Kwa Katiba hii mbovu Rais anaweza kuuza mkoa wa Arusha na asihojiwe wala kushitakiwa mahala popote. Tuibadilishe

Kwa Katiba hii mbovu Rais anaweza kuuza mkoa wa Arusha na asihojiwe wala kushitakiwa mahala popote. Tuibadilishe

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Nilimsikia waziri Ndumbaro pale bungeni akisigina manung'uniko na malalamiko ya wamaasai kuondolewa kwenye ardhi yao ya asili Ngorongoro.

Ndumbaro alisema "ardhi siyo ya kabila fulani, ardhi ni mali ya watanzania wote. Kwa mujibu wa katiba ardhi yote iko chini ya rais".

Kwahiyo basi, katiba imempa mhe rais madaraka na mamlaka ya kuamua chochote juu ardhi ya eneo fulani kama ikodishae, iuzwe, ama igawiwe bure kwa wananchi, marafiki wa nje n.k. Hii ni hatari.

Hatuombei atakuja rais kichaa atauza ama kutoa kama zawadi ya birthday ardhi yote ya mkoa fulani kwa nchi ama makampuni ya nje. Na Wala hatoshitakiwa.

Tupate katiba mpya ndugu zangu watanzania.
 
Dada katiba mpya ni makaratasi tu!

Hii iliyopo yenyewe wanaikanyaga na hamna kitu mnafanya!

Ishu hapo ni tamaa na ulafi wa hao viongozi tu! Hawajali maishha ya nyie masikini. Nyie masikini hamna haki ya kuishi sehemu nzuri hizo ni kwa ajili ya matajiri kina Ritz 1 na the like,

Na mkome, maana Magufuli aliposema yupo kwa ajili ya kutetea wanyonge mkawa mnakuja mnabinua matakle humu kila siku mnaanzisha thread kwamba nyie sio wanyonge!

Tena muache kutupigia kelele kabisa hasa nyie mabavicha.

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Raha ya Katiba yetu Pendwa ni hii.

Inaweza kukupa hata urais hata kama huutaki au hata hujawahi hata kuuomba.

Na inaweza kukunyima Urais hata kama ulijiandaa for more than 20yrs.

Dunia ina siri nyingi sana hasa Tanzania
 
Hili nalo ni neno, masai hana thamani kwenye ardhi yake ambayo amerithi kutoka vizazi, mwindaji kutoka nchi nyingine mwenye pesa zake ndo anaonekana mtu muhimu wa kumilikishwa ardhi.
 
Nilimsikia waziri Ndumbaro pale bungeni akisigina manung'uniko na malalamiko ya wamaasai kuondolewa kwenye ardhi yao ya asili Ngorongoro...
Na ukimuuliza anaweza kuamua kukupoteza au kukufunga kifungo cha maisha.
 
Nimecheka Sana hili neno Matakle

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mleta mada ni mpumbavu sana. Halieleweki linasimamia kitu gani.!

Hebu wewe dada mleta mada mwambie huyo rais wako muwazi sana kuwahi kutokea akuweke wazi hata kinachoendelea ngorongoro basi,
20220221_082536.jpg

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Hili nalo ni neno, masai hana thamani kwenye ardhi yake ambayo amerithi kutoka vizazi, mwindaji kutoka nchi nyingine mwenye pesa zake ndo anaonekana mtu muhimu wa kumilikishwa ardhi.
Rais muwazi sana kuwahi kutokea kwa mujibu wa mleta mada
20220221_082536.jpg

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Dada katiba mpya ni makaratasi tu!

Hii iliyopo yenyewe wanaikanyaga na hamna kitu mnafanya...
Ukipona kichaa utaelewa kuwa kwanini katiba mpya ni muhimu acha ushamba katiba mpya na Bora sio kwa Wana chadema katiba mpya na Bora ni kwa ajili ya taifa zima na wananchi wake wote ukiwepo na wewe mpuuzi mmoja.

