Kwa kauli hizi ni kweli Kiba anabaniwa

Kwa kauli hizi ni kweli Kiba anabaniwa

Kijana siri ya mtungi haya mambo ni makubwa sana hili bifu lisipo patanishwa watatiana ukilema hawa watu na yote ni team wema
Hafu nikuambie kitu hizi media za bongo zote diamond platinum akienda kwenye interview anasema asiulizwe swali kuhusu wema wala ali kiba kama huamini fuatilia interview zake vizuri ni kama gadner na lady jaydee

Japokuwa hill bifu naona kama limeisha halina hype kama iliyokuwa mwaka jana mwezi wa saba, sita hivii kurudi nyuma.. Jinsi Diamond anavyozidi kupata mafanikio nguvu ya kuwashindanisha mashabiki inaisha, kinabaki majungu tu

Diamond hataki kumuongelea kiba popote pale maana kila atapomuongelea itazua mjadala, kitu kilicho tofauti kwa kiba yeye anamuongelea sana diamond na ni moja ya vitu vinavyokuza hii bifu pamoja na wema kuingilia kati kutoa vimaneno vya shombo hivii..

Upande wa mashabiki maneno maneno kuwepo ni kitu cha kawaida, maana bila umbea, fitna, matusi mitandao hasa insta huko kama hakuendi hivii
 
Icon wa Bongo flava Naseeb ‘Diamond’ Abdul, amewashangaa wasanii wanaomtupia maneno kila kukicha kuwa anawabania wasanii wengine ‘connections’ za kung’ara kimataifa.

Akizungumza na TBC juzi, Platnumz amesema anasikitishwa sana na maneno hayo ilhali anafanya juhudi kubwa kujitafutia na kuwatafutia wasanii wengine masoko ya kimataifa.

“Mi nashangaa sana kusikia hayo maneno, wanasema hivyo wakati mi najitahidi kuwasaidia wenzangu tutoboe wote, kila kolabo ya msanii wa nyumbani na msanii wa Nigeria inayofanywa mi ndo huwa nasababisha.” alisema Diamond

“Nikiamua kubana mbona naweza tu, kwa sababu vituo vingi vya nje vinanisikiliza kwa mfano tu MTV wenyewe wakipokea video ya msanii yoyote kutoka hapa (Tanzania) wananipigia wananiuliza kwanza huyu vipi? tuicheze ngoma yake au? mi huwa nasema tu anafanya vizuri huku, basi inapita wanaicheza nikiamua kubana si naweza tu?”

Katika ‘line’ nyingine, baba Tiffah amesema timu yake ya Wasafi ndiyo iliishauri kituo cha tv cha Nigeria Sound City na MTV kuanzisha chati za Afrika Mashariki kwenye vituo hivyo.

Chanzo: Timesfm
Kwa hiyo diamond ndio executive director wa MTV kiasi kwamba hawarushi wimbo bila ithini yake sio???
 
Naamini katika uwezo wake wa kujitangaza mbali, BUT katu hana uwezo wa kuamua nani atoke na nani asitoke. Hiyo nakataaa
 
Hivi mbona watanzania ni wavivu sana wa kutafuta maarifa? hivi hizo smartphone mnazozitumia mnashindwa hata kutafuta maarifa juu ya swala dogo tu la kufatilia mfumo mzima unaotumiwa na mtv base africa ili kucheza video kwenye tv zao...kwa kifupi Diamond hana uwezo wa kupigiwa simu aulizwe huyu mtu vipi sababu itakua kuna mgongano wa maslahi maana nae ni msanii anaweza kutumia huo mwanya kuwabania wasanii toka Tanzania MTV haiendeshwi kijinga hivyo, pia diamond hayupo kwenye panel ya mtv inayokaa kuireview video wiki 3-4 baada ya video kua submitted kwao...hao mtv kwa kifupitv base wana criteria zao za kuichuja video google hili neno "mtv base africa video submission guidelines" watanzania wamefichwa kwenye ujinga mkubwa sana...
 
Mi nahisi alijibu hivyo kama dhihaka tu,wala hakuwa anamaanisha,kwa sababu kumekuwa na maneno mengi sna yakisemwa kuwa kuna watu wanafanyiwa fitna video zao zisichezwe uko nje au wasipatiwe tuzo,sasa ndo kama vile anawajibu kwa kibase..."ndio kwa sababu mimi ndio ninashauriwa kwanza kabla nyimbo ya mbongo haijachezwa mtv,ndo maana za wengine hazichezwi kwa sababu zimekosa viwango"..ili wazidi kuongea wenye kujua kuongea
 
Hivi mbona watanzania ni wavivu sana wa kutafuta maarifa? hivi hizo smartphone mnazozitumia mnashindwa hata kutafuta maarifa juu ya swala dogo tu la kufatilia mfumo mzima unaotumiwa na mtv base africa ili kucheza video kwenye tv zao...kwa kifupi Diamond hana uwezo wa kupigiwa simu aulizwe huyu mtu vipi sababu itakua kuna mgongano wa maslahi maana nae ni msanii anaweza kutumia huo mwanya kuwabania wasanii toka Tanzania MTV haiendeshwi kijinga hivyo, pia diamond hayupo kwenye panel ya mtv inayokaa kuireview video wiki 3-4 baada ya video kua submitted kwao...hao mtv kwa kifupitv base wana criteria zao za kuichuja video google hili neno "mtv base africa video submission guidelines" watanzania wamefichwa kwenye ujinga mkubwa sana...
Wee ndomjinga kwel usiropoke bila evidence, asa apo ndounajiona mjuaji tz nzima!! Mwehu kwel ingia youtube tafta interview ya millardayo na chege umsikie akiongea nafasi ya diamond ukitaka kufaamika nje
 
Elewa ninachobisha mimi ni kwamba Diamond lazima aulizwe kabla ya video ya msanii yeyote wa Tanzania kupigwa MTV Base, tatizo hujasoma nini MTV Base Submission guidelines ndo mana unaongea kishabiki, Diamond ana influence yale kama ilivyokua kwa AY hilo halina ubishi hauwezi kuamini maneno ya chege kama video yako haina 50MB/rate, sio HD, haipo kwenye Mov format na haijapita kwenye panel review ya MtV base video haitapigwa milele...aiseee ndo mana shauri zao baada ya kutoka Tanzania ilichukua wiki 2 mpaka 3 kupigwa MTV Base Africa....ujinga umekukithiri...soma submission guidelines hizo halafu urudi na ujinga wako....
 
Kuna siku diamond huwa anateleza kama alivyoongea hivo,,, influence anayo as A list star in Africa, ila sio kwa hivo alivyoeleza maana nasema nawe wangecheza, Salima wangecheza ila zote zilipigwa kapuni hazikugusa Trace, wala MTV...

Infact hakuna msanii yeyote Africa wala kutoka nje mwenye nguvu ya namna hii..
 
Mimi siwezi kuamini hayo maneno mpaka utuwekee Video au audio clip hapa tuone au kusikia wote. Tushachoka na hizi habari za kutungatunga tu bila ushahidi wowote kama huna uthibitisho nenda kalale usituletee uongo. Maana naona umeandika jarida reeefu lakini maneno matupu sisi tutakuami vipi? Labda unatunga tu kwa chuki zako binafsi.
 
Back
Top Bottom