Kwa kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?


Mkuu mengi uliyoyasema miaka hiyo yanadhihiri sasa, changamoto ni zile zile kwa mtizamo huo, Kama hakuna ‘check and balance’ kuna hatari ya kundi au makundi fulani kufaidika na mfumo kwa njia halali au siyo halali na kwa muda mrefu

Pia kuna kundi au makundi ktk jamii yataumia kwa muda mrefu kwa kukosa nilichokieleza pia kihalali ama la

Hapa kuna wanafunzi, wafanyabiashara (wajasiriamali ) na baadhi ya wana siasa ukiwa umekaa ktk upande wa maumivu yanakuwa endelevu mpaka mtu ‘high table’ na kundi la wachache wajisikie vinginevyo

Tutaanza kuishi kutegemea kundi dogo la ndani ya mfumo tu linafurahi na kuudhika vipi na mfumo wao wa ndani amabao utapelekea ukindhani wa ndani yao hapo labda ndo salama yetu na siyo maamuzi yaliyowekwa kwa maandishi kama sheria kuu kwa wananchi wote

Kama nivyosema faida zipo na hasara zipo kwa mfumo tuliochagua inakula kwako vipi itategemea upo upande wa kupata au kupoteza na ubaya wake ni kwa kipindi kirefu tu na hasa kama huo ukomo ukiondolewa
 
Sasa matamwelewa P
 
Kiukweli wapinzani wa Tanzania wanapenda sana kujifurahisha kwa kuingia kwenye uchaguzi ambao wanajua watashindwa, na wakiisha shindwa kweli, kinachofuatia ni baby cry!.
Poleni sana wapinzani, msije kusema hamkujua, mliambiwa kabla!.
P
 
Uchaguzi ulikuwa wa haki na huru?

Umejibu hili?
Mkuu Kiranga, kwa vile wengi wanauzungumzia uchaguzi based on kilichotokea, mimi nimeanza kuuzungumzia zamani na matokeo ya uchaguzi wa 2020, niliishayajua tangu ile 2015 baada ya Jembe JPM, kuingia ulingoni.
Karibu pande hizi
P
 
Kwa hiyo unatetea ubakaji wa demokrasia uliotokea?
Mkuu Kiranga , kwenye uchaguzi huu kuna kambi mbili, the wishful thinkers and the realists. The wishful thinkers wali wish JPM na CCM watashindwa, TL na upinzani watashinda, sasa waliposhindwa kihaki na kikahali, bado wanaamini walishinda wakapigwa, wakaporwa ushindi kwa ubakaji wa demokrasia.

The realists ni wale tuliojua kuwa JPM na CCM, watashinda kwa kishindo, TL na upinzani hauwezi kushinda hata kwa dawa, hivyo iwe isiwe, kwa track record ya JPM, CCM ilikiwa lazima ishinde kwa vyovyote vile, call it what you may, kama kukubali the plain reality ndio kutetea ubakaji wa demokrasia, then be it!.
P
 
I thought people trained innm the law were supposed to stand up for justice and what is right.

Apparently, realpolitik wins.
 
Hao jamaa hawana wanalokubali hata moja kama ni jambo la heri & mafanikio la upande mwingine! Lazima watapaka tope zao na kuonesha huo uchafu kama ndiyo dosari. Miaka 5 iliyopita na kwenye kampeni walikuwa frontline kukashifu maendeleo yote na kueneza sera za matusi na uzushi na ushari na machafuko, hiyo ndiyo mbinu yao ya msingi plus kutengeneza matukio na kuwagombanisha raia na serikali. Hiyo ndiyo kazi wanayoijua na wamefuzu mpaka wamekubuhu!
 
Wanabodi, mimi ni miongoni mwa wana jf, tuliandika mengi kumhusu rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo kipindi hiki cha maombolezo, napitia baadhi ya mabandiko kwa ajili ya kumuaga rasmi.

Japo umetangulia, lakini kauli zako, maono yako na kile ulichokiamini, kitabaki na sisi Milele.
Sisi tulikupenda, lakini Mungu amekupenda zaidi.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele, Umuangazie, Apumzike kwa Amani...Amina x3.
RIP Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Buriani ya kuonana...
Paskali
Wanabodi, mimi ni miongoni mwa wana jf, tuliandika mengi kumhusu rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo kipindi hiki cha maombolezo, napitia baadhi ya mabandiko kwa ajili ya kumuaga rasmi.

Katika bandiko hili la mwezi November, 2015, kuna mstari nilizungumzia kasi ya JPM.

Japo umetangulia, lakini kauli zako, maono yako na kile ulichokiamini, kitabaki na sisi Milele.
Sisi tulikupenda, lakini Mungu amekupenda zaidi.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele, Umuangazie, Apumzike kwa Amani...Amina x3.
RIP Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Buriani ya kuonana...
Paskali
 
Bwana Pascal Mayalla umejikomba kwa miaka 6 na hukuambulia teuzi.
Kwa taarifa yako tangu siku ile ulipomuuliza Magufuli swali lililomuudhi tayari alishakupiga X. Na wewe nadhani hukulijua hili.
Ushauri : Acha unafiki , nchi iko mikononi mwa Mtanzania wa Zhenj. Hawa watu wa Zhenj hawapendi unafiki na kujikombakomba. Fanya kazi accordingly na sio kwa kujipendekeza.
Hivi unajisikiaje ulivyojipendekeza kwa miaka yote hii na umetoka kappa?.
Tulivyokuambia kuwa teuzi utazisikia redioni tu ulijua tunatania?
 
Mwanasheria did you write this?? Dah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…