Pre GE2025 Kwa kasi hii ya kurekebisha miundombinu Mbeya, tunatamani Uchaguzi uwe kila Mwaka

Pre GE2025 Kwa kasi hii ya kurekebisha miundombinu Mbeya, tunatamani Uchaguzi uwe kila Mwaka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hizi chaguzi Zina Raha yake jamani,huku Mbeya karibia kila mtaa utakaopita unakutana na Magreda yakiendelea na kazi ya kurekebisha Barabara.

Na hii huwa inatokea kila tuingiapo Kwenye kipindi Cha kuelekea uchaguzi tofauti na kipindi lingine.

Mwanongwa natamani uchaguzi uwe unafanyika kila baada ya miaka miwili naamini kila mtaa utakuwa unapendeza.

Shughuli hizi za kurekebisha miundombinu isiishie kipindi hiki tu Cha kuelekea bali ziwe endelevu kwaajili ya kuimarisha miundombinu ya mitaa yetu.

View attachment 3133988View attachment 3133991View attachment 3133992
Magufuli alifanya bila kusubiri uchaguzi. Hiyo danganya toto.
 
Huku kibaha mjini pwani mtaa wa Lumumba mvua ikinyesha tu shughuli hamna, wamama wajawazito wanakosa huduma kwenda hospitali wengine wanapoteza maisha..Tuwekewe hata kokoto tu kuingilike
 
Hizi chaguzi zina raha yake jamani, huku Mbeya karibia kila Mtaa utakaopita unakutana na Magreda yakiendelea na kazi ya kurekebisha Barabara.

Hii huwa inatokea kila tuingiapo kwenye kipindi cha kuelekea uchaguzi tofauti na kipindi lingine.

Mwanongwa natamani uchaguzi uwe unafanyika kila baada ya miaka miwili naamini kila mtaa utakuwa unapendeza.

Shughuli hizi za kurekebisha miundombinu isiishie kipindi hiki tu cha kuelekea bali ziwe endelevu kwaajili ya kuimarisha miundombinu ya mitaa yetu.

Pia soma ~ Ujenzi wa njia nne Mbeya washika kasi
Heri yenu . Huku kahama Hadi barabara zimflefungwa kwa kujengwa mashine za mpunga , yaani ni kuziba kabisa !
 
Back
Top Bottom