Kwa katiba hii basi mbunge wangu hana sifa kurudi bungeni!

Kwa katiba hii basi mbunge wangu hana sifa kurudi bungeni!

Ndugu Bulesi hilo wazo lako naomba nilipinge, kwa sasa nchi yetu nadhani haijawa na wasomi wa kutosha wenye shahada kiasi cha kuruhusu hiyo kitu itokee, nafikiri kwa hapa tuliposimama tuwape nafasi pia watu waliofika japo form four ili tuwe na wigompana wa kuchagua. Ungesema kuwa mawaziri wote teuliwa ni lazima wawe at least na Bachelor hapo nitakuwa wa kwanza kukuunga mkono...

Ikitokea 98% ya wabunge waliochaguliwa ni form 4 tutapata mawaziri kweli?
 
Kwa taarifa yako we mburura, Sugu ni f6 aliyefaulu na ana diploma ok. Muulize Amimu Agustino aliyenunua vyeti vya marehemu Philip Mulugo aliyezikwa makaburi ya Mwambene hapa Mbeya mjini

Diploma ya matusi au muziki?
 
Ikitokea 98% ya wabunge waliochaguliwa ni form 4 tutapata mawaziri kweli?

Kaka kumbuka kuna kifungu kinasema mawaziri hawatakuwa wabunge, this means rais atateua watu wenye taaluma ya kada husika. Nafikiri imekaa vizuri
 
Inauma sana kuona mbunge wangu mpenda maendeleo anayejali wananchi wake mpaka anahamisha mifugo kinyemela toka kwenye mazizi ya wenzake nakuwapeleka kenya ndugu Lameck Airo a.k.a Lakairo hatorudi bungeni kwani yeye ni darasa la4. Ila nilimshauri asome akakataa.

kwahiyo ushauri wako ulipotea bure ! Pole sana !
 
mh.jah people kwa rasmu hii hana sifa maana ni darasa la pili

Hahaaaaaaa, bwana tweve nimeshangaa wanamwona prof kina kirefu ndo under-educated kuliko wote hawajui kama kuna jah, hebu shusha cv yake tuburudike hapa, ama kweli ukistaajabu ya omari utaona ya mbuzi
 
Hapo mwanzo ni nyie mlipomshangaa yule Dr. Kule Kagera kwa kuachana na CCM na kujiunga CDm mkisema anaganga njaa kujiingiza kwenye Siasa badala ya kutoa huduma ya Tiba kwa jamii kwani serikali imemsomesha kwa gharama Kubwa leo hii tena mnasema ili awe Mbunge awe na Shahada je hao pia kuingia kwenye siasa si watakuwa wanaganga njaa?

Wewe mbona unakurupuka??!! Mimi nilisema wapi Dr anaganga njaa??
 
Vipo vitu vichache ambavo sijavipenda katika rasimu ya pili ya katiba mpya lakini kwa zaidi ya 75% iko vizuri, moja kati ya vitu nilivyovipenda ni kwamba kama ikipita basi angalau tunaweza kupata watunga sheria wanaojua angalau ni nini wanachokifanya kwa kuangalia kigezo cha elimu pale inaposema mbunge awe at least amefika form 4 au zaidi ya hapo. hili likifanikiwa basi mbunge wangu a.k.a Prof. Maji Marefu atakosa sifa za kugombea na huenda tukapata mtu anayejielewa ni nini anafanya huko mjengoni!

Natamani sana sijui hili litokee, sijui wewe Mtanzania mwenzangu...
Rorya walimkataa Profesa
 
Pamoja na Elimu Kuna mambo muhimu ya kuzingatiwa katika hili suala la ubunge ili wanaochaguliwa wawe wanawajibika kwa wananchi wao ipasavyo

  1. Wananchi wawe na uwezo wa kumfukuza Mbunge 9pale inapobidi kufanya hivyo) within three year tangu kuchaguliwa...ikishapita miaka mitatu basi aendelee kumalizia kipindi cha ubunge. Ukishakuwa Mbunge isiwe ndio tiketi ya watu wengine kupata njia ya kujitarisha/kupatia mitaji ya miradi ya familia zao
  2. Mihula ya ubunge; kuwe na ukomo wa vipindi vya ubunge (vipindi viwili vya miaka 5 vinatosha sana).......kuna watu wamefanya hii nafasi ni ya kwao milele, siku hizi watu wenye uchungu na mamendeleo ya sehemu zao wako wengi....hivyo ukomo wa ubunge utaleta changamoto za kukamilisha maendeleo yanayokusudiwa na mbunge

sina hakika kama hayo masuala yamo kwenye rasimu ya katiba
 
Back
Top Bottom