Kwa katiba hii basi mbunge wangu hana sifa kurudi bungeni!

Kwa katiba hii basi mbunge wangu hana sifa kurudi bungeni!

Vipo vitu vichache ambavo sijavipenda katika rasimu ya pili ya katiba mpya lakini kwa zaidi ya 75% iko vizuri, moja kati ya vitu nilivyovipenda ni kwamba kama ikipita basi angalau tunaweza kupata watunga sheria wanaojua angalau ni nini wanachokifanya kwa kuangalia kigezo cha elimu pale inaposema mbunge awe at least amefika form 4 au zaidi ya hapo. hili likifanikiwa basi mbunge wangu a.k.a Prof. Maji Marefu atakosa sifa za kugombea na huenda tukapata mtu anayejielewa ni nini anafanya huko mjengoni!

Natamani sana sijui hili litokee, sijui wewe Mtanzania mwenzangu...

Inauma sana kuona mbunge wangu mpenda maendeleo anayejali wananchi wake mpaka anahamisha mifugo kinyemela toka kwenye mazizi ya wenzake nakuwapeleka kenya ndugu Lameck Airo a.k.a Lakairo hatorudi bungeni kwani yeye ni darasa la4. Ila nilimshauri asome akakataa.
 
Kama kweli tunataka maendeleo mbunge awe na minimum qualification ya kuwa na degree ya kwanza. Siku hizi vijana lukuki wana degree ya kwanza halafu mnataka wabunge wa form four; heshima ya ubunge iko wapi?
 
Babu alieakuwa msimamizi mkuu wa rasimu ya katiba anadai viongozi wa siasa sijui wafanyakazi wa umma wasiwe na account nje ya nchi. Sasa basi unless mabenki yawe na ulazima wa ku-deposit accounts za watu kwa fedha za kigeni vinginevyo ni moja ya mapendekezo yake mengine ambayo ni vichekesho. Maana hela ya Tanzania ina depreciate kila kukicha, anacho pendekeza ni kwamba mfanyakazi wa serikali aruhusiwi kuchukua precautions with his/her finances, hiwe tabu kwake kuwekeza kwenye international markets with ease, hali kadhalika: governor ajae, waziri wa fedha, waziri wa biashara na serikali ijayo watakuwa na mikakati mizuri sana kutokua na sababu ya watu kutaka kujikinga na currency depreciation. Huyo babu keshakuwa waziri mkuu na ni judge by professional (msomi) ndio kaja na mapendekezo hayo.

Tatizo sio elimu ya mmbunge, tatizo ni wapiga kura unaweza vipi kumchagua mtu ambae asemi anaenda kukusimamia vipi huko mbele wala aombi kura kwa kusema ataenda kuhakikisha local problems are addressed in the parliament hili serikali itungie sera. Yeye anakwambia ntaleta barabara sijui shule kama hivyo vitu havipo kwenye sera za serikali kufika huko na vikaja binafsi naona ni siasa za wizi na influence kuliko sera. On the other hand kila siku budget na sera za serikali zinapita kiulaini bila ya commentary za wabunge ambao wananchi wao wanaenda athirika au kutofaidika na mazingira ya sera. Kosa ni mmbunge au mwananchi ambae hakujua hata huyo jamaa anaemchagua anaenda kumuwakilisha vipi.
 
Namuonea huruma rafiki yangu Komba mpiga usingizi huyu ataondolewa na waliomchagua maana hawawakilishi baki kakodi chumba cha mapumziko bungeni. Oh!!! Lyatonga upo???? Utagombea tena Vunjo???
 
Vipo vitu vichache ambavo sijavipenda katika rasimu ya pili ya katiba mpya lakini kwa zaidi ya 75% iko vizuri, moja kati ya vitu nilivyovipenda ni kwamba kama ikipita basi angalau tunaweza kupata watunga sheria wanaojua angalau ni nini wanachokifanya kwa kuangalia kigezo cha elimu pale inaposema mbunge awe at least amefika form 4 au zaidi ya hapo. hili likifanikiwa basi mbunge wangu a.k.a Prof. Maji Marefu atakosa sifa za kugombea na huenda tukapata mtu anayejielewa ni nini anafanya huko mjengoni!

Natamani sana sijui hili litokee, sijui wewe Mtanzania mwenzangu...

