Kwa kauli za Mbowe na Mdude ni wazi Ole Sabaya ataachiwa huru

Sawa mkuu, ni kwanini mbowe na wenzake wameachiwa ikiwa mahakama hizitumiki kisiasa, vipi kesi ya huyo mdude? Umesahau kesi za kina Abdul Nondo na Eric kabendela? Unakumbuka kesi ya Sugu?
Kwahiyo JPM hakuwabambikia watu kesi ila tu zilikuwa porojo za kisiasa tu?.
Binafsi naamini hao jamaa waliachiwa kwasababu hapakuwa na ushahidi wa kuwatia hatiani wahukumiwe vifungo gerezani, lakini kwa Sabaya na ushahidi uliotapakaa kila mahali dhidi yake, sioni ni kwa namna gani atapona, tuiache mahakama ifanye kazi yake na mashahidi wa kesi yake wasibughudhiwe kwa namna yoyote.
 
Wanachopigania Chadema & co ni kuondoa haya uliyaorodhesha hapa chini 👇 👇 yasitokane na utashi wa rais aliyeko madarakani bali yatokane na mwongozo wa katiba.

Wakati wa kudai katiba yao, Wakenya walikuwa na mashinikizo na kauli kali na mbaya dhidi ya serekali yao zaidi hata ya hizi za huku Tanzania. Matokeo yake? Wakenya wamepata moja ya katiba bora kabisa barani Africa ambayo mathalani leo hii nimeona kwenye newsstreams nyingi rais wao yupo mahakamani akiwa amekata rufaa dhidi ya hukumu aliyopewa na mahakama.
Ni kweli mkuu na mimi wala sipingi katiba mpya na lakini pia sikubaliani na matamshi ya hivi kuyapa uhalali wa kuwa ndio njia ya kudai katiba.
Mfano wa wakenya si lazima na sisi tuutumie, utajiuliza Kenya kila uchaguzi lazima wauane je na sisi tuige njia hiyo pia ndio haki itendeke?

Kwa upande wangu naona hapana bali tunaweza kukaa meza moja na majibu yakapatikana vizuri tu bila kuandamana na kumwaga damu za watu wasio na hatia.

Kingine maoni yangu niliyo yatoa hapo ni kulingana na hali ya kisiasa kwa sasa ilivyo, rais anauwezo wa kutumia mahakama kuumiza watu ama kufurahisha watu.
 
Binafsi naamini hao jamaa waliachiwa kwasababu hapakuwa na ushahidi wa kuwatia hatiani wahukumiwe vifungo gerezani, lakini kwa Sabaya na ushahidi uliotapakaa kila mahali dhidi yake, sioni ni kwa namna gani atapona, tuiache mahakama ifanye kazi yake na mashahidi wa kesi yake wasibughudhiwe kwa namna yoyote.
Sawa mkuu, ila nadhani kuwa wewe ni wakwanza kuamini kuwa hawa hawakubambikiwa kesi.
Sawa ngoja tusubiri.
 
Hapa unamaanisha serikali huingilia maamuzi ya mahakama, nakubaliana nawe, lakini jambo hili linatakiwa kupigwa vita na kila mpenda nchi.

Kwa kauli zenu mnaonesha dhahiri mnavyoingiza siasa kwenye kesi iliyoko mahakamani kwa ajili ya uamuzi, sijaona uhusiano wa kauli ya Mdude na suala la Sabaya lililoko mahakamani, bado nioneshe vizuri.

Mwisho kabisa, kesi ya Sabaya imeshaonesha muelekeo mbaya pale wanapokuwepo "vibaraka" wa kumshangilia nje ya jengo la mahakama kwa lengo la kumfanya aonekane "shujaa" wenu, hapa usisingizie kauli aliyoitoa Mdude jana.
Mahakama ni kama bendera na serkali ni upepo

USSR
 
Ni kawaida sana mtu aliyeumizwa, kuonewa au kupigwa kutoa kauli zisiofaa kwakuwa Kisaikolojia wanakuwa bado hawapo sawa kutokana na maumivu waliyoyapitia.

Wote tunajua kadhia waliyopitia viongozi wa Chadema kwa kipindi chote cha miaka 6. Hivyo sishangai kusikia hizi kauli zao.

Kuna ulazima wa Rais akutane nao kama alivyoahidi kisha awatulize wafanye Siasa kwa amani.
Rais asiseme tena yeye na mtangulizi wake kuwa wao ni kitu kimoja.
 
Kwahiyo ni haki yao kutoa kauli za hivyo?
 
Nafurahi sana kukuona hapa mkuu salama lakini.

Mimi nimetoa maoni yangu kutokana na upepo wa kisiasa unaovuma kwa sasa ila hayo unayo yasema wewe ni matarajio yako ambayo ulitegemea kuyaona maybe yanaweza kuja ama yasije kabisa ila viashiria vilivyopo kwa sasa vinaonyesha hali iko hivo na ndicho hasa mimi nilicho kuzungumza.

Au labda unambie kuwa kwa sasa mahakama zinatenda haki haziwezi tena kutumiwa na mkulu kwa manufaa ya kisiasa Kama alivyokuwa hapo awali mana tunaamini watu walibambikiwa kesi kisiasa tu?

Nadhani umeuona vizuri msingi wa mada yangu mkuu, jiulize kabla ya kauli za wiki hii ni vitu gani alifanya mama vilivyopelekea kusifiwa sana kila kona na leo kwanini kageukwa?

Mama alisifiwa kwa kutenda haki baadhi ya sehemu, lakini iliwekwa wazi kuwa hatutaki utawala wa hisani bali tunataka utawala wa sheria, na huo ni ndani ya katiba mpya. Ni kipi ulikuwa huelewi hapo?
 
Screenshot_20210702-125102_millardayo.jpg

mwanzo mzuri sabaya anatoka hakuna shahidi atakae kubali ujinga wa kwenda kujidharirisha kwa kesi ya kubumba
 
Kwahiyo ni haki yao kutoa kauli za hivyo?
Ndio ni haki yao kuongea hivyo.
Kumbuka hizi kauli zao zimesababishwa na kauli alizoongea Rais Juzi kuhusiana na Katiba mpya na shughuli za Siasa.

Kumbuka hawa Chadema ni waathirika wa utawala wa Magufuli. Na kauli za Rais bado zinaendeleza maumivu yao badala ya faraja kwao, Ndio maana unawaona wamepaniki na kuongea hivyo.

Kule Bungeni 99% ni CCM watupu hivyo hiki ni kipindi kizuri sana kwa wabunge wa CCM kupitisha katiba kule Bungeni, maana wapo wenyewe tupu.
 
Hizo kauli zinazokuumiza leo zimekuwa zikitolewa hadharani na yule rais muovu pamoja na genge lake, lakini wakati huo ulichekelea ukisema nchi inanyooshwa. Leo wengine wanaonyesha hisia zao kwa mateso waliyopatiwa kwa uonevu, unaona wanakosea!

Ni hivi, kama kweli huyo rais unataka tuone hiyo nguvu yake, sio kumtaka achukue hatua dhidi ya wapiga maneno ya siasa maana hayana madhara kwetu, bali mtake achukue hatua ya upotevu wa 24b zilizopotea kwenye halmashauri ya jiji la Dar, ama achukue hatua kwa hao waliojiunganishia bomba la mafuta. Sasa mnaacha kumpima rais kwa mambo ya msingi, mnamjaza muone nguvu zake dhidi ya kauli za wahanga wa utawala wa kihayawani wa Magu!?
 
Mm nashauri mama aachane na hawa wapinzani uchwara na hata asikutane nao.

Hata hivyo vikao vya ndani piga marufuku. Hawa wapinzani uchwara wabatufanya tuone matendo haram ya jiwe kua yalikua sahihi. Wanampiga mkwara mama? Stupidity kabisa.
 
Swala la katiba mpya rais kusema kwamba apewe muda ashughulikie uchumi kwanza sio sahihi kwani inaonekana ni mbinu tu ya kupoteza muda ili 2024 aje aseme muda umeisha tusubiri baada ya uchaguzi.

Ni aibu kubwa sana kwa chama kilichokaa madarakani kwa "Silver Jubilee" nzima kuogopa katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi na kutegemea katiba yao wenyewe eti ndio iwabebe kubaki madarakani.

Kwa hiyo ccm inakiri kwamba haina ubavu wa kupambana na wapinzani wake kwenye uwanja ulio sawa na kwamba wenyewe lazima wabebwe tu ili wabaki madarakani. This is very stupid and naive.
 
Ni suala la muda tu na kujipa subira kidogo tutajionea kwa macho yetu Mungu akitupa uzima.

Jana tulishuhudia mh. Mbowe akitamka kauli tata zenye vitisho na amri dhidi ya Rais wa nchi.

Swali jiulize kama Rais wa nchi anatamkiwa maneno kama yale hadharani je vipi kuhusu mkuu wa wilaya tena pale nyumbani kwake Hai hali ilikuwaje kwake?

Matusi mangapi aliyoyaoga Sabaya ikiwa tu Rais wa nchi haheshimiwi hata kidogo?

Ukiangalia kauli za Mdude CHADEMA eti alimnyoa mwendazake na sasa atamnyoa mama akileta jeuri hapo utajiuliza alimyoaje mwendazake na huyu mama nae atanyolewa vipi?

Yeye ndio alimtoa madarakani kwa kumnyoa hadi kufa sivyo?

Ni kipi hasa mama anachotakiwa kumtii mdude/mnyoaji kwa heshima zote ili asinyolewe?

Ni wazi kuongoza watu wa namna hii inahitaji kiwango cha juu sana chauvumilivu.
Ukiunganisha matukioa ya kesi ya Sabaya.
Kuachiwa Mdude.
Kutumbua baadhi ya watumishi wa enzi za JPM.
Kufutwa kwa kesi ya Mbowe na wenzake utagundua kuwa ulikiwa mkakati maalumu wa mama kutaka kuwaridhisha wapinzani kwa kuwapa matumaini ya utawala mpya lakini kwa hiki wanachokifanya kwasasa hata ile kafara ya Sabaya iliyotaka kutolewa Kama sadaka ya kuwatuliza muda si mwingi itaghairishwa.
Kesi ya huyu mtu imekaa kisiasa sana na nguvu kuwa sana inatumika dhidi yake kutoka fulani wenye hasira na visasi vikubws ndani ya mioyo yao kuliko uhalisia wa aliyo yatenda.

Nadhani sasa mama Kesha wajua vizuri watu aliotaka kuwafurahisha ni watu wa namna gani.

Tujiandae Sabaya kuwa huru hivi karibuni kafara yake imekataliwa.
Mwachieni tukutane kitaa akiwa sio DC atajua kuwa haajui mamaeeee
 
Mama alisifiwa kwa kutenda haki baadhi ya sehemu, lakini iliwekwa wazi kuwa hatutaki utawala wa hisani bali tunataka utawala wa sheria, na huo ni ndani ya katiba mpya. Ni kipi ulikuwa huelewi hapo?
Nadhani mkuu wewe ndie ambaye hukunielewa tangu kwenye mada hapo juu na ndio mana nikarudia tena maelezo hayo.

Alafu pia ni ukweli usio pingika kuwa uungwaji mkono na kusifiwa alikosifiwa mama kulitokana na hisani hiyo hiyo unayo ikataa kwa kuzitumia mahakama kufuta kesi za wanasiasa ambazo iliaminika na watu kuwa zilibambikwa pamoja na nyingine nyingi ili kufurahisha makundi kadha wa kadhi, mfano kundi la dini e.g mashekhe wa uamsho, kwa wafanya biashara watu Kama kina Papaa Musofe wako huru, wanasiasa ndio kabisaa kina Mdude, Mbowe na wenzake hawa yote yamefanyika lengo moja tu kurudisha imani iliyo potea enzi za mtangulizi wake wakiamini hawajatendewa haki.

Na ndio mana nasema kwa mawazo yangu hata huyu Sabaya pia yupo ndani ya kimbunga hiki hiki cha kutafuta imani ila tu yeye amekuwa mbuzi wa kafara tena ukizingatia katokea pale pale sebuleni kwa Mbowe, huyu Sabaya ni adui wa pili wa Mbowe baada ya marehemu. Kwangu mimi binafsi kinacho mkuta huyu ni mbinu tu ya kutuliza hali ya hewa.

Ni kweli tunadai katiba lakini si kwa njia ya kumpa amri rais na vitisho vya kunyolewa kwa hapo hatuwezi kufika mkuu.
Na hata hizo hisani hatuta ziona tena badala yake itatumika dola Kama nyakati zilizopita tu na nasema hata huyu Sabaya atakuwa huru muda si mwingi.

Okay, ni maoni yangu lakini.
 
Mwachieni tukutane kitaa akiwa sio DC atajua kuwa haajui mamaeeee
🤣🤣 Sasa mkuu utamfanya nini unadhani mbona yule Makondakta wa daladala anadunda mtaani wakati alipigwaga ban hadi na Pompoe?
 
Kama mama alikuwa ana mpango wa kukutana na wapinzani itakuwa ngumu Sana Kwa kauli ya Jana aliyoitoa mbowe!!!
Kwa kifupi mbowe amekosea Sana kupiga mikwala ya kishamba ya kudai katiba mpya Kwa kuingia barabaran.... kipindi cha mwendazake mbowe alitulia Tu
Huu ni uongo mkubwa umeandika. Sijasikiliza hotuba ya mbowe hivo siwezi kusema chochote, lakini kuhusu hoja yako kwamba Mbowe alikuwa ametulia wakati wa JPM huu uongo nenda ukawadanganye vijiwe vya kahawa.
Nikukumbushe tu, Mbowe alimkosoa sana JPM kuhushu jinsi ya kushughulikia Covid na pia alililia sana Democrasia na uhuru wa mahakama.
 
Ndio ni haki yao kuongea hivyo.
Kumbuka hizi kauli zao zimesababishwa na kauli alizoongea Rais Juzi kuhusiana na Katiba mpya na shughuli za Siasa.

Kumbuka hawa Chadema ni waathirika wa utawala wa Magufuli. Na kauli za Rais bado zinaendeleza maumivu yao badala ya faraja kwao, Ndio maana unawaona wamepaniki na kuongea hivyo.

Kule Bungeni 99% ni CCM watupu hivyo hiki ni kipindi kizuri sana kwa wabunge wa CCM kupitisha katiba kule Bungeni, maana wapo wenyewe tupu.
Kwahiyo wakisha mpa vitisho rais vya kumnyoa ndio ataogopa kisha atawapa katiba mpya?
 
Ni suala la muda tu na kujipa subira kidogo tutajionea kwa macho yetu Mungu akitupa uzima.

Jana tulishuhudia mh. Mbowe akitamka kauli tata zenye vitisho na amri dhidi ya Rais wa nchi.

Swali jiulize kama Rais wa nchi anatamkiwa maneno kama yale hadharani je vipi kuhusu mkuu wa wilaya tena pale nyumbani kwake Hai hali ilikuwaje kwake?

Matusi mangapi aliyoyaoga Sabaya ikiwa tu Rais wa nchi haheshimiwi hata kidogo?

Ukiangalia kauli za Mdude CHADEMA eti alimnyoa mwendazake na sasa atamnyoa mama akileta jeuri hapo utajiuliza alimyoaje mwendazake na huyu mama nae atanyolewa vipi?

Yeye ndio alimtoa madarakani kwa kumnyoa hadi kufa sivyo?

Ni kipi hasa mama anachotakiwa kumtii mdude/mnyoaji kwa heshima zote ili asinyolewe?

Ni wazi kuongoza watu wa namna hii inahitaji kiwango cha juu sana chauvumilivu.
Ukiunganisha matukioa ya kesi ya Sabaya.
Kuachiwa Mdude.
Kutumbua baadhi ya watumishi wa enzi za JPM.
Kufutwa kwa kesi ya Mbowe na wenzake utagundua kuwa ulikiwa mkakati maalumu wa mama kutaka kuwaridhisha wapinzani kwa kuwapa matumaini ya utawala mpya lakini kwa hiki wanachokifanya kwasasa hata ile kafara ya Sabaya iliyotaka kutolewa Kama sadaka ya kuwatuliza muda si mwingi itaghairishwa.
Kesi ya huyu mtu imekaa kisiasa sana na nguvu kuwa sana inatumika dhidi yake kutoka fulani wenye hasira na visasi vikubws ndani ya mioyo yao kuliko uhalisia wa aliyo yatenda.

Nadhani sasa mama Kesha wajua vizuri watu aliotaka kuwafurahisha ni watu wa namna gani.

Tujiandae Sabaya kuwa huru hivi karibuni kafara yake imekataliwa.
Ndugu usitishwe na hivi vitisho..sisi huku uswahilini huwa tunamisemo yetu..DEBE TUPU HALIACHI KUTIKA.. Pia husema...KELELE ZA MLANGO HAZIMKOSESHI USINGIZI MWENYE NYUMBA.....Kwani uliona au kusikia wapi ..KELELE ZA CHURA ZINAMZUIA NG'OMBE KUNYWA MAJI? Relax!
 
Ni suala la muda tu na kujipa subira kidogo tutajionea kwa macho yetu Mungu akitupa uzima.

Jana tulishuhudia mh. Mbowe akitamka kauli tata zenye vitisho na amri dhidi ya Rais wa nchi.

Swali jiulize kama Rais wa nchi anatamkiwa maneno kama yale hadharani je vipi kuhusu mkuu wa wilaya tena pale nyumbani kwake Hai hali ilikuwaje kwake?

Matusi mangapi aliyoyaoga Sabaya ikiwa tu Rais wa nchi haheshimiwi hata kidogo?

Ukiangalia kauli za Mdude CHADEMA eti alimnyoa mwendazake na sasa atamnyoa mama akileta jeuri hapo utajiuliza alimyoaje mwendazake na huyu mama nae atanyolewa vipi?

Yeye ndio alimtoa madarakani kwa kumnyoa hadi kufa sivyo?

Ni kipi hasa mama anachotakiwa kumtii mdude/mnyoaji kwa heshima zote ili asinyolewe?

Ni wazi kuongoza watu wa namna hii inahitaji kiwango cha juu sana chauvumilivu.
Ukiunganisha matukioa ya kesi ya Sabaya.
Kuachiwa Mdude.
Kutumbua baadhi ya watumishi wa enzi za JPM.
Kufutwa kwa kesi ya Mbowe na wenzake utagundua kuwa ulikiwa mkakati maalumu wa mama kutaka kuwaridhisha wapinzani kwa kuwapa matumaini ya utawala mpya lakini kwa hiki wanachokifanya kwasasa hata ile kafara ya Sabaya iliyotaka kutolewa Kama sadaka ya kuwatuliza muda si mwingi itaghairishwa.
Kesi ya huyu mtu imekaa kisiasa sana na nguvu kuwa sana inatumika dhidi yake kutoka fulani wenye hasira na visasi vikubws ndani ya mioyo yao kuliko uhalisia wa aliyo yatenda.

Nadhani sasa mama Kesha wajua vizuri watu aliotaka kuwafurahisha ni watu wa namna gani.

Tujiandae Sabaya kuwa huru hivi karibuni kafara yake imekataliwa.
Watu wa pwani wanasema UKICHEZA NA MBWA ATAKUFUATA HADI MSIKITINI mama anecheza nao acha wamfuate hadi msikitini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom