Kwa katiba hii basi mbunge wangu hana sifa kurudi bungeni!

Kwa katiba hii basi mbunge wangu hana sifa kurudi bungeni!

Mzee Dogo

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2010
Posts
400
Reaction score
140
Vipo vitu vichache ambavo sijavipenda katika rasimu ya pili ya katiba mpya lakini kwa zaidi ya 75% iko vizuri, moja kati ya vitu nilivyovipenda ni kwamba kama ikipita basi angalau tunaweza kupata watunga sheria wanaojua angalau ni nini wanachokifanya kwa kuangalia kigezo cha elimu pale inaposema mbunge awe at least amefika form 4 au zaidi ya hapo. hili likifanikiwa basi mbunge wangu a.k.a Prof. Maji Marefu atakosa sifa za kugombea na huenda tukapata mtu anayejielewa ni nini anafanya huko mjengoni!

Natamani sana sijui hili litokee, sijui wewe Mtanzania mwenzangu...
 
ajiandae nakuloga pia maana yule mganga wa kienyeji ni hatari..
 
Vipo vitu vichache ambavo sijavipenda katika rasimu ya pili ya katiba mpya lakini kwa zaidi ya 75% iko vizuri, moja kati ya vitu nilivyovipenda ni kwamba kama ikipita basi angalau tunaweza kupata watunga sheria wanaojua angalau ni nini wanachokifanya kwa kuangalia kigezo cha elimu pale inaposema mbunge awe at least amefika form 4 au zaidi ya hapo. hili likifanikiwa basi mbunge wangu a.k.a Prof. Maji Marefu atakosa sifa za kugombea na huenda tukapata mtu anayejielewa ni nini anafanya huko mjengoni!

Natamani sana sijui hili litokee, sijui wewe Mtanzania mwenzangu...

Wakifuta form 4 kama walivyo fanya kuleta division 5, kwenye katiba itakuweje?
 
Hivi kwa nini wasingeweka shahada ya kwanza kabisa?? Hizi kazi wakipewa wasomi naamini ni muafaka kabisa.
 
Haha! Weru anaitwa Mbunge .... Mkaazi wa Dar Es Salaam mwaka sasa hatuja muona, Naamini kwa Katiba hii Tungeshampoteza.

Yule wa Jirani Iko Gonjwa Mwaka sasa naye pia Tungeshampoteza.
 
mh.jah people kwa rasmu hii hana sifa maana ni darasa la pili
 
Sugu," Yamenikuta mzee mwenzangu, sina changu,wanga wengi anga zangu, ama zao ama zangu, ukiishi kwa upanga nawe utakufa kwa upanga," form 2.
 
sugu je aliyeishia form 2

Sugu anawafanya mbaya eeh? Kwa taarifa yako,SUGU kamaliza kidato cha 6 na kusomea uongozi huko Marekani baada ya kusimama kuimba hip hop. Wewe endelea mawazo mgando hayo,wenzio wanasonga,maana naona unalala unamuota sugu maana kawashka pabaya kama rais wako ambaye halali kisa Mwanaharakati TUNDU LISU. Limewafika,limewafka tu subiri kuumbuliwa MWAKANI.
 
Natamani haka kasheria kashuke na kwa madiwani, binafsi sina elimu ya kulingishia wasomi na wala sina mpango wa kutaka uongozi wowote but I REAL WANT TO SEE TZ HEADING SOMEWHERE!
 
Ni rasimu ya katiba ya muungano sio katiba ya Tanganyika, ikipita hii itafuata ya Tanganyika na sisi watanganyika tupo bize na maisha huenda wanaojua kututawala wakatengeneza katiba ya kututawala badala ya kutuongoza km wanavyolazimisha muundo wa muungano uwe km wanavyotaka wao na sio matakwa ya wananchi
 
Back
Top Bottom