Kwa kifupi: Lissu alichofanya leo mahakamani

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
Tundu Lissu aliendelea na majumuisho yake ya mwisho katika kesi yake ya uhaini, akijikita zaidi kwenye hoja kuu mbili:

1. Hoja ya publication: Alipinga madai kwamba yeye ndiye aliyechapisha video ya mkutano wa CHADEMA kwenye Jambo TV. Alirejea ushahidi wa PW1, PW2, PW3, PW16 na hasa PW17, akisema ushahidi unaonyesha kuwa wafanyakazi wa Jambo TV ndio waliorekodi na kurusha video hiyo.

2. Kama Serikali ilitishwa: Alisema upande wa mashtaka haukuleta ushahidi kuthibitisha kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilitishwa na maneno yaliyotajwa kwenye mashtaka. Alisema watu mbalimbali aliokuwa ameomba waitwe kutoa ushahidi kuhusu hilo hawakufika Mahakamani.

Lissu akahitimisha hoja hiyo kwa kusema:

“Jibu la swali la saba can only be NEGATIVE — Serikali haikutishwa.”

Baada ya hapo aliomba mapumziko ya saa 1½, akieleza kuwa amekuwa akikesha usiku akiandaa kazi hiyo na anahitaji kupumzisha mwili.

Majaji wakaamua kusitisha kwa siku ya leo Mpaka Jumatatu saa 3:00 asubuhi.

Soma zaidi Kinachojiri Mahakamani leo Septemba 25, 2026, kesi ya Uhaini Tundu Lissu vs Jamhuri
 
mpe pole sana aise,
maana kazi hizi za kujitakia na kuzifanya kibinafsi bana, saa zingine zinakua ngumu mno aise na zinaweza kukupelekea kua mwehu kabisa.

namsalimia sana homeboy 🐒
 
bado washtaka hawajafanya hitimisho na tarehe ya hukumu, hapo ndipo itaisha.
Rostaz Aziz aliwahi kusema "mtu mwenye akili timamu hawezi kuwekeza mtaji wake mkubwa kwenye nchi ambayo mahakama pamoja majaji na mahakimu wanapokea simu za maelekezo" baada ya hapo wenye mamlaka wakaanza kusema kuwa ameidhalilisha mahakama
 
Back
Top Bottom