Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Nadhani mkuu wewe ndie ambaye hukunielewa tangu kwenye mada hapo juu na ndio mana nikarudia tena maelezo hayo.
Alafu pia ni ukweli usio pingika kuwa uungwaji mkono na kusifiwa alikosifiwa mama kulitokana na hisani hiyo hiyo unayo ikataa kwa kuzitumia mahakama kufuta kesi za wanasiasa ambazo iliaminika na watu kuwa zilibambikwa pamoja na nyingine nyingi ili kufurahisha makundi kadha wa kadhi, mfano kundi la dini e.g mashekhe wa uamsho, kwa wafanya biashara watu Kama kina Papaa Musofe wako huru, wanasiasa ndio kabisaa kina Mdude, Mbowe na wenzake hawa yote yamefanyika lengo moja tu kurudisha imani iliyo potea enzi za mtangulizi wake wakiamini hawajatendewa haki.
Na ndio mana nasema kwa mawazo yangu hata huyu Sabaya pia yupo ndani ya kimbunga hiki hiki cha kutafuta imani ila tu yeye amekuwa mbuzi wa kafara tena ukizingatia katokea pale pale sebuleni kwa Mbowe, huyu Sabaya ni adui wa pili wa Mbowe baada ya marehemu. Kwangu mimi binafsi kinacho mkuta huyu ni mbinu tu ya kutuliza hali ya hewa.
Ni kweli tunadai katiba lakini si kwa njia ya kumpa amri rais na vitisho vya kunyolewa kwa hapo hatuwezi kufika mkuu.
Na hata hizo hisani hatuta ziona tena badala yake itatumika dola Kama nyakati zilizopita tu na nasema hata huyu Sabaya atakuwa huru muda si mwingi.
Okay, ni maoni yangu lakini.
Kwa taarifa yako hata kama hao cdm wangelala chini rais apite juu ya migongo yao, bado huyo Sabaya angetoka tu. List ya waovu waliofaidika na uovu wa Magu ni pamoja na huyu mama. Hivyo hakuna namna mama angeweza kuchukua hatua za ukweli dhidi ya mtu muovu, wakati yeye binafsi ni mfaidika wa huo uovu huo aliofadika nao Sabaya. Kama alikuwa anacheza maigizo kutuonyesha kuwa anapambana na uovu, mshauri tu aache, bali tunawaka katiba mpya.Na kama atachukua hatua zozote kutokana na maneno ya Mdude, basi atakuwa ni rais mwenye uwezo duni kweli kweli.