Kwa kauli za Mbowe na Mdude ni wazi Ole Sabaya ataachiwa huru

Kwa kauli za Mbowe na Mdude ni wazi Ole Sabaya ataachiwa huru

Dam55

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
5,641
Reaction score
11,958
Ni suala la muda tu na kujipa subira kidogo tutajionea kwa macho yetu Mungu akitupa uzima.

Jana tulishuhudia mh. Mbowe akitamka kauli tata zenye vitisho na amri dhidi ya Rais wa nchi.

Swali jiulize kama Rais wa nchi anatamkiwa maneno kama yale hadharani je vipi kuhusu mkuu wa wilaya tena pale nyumbani kwake Hai hali ilikuwaje kwake?

Matusi mangapi aliyoyaoga Sabaya ikiwa tu Rais wa nchi haheshimiwi hata kidogo?

Ukiangalia kauli za Mdude CHADEMA eti alimnyoa mwendazake na sasa atamnyoa mama akileta jeuri hapo utajiuliza alimyoaje mwendazake na huyu mama nae atanyolewa vipi?

Yeye ndio alimtoa madarakani kwa kumnyoa hadi kufa sivyo?

Ni kipi hasa mama anachotakiwa kumtii mdude/mnyoaji kwa heshima zote ili asinyolewe?

Ni wazi kuongoza watu wa namna hii inahitaji kiwango cha juu sana chauvumilivu.
Ukiunganisha matukioa ya kesi ya Sabaya.
Kuachiwa Mdude.
Kutumbua baadhi ya watumishi wa enzi za JPM.
Kufutwa kwa kesi ya Mbowe na wenzake utagundua kuwa ulikiwa mkakati maalumu wa mama kutaka kuwaridhisha wapinzani kwa kuwapa matumaini ya utawala mpya lakini kwa hiki wanachokifanya kwasasa hata ile kafara ya Sabaya iliyotaka kutolewa Kama sadaka ya kuwatuliza muda si mwingi itaghairishwa.
Kesi ya huyu mtu imekaa kisiasa sana na nguvu kuwa sana inatumika dhidi yake kutoka fulani wenye hasira na visasi vikubws ndani ya mioyo yao kuliko uhalisia wa aliyo yatenda.

Nadhani sasa mama Kesha wajua vizuri watu aliotaka kuwafurahisha ni watu wa namna gani.

Tujiandae Sabaya kuwa huru hivi karibuni kafara yake imekataliwa.
 
Hapa unamaanisha serikali huingilia maamuzi ya mahakama, nakubaliana nawe, lakini jambo hili linatakiwa kupigwa vita na kila mpenda nchi.

Kwa kauli zenu mnaonesha dhahiri mnavyoingiza siasa kwenye kesi iliyoko mahakamani kwa ajili ya uamuzi, sijaona uhusiano wa kauli ya Mdude na suala la Sabaya lililoko mahakamani, bado nioneshe vizuri.

Mwisho kabisa, kesi ya Sabaya imeshaonesha muelekeo mbaya pale wanapokuwepo "vibaraka" wa kumshangilia nje ya jengo la mahakama kwa lengo la kumfanya aonekane "shujaa" wenu, hapa usisingizie kauli aliyoitoa Mdude jana.
 
Screenshot_20210702-125102_millardayo.jpg

mwanzo mzuri sabaya anatoka hakuna shahidi atakae kubali ujinga wa kwenda kujidharirisha kwa kesi ya kubumba
 
Unamaanisha serikali huingilia maamuzi ya mahakama, nakubaliana nawe, lakini jambo hili linatakiwa kupigwa vita na kila mpenda nchi.
Upo sahihi mkuu ni ukweli ulio wazi mahakama zinafanya kazi kwa maelekezo maalumu kutoka juu kwa maslahi fulani fulani ambayo yanaweza umiza wachache ama wengi kulingana na wakati husika.

Jk alizitumia mahakama kukomesha fujo ( kumbuka mashekhe wa uamsho),JPM alizitumia mahakama kukamata majambazi yanayofanya kazi zao kwa akili kubwa bila kukamatwa mfano wauza madawa kwa kuwawekea kwa makusudi kisha kuwakamata.

Pia alizitumia mahakama kukataa kukosolewa mfano kesi za uchochezi, uhujumu uchumi n.k Sasa huyu mama yeye anatumia mahakama hizo hizo kutaka kutafuta kupendwa na uungwaji mkono kwa kuachia watu na kutoa sadaka wengine.
 
Upo sahihi mkuu ni ukweli ulio wazi mahakama zinafanya kazi kwa maelekezo maalumu kutoka juu kwa maslahi fulani fulani ambayo yanaweza umiza wachache ama wengi kulingana na wakati husika....
Mahakama hazitakiwi kutumiwa kisiasa, kesi ipelekwe mahakamani ushahidi upatikane mtu ahukumiwe kutokana na makosa yake, sio vinginevyo, hivyo usitake Sabaya aachiwe kwasababu ya kauli ya Mdude unakosea.
 
Kama mama alikuwa ana mpango wa kukutana na wapinzani itakuwa ngumu Sana Kwa kauli ya Jana aliyoitoa mbowe!!!
Kwa kifupi mbowe amekosea Sana kupiga mikwala ya kishamba ya kudai katiba mpya Kwa kuingia barabaran.... kipindi cha mwendazake mbowe alitulia Tu
 
Ni suala la muda tu na kujipa subira kidogo tutajionea kwa macho yetu Mungu akitupa uzima.

Jana tulishuhudia mh. Mbowe akitamka kauli tata zenye vitisho na amri dhidi ya rais wa nchi.

Swali jiulize Kama rais wa nchi anatamkiwa maneno kama yale hadharani je vipi kuhusu mkuu wa wilaya tena pale nyumbani kwake Hai hali ilikuwaje kwake?
Sawa, tuseme Sabaya anaweza kuachiwa kwa kile unachoamini huenda alikuwa anararuriwa kweli kweli na Mbowe!!!

Kwahiyo na zile kesi za uhujumu uchumi zinazomhusu Sabaya na zenyewe zimetokana na "kuraruriwa raruriwa na Mbowe", au?!
 
Ni suala la muda tu na kujipa subira kidogo tutajionea kwa macho yetu Mungu akitupa uzima.

Jana tulishuhudia mh. Mbowe akitamka kauli tata zenye vitisho na amri dhidi ya rais wa nchi...
endelea kuchochea ila mtambue MHUTU wenu keshanyofolewa na harudi milele
 
Back
Top Bottom