Kwa Kiingereza hiki kwenye barua ya ufafanuzi kukamatwa kina Dkt. Slaa heri tuendelee na Kiswahili, ni aibu ya mwaka

Kwa Kiingereza hiki kwenye barua ya ufafanuzi kukamatwa kina Dkt. Slaa heri tuendelee na Kiswahili, ni aibu ya mwaka

Hili ni bango la wizara kwa lugha ile............tuanzie hapo mleta mada, onyesha utata wa kisarufi, kimuundo na kimantiki.


The United Republic of Tanzania​

Ministry of Information, Communication and Information Technology​

Swali lako limekaa vizuri ,

Usahihi ni huu:
1692352108063.png

Maelezo:
-
kifungu cha maneno, "The United Republic of Tanzania Ministry of Information, Communication and Information Technology", hakiko sawa. Kina makosa ya kisarufi na kimuundo. Makosa hayo ni:
  • Kurudia neno “Information” katika jina la Wizara. Hii inasababisha utata wa kimuundo kwa sababu haijulikani kama ni Wizara ya Habari na Mawasiliano au Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
  • Kutumia herufi kubwa katika maneno yote ya jina la Wizara. Hii inakiuka kanuni za uandishi wa Kiswahili ambazo zinataka herufi kubwa kutumika tu mwanzoni mwa sentensi au katika majina maalum ya watu, mahali, n.k.
  • Kutotumia alama za uakifishaji kama vile mstari mrefu (-) au koma (,) kuonyesha mgawanyo wa maneno katika jina la Wizara. Hii inasababisha ugumu wa kusoma na kuelewa jina la Wizara.
Kifungu cha maneno hicho kingeandikwa vizuri zaidi kama ifuatavyo:
"The United Republic of Tanzania
Ministry of Information, Communication, and Technology"
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia
 
Nyumbu na haters bwana wakikosa hoja huku wakiwa na wingi wa utoto kichwani huwa wanachekesha sana!!! Kumbe hawa ndo maana wanazidiwa na Diamond aisee!

Haya, hebu kila nyumbu na hater abadilishe comment yake kwenda kikngereza tuone ni kwa umbali gani mwenzetu umepiga hatua! Tadadhali postini tena comments zenu kwa kiingereza........tunasubiri🙏🙏🙏
Nyumbu ni wewe mwenyewe. Ukijiona nyumbu usifikiri wote ni Kama wewe.
 
Hapo tayari CHADEMA imepata agenda wakati CCM iko bize kutetea jimbo Mbarali kwenye uchaguzi mdogo. Upinzani ukiwa unayumbishwa na mambo madogo wataendelea kuilaumu CCM
Lini CHADEMA imejadili hiyo barua?. Nyie endeleeni na uchaguzi mbarali maana hamna jipya, mmekaa kinafiki.
 
Kiingereza siyo lugha yetu, kwahiyo mi sioni ajabu...Si Kila jambo la kukomalia. Hata hao wazungu wenyewe viingereza vyao vina shombo kama sisi kama siyo lugha Yao ya asili
Ungemshauri atumie kiswahili, kuliko kujivua nguo hadharani.
 
Binafsi sehemu pekee nilizoona zina makosa ni mbili tu ambapo ya kwanza ni 'TANZANIAN GOVERNMENT RESPONSE' ilitakiwa kuwa 'TANZANIAN GOVERNMENT'S RESPONSE' na sehemu nyingine ni neno government na president yameandikwa kwa kuanza na herufi kubwa yakiwa katikati ya sentence.

Kwa ufahamu wangu, kwingine kote sijaona kosa. Sasa kama niko sahihi, basi wewe mtoa mada pamoja na 90% ya walio'reply hamjui kitu chochote kuhusu lugha iliyotumika (ni weupe kichwani).
Wewe ndio mweupe kuliko huyo kilaza Nape.
 
Mwl Nyerere pamoja na kusaidia kudai uhuru ila hakuwa muelewa wa diplomasia ya uchumi, in fact alikuwa mtupu kabisa. Mifano mingi sana juu ya udhaifu wa Mwl. Mfano mmojawapo kulikuwa na haja gani ya kuondokana na mfumo wa Elimu ya Muingereza??? Je kulikuwa na haja gani ya kuondokana na mfumo wa uendeshaji wa uchumi wa muingereza??? Ukitaka kujua Mwl alikuwa hajui diplomasia ya uchumi mcheki Madiba a.k.a Mzee Mandela. Yeye alipo pata uhuru alisema kabisa hawa Makaburu pamoja na ubaya wao il Elimu na Uchumi aliwaachia na yeye akaamua tu kitu kimoja uhuru wa kujitawala ambao mpaka leo bado ni kituko. Rais Dkt Samia ni Professor wa diplomasia ya uchumi na Elimu (ingawa elimu uharibifu wake alioufanya Mwl Nyerere ni mkubwa na repair yake it will take years kuponya). Kwenye uchumi sasa tunaona Rais Dkt Samia anavyotupambania kuhakikisha tunakuwa kama au zaidi ya Dubai. Ni muhimu tumuunge mkono rais wetