Tusaidie kuielewa hiyo teknolojia mpya na faida zakeKwa kasi hii ya Azam wachina wa Startimes wajiandae kufungasha virago?
Naona Azam media wanazidi kuja kwa kasi leo hii wamezindua minara ya bilioni 50 mikoa 21
Baada ya Dish wamekuja na vya Antenna hawa jamaa wapo vizuri sana naona kwa sasa Wachina wa Startimes wajiandae kisaikolojia tu maana sidhani kama kuna mtu timamu atatumia vile vidubwashwa vyao
Kongole Azam media sasa huku kwa vya Antenna ndo mnaenda kusepa na nyomi ya kijiji
Mi mwenyewe natumia Startimes ukitoa mambo ya ligi ya bongo sioni cha maana Azam.Jamii forums ni sehemu ndogo sana ya maisha yetu. Hiko kisimbuzi cha Star times mnavyokisakama kila siku humu mpaka juzi nikaona takwimu ndio kinachoongoza kwa mbali sana kuwa na watumiaji wengi Tanzania.
EPL Dstv alilipia haki kwa zaidi ya bilioni 100Bilioni 50 kusambaza antena?badala ya kulipia EPL??
Azam bado sana...hawana channels za maana kabisa ...hata channels za south Africa Tu hawana hata moja
Kilichowabeba ni minara ya tbc wanayotumia pia kuhama analog to digital walipewa tenda waoJamiiforums ni sehemu ndogo sana ya maisha yetu. Hiko kisimbuzi cha Star times mnavyokisakama kila siku humu mpaka juzi nikaona takwimu ndio kinachoongoza kwa mbali sana kuwa na watumiaji wengi Tanzania.
Hamna kitu paleUkitoa DSTV king'amuzi kinachofuata kwa ubora ni startimes, kwa upande wa football wako vizuri, series za kizungu, kihindi kichina, kikorea na kituruki wako vizuri kwa upande wa Tamthilia zilizotafsiriwa ingawa mimi sio mpenzi nazo ila The Brothers hainipiti, kwa upande wa michuano ya kimataifa star times inaonyesha ligi nyingi zaidi ya Azam huku mpaka Ronaldo anaonekana,kwa upande wa soka la Africa, wanaonyesha michuano yote inayosimamiwa na caf, Tunaangalia ligi ya kenya, tunaangalia ligi ya Uganda na kwa upande wa Tanzania wameanza na champioshp,