Utashangazwa ifikapo 2015 watakapo ibuka na vyeti fake vya elimu ya sekondari na vyuo nakadhalika.. hapo walipo tu wengi ni vihiyo wanavyeti fake..
 
Kama kweli tunataka maendeleo mbunge awe na minimum qualification ya kuwa na degree ya kwanza. Siku hizi vijana lukuki wana degree ya kwanza halafu mnataka wabunge wa form four; heshima ya ubunge iko wapi?

Ndugu Bulesi hilo wazo lako naomba nilipinge, kwa sasa nchi yetu nadhani haijawa na wasomi wa kutosha wenye shahada kiasi cha kuruhusu hiyo kitu itokee, nafikiri kwa hapa tuliposimama tuwape nafasi pia watu waliofika japo form four ili tuwe na wigompana wa kuchagua. Ungesema kuwa mawaziri wote teuliwa ni lazima wawe at least na Bachelor hapo nitakuwa wa kwanza kukuunga mkono...
 
Utashangazwa ifikapo 2015 watakapo ibuka na vyeti fake vya elimu ya sekondari na vyuo nakadhalika.. hapo walipo tu wengi ni vihiyo wanavyeti fake..

Kama wana Phd feki sembuse form four? Labda siyo Tz na Necta ninayoijua mimi
 
Namuonea huruma rafiki yangu Komba mpiga usingizi huyu ataondolewa na waliomchagua maana hawawakilishi baki kakodi chumba cha mapumziko bungeni. Oh!!! Lyatonga upo???? Utagombea tena Vunjo???

Huyu komba nilimuona siku moja kwenye kipindi fulani maarufu hapa nchini akihojiwa, moja kati ya vitu alivyosema ni kwamba hagombei tena ubunge, labda ayageuke maneno yake kama walivyo wengi wao...
 
Hivi kwa nini wasingeweka shahada ya kwanza kabisa?? Hizi kazi wakipewa wasomi naamini ni muafaka kabisa.

Hapo mwanzo ni nyie mlipomshangaa yule Dr. Kule Kagera kwa kuachana na CCM na kujiunga CDm mkisema anaganga njaa kujiingiza kwenye Siasa badala ya kutoa huduma ya Tiba kwa jamii kwani serikali imemsomesha kwa gharama Kubwa leo hii tena mnasema ili awe Mbunge awe na Shahada je hao pia kuingia kwenye siasa si watakuwa wanaganga njaa?
 
Wabunge wenye elimu ndogo ndo huwa wanaunga kila hoja bungeni... Hata kama wangeleta mswada wa kula mav waweza kuunga hawa wenye IQ ndogo
 
sugu je aliyeishia form 2

Kwa taarifa yako we mburura, Sugu ni f6 aliyefaulu na ana diploma ok. Muulize Amimu Agustino aliyenunua vyeti vya marehemu Philip Mulugo aliyezikwa makaburi ya Mwambene hapa Mbeya mjini
 
Msisahau kuwa hii ni katiba ya JMT katiba ya Tanganyika bado haijatungwa tunapozungumzia katiba hii ni ya wale wabunge 75 tu wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania tu pengine katiba ya Tanganyika inaweza ikaruhusu STD VII kuwa mbunge
 
Elimu ni sawa lakini jambo la muhimu nionavyo ni kuwa hata kama we ni profesa au sijui PHD una msaada gani kwa waliokuchagua? mchango wako kwa jamii ambao umejipambanua ni upi?
 
Kama kweli tunataka maendeleo mbunge awe na minimum qualification ya kuwa na degree ya kwanza. Siku hizi vijana lukuki wana degree ya kwanza halafu mnataka wabunge wa form four; heshima ya ubunge iko wapi?
mkuu kuna wabunge wengi wana madegree halafu bungeni huongea pumba tupu!
 
Kama kweli tunataka maendeleo mbunge awe na minimum qualification ya kuwa na degree ya kwanza. Siku hizi vijana lukuki wana degree ya kwanza halafu mnataka wabunge wa form four; heshima ya ubunge iko wapi?

Wewe umenena mkuu. Form four bado uwezo wa kujenga hoja ni shida walau hata form six ndio ingekuwa kigezo kidogo cha elimu. Form four si ndio hao mjengoni hamna kitu
 
Back
Top Bottom