Nikukumbushe tu kuwa katiba ya iliyopo inakanyagwa sana kwa sababu hakuna sehemu imejilinda isikanyagwe zaidi imempa mwenye mamlaka kufanya atakavyo kwa kifupi katiba iliyopo ni Kama imeruhusu utashi wa mwenye mamlaka bila kumpa onyo lolote
 
Nilimsikia waziri Ndumbaro pale bungeni akisigina manung'uniko na malalamiko ya wamaasai kuondolewa kwenye ardhi yao ya asili Ngorongoro.

Ndumbaro alisema "ardhi siyo ya kabila fulani, ardhi ni mali ya watanzania wote. Kwa mujibu wa katiba ardhi yote iko chini ya rais"...
Tulikuwa na kichaa awamu ya Tano. Ambaye alikuwa anaamua tu maendeleo sipeleki Mbeya kwa sababu mmemchagua mpinzani alafu Kodi za mbeya anapeleka chato.
 
Tulikuwa na kichaa awamu ya Tano. Ambaye alikuwa anaamua tu maendeleo sipeleki Mbeya kwa sababu mmemchagua mpinzani alafu Kodi za mbeya anapeleka chato.
Unaonaje sasa hivi baada ya kichaa wako kuondoka jinsi mnavyogawiwa maendeleo na kushirikishwa kila amuzi linalofanyika.

Unaonaje pia hata maendeleo wanayopata watu wa Roliondo baada ya kichaa wako kuondoka.?

Nasikia baada ya kichaa wako kuondoka umasikini wako umeisha maana hangaya kakuletea maendeleo kila kona

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Ukipona kichaa utaelewa kuwa kwanini katiba mpya ni muhimu acha ushamba katiba mpya na Bora sio kwa Wana chadema katiba mpya na Bora ni kwa ajili ya taifa zima na wananchi wake wote ukiwepo na wewe mpuuzi mmoja, nikukumbushe tu kuwa katiba ya iliyopo inakanyagwa sana kwa sababu hakuna sehemu imejilinda isikanyagwe zaidi imempa mwenye mamlaka kufanya atakavyo kwa kifupi katiba iliyopo ni Kama imeruhusu utashi wa mwenye mamlaka bila kumpa onyo lolote
Wewe ndio kichaa kama huwezi kuona hata vitu vidogo tu!

Hii katiba haijaruhusu hayo mnayolalamikia kufanyika!

Hata hiyo mnayotaka mpya ikija wakiamua wataikanyaga tu na hamna kitu mtafanya, maana hii iliyopo imekanyagwa na mmezubaa tu!

Kama huwezi kuheshimu kidogo huwezi kuheshimu kikubwa.

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Dada katiba mpya ni makaratasi tu!

Hii iliyopo yenyewe wanaikanyaga na hamna kitu mnafanya...
Hamna mtetezi wa wanyonge anapora korosho zao. Usidhani tulikuwa tunasikiliza porojo zake, tulikuwa tunaangalia matendo yake. Yule alikuwa nusu shetani na sio mtetezi wa wanyonge.
 
Hii iliyopo yenyewe wanaikanyaga na hamna kitu mnafanya!
Inakanyagwa kwasabb siyo Bora. Katiba bora huwa Ina mifumo ya kujilinda ili isikanyagwe. Na yeyote anayethubutu kuikanyaga huathibiwa na katiba
 
Bora kuuzwa marekani ili tuwa chini yao maisha yabadilike
 
Nikukumbushe tu kuwa katiba ya iliyopo inakanyagwa sana kwa sababu hakuna sehemu imejilinda isikanyagwe zaidi imempa mwenye mamlaka kufanya atakavyo kwa kifupi katiba iliyopo ni Kama imeruhusu utashi wa mwenye mamlaka bila kumpa onyo lolote
Comment yako ifanyiwe lamination na kuwekwa kwenye bango kubwa kama la mume wa Zamaradi
 
Back
Top Bottom