Nyamizi
Platinum Member
- Feb 19, 2009
- 9,186
- 13,757
Naomba nikurudishe kwa comment yako ya mwanzo,tayari hata wewe ulishaegemea upande wa Ruto rudia tena kuisoma comment yako na uje uniambie kama kweli ulikuwa neutral.Hiyo comment peke yake inakuondoa katika mtu anaetaka kujifanya yupo neutral.Sasa wacha tuiachie Mahakama itoe uamuzi wake usio na mahaba ya kuegemea upande kama mimi na wewe ambao tayari tushaside na upande mmoja.Tatizo la sisi watanzania ni kuegemea upande fulani bila kujali hali halisi. Na mtu akisha-side na upande fulani, haambiwi, hasikii ila anabisha kila kitu. Nadhani umeelewa vibaya dhumuni la mchango wangu. Sikatazi Raila kwenda kutafuta haki yake ila nimetoa mawazo kulingana na ninavyodhani. Hata mimi ningependa sana atafute haki yake na akishinda uchaguzi urudiwe kwani ni kwangu ni kielelezo cha mageuzi. Ningependa sana apate reward baada ya kupigana kwa muda mrefu.