongozi wazuri walikuwepo na wataendelea kuwepo.

Hakika nilipotoka, tuliaminishwa sivyo, tulidanganywa. Kifo cha mzee Mkapa kimefichua mengi mazuri ya waliopita ambayo yalikuwa hayasemwi
 

Attachments

  • Screenshot_2020-07-29-10-50-03.jpeg
    Screenshot_2020-07-29-10-50-03.jpeg
    73.5 KB · Views: 2
alafu kesho atasahau yote aliyosema,atasema yeye ndiye pekee ameleta maendeleo,usimuamini yule
 
Jamani Magufuli bado yake tano mingine ndo tumpime kwenye mizani hii tunaowapimia wengine
 
Back
Top Bottom