econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Wadau nimeshanganzwa sana na kauli ya Waziri mwenye dhamana ya sheria na katiba.
Nilitarajia waziri huyu angekuwa bega kwa bega na wananchi wanaotaka katiba mpya kwani ni haki yao, kauli hii ya Waziri ni kauli ya Serikali na kama ni ya Serikali basi hata Rais anahusika.
Nipende kuchukua nafasi hii kuwataka viongozi wa CHADEMA waachane na maridhiano na CCM kwani kama waziri wa sheria anakuja na kauli hizi ni wazi CCM haina nia njema na katiba mpya.
Wananchi ndio wenye katiba wananchi walitoa maoni na mapendekezo yao kwa tume ya warioba jinsi wanavyotaka katiba yao iwe hao wabunge watakataaje katiba ya wananchi?
Waliokataa pendekezo la katiba ya warioba ni CCM na wabunge wake kwani hawataki katiba mpya, suala la katiba mpya kutokumaliza changamoto sio hoja kwani katiba iliyopo imemaliza au ndio imeongeza na kuleta changamoto?
Suala la changamoto lipo tu halikwepeki kwani hata Biblia na Quran zina changamoto.
CHADEMA maridhiano yenu na CCM hayana tija wenzenu hawataki katiba mpya.
View attachment 2597754View attachment 2597755
Sio CHADEMA ni Mbowe ndio anazingua. Tukimpata Mwenyekiti mpya tutarudi kwenye mstari. Sio huyu Mbowe ambaye analazimisha urafiki wake na Samiah uwe wa chama. I hate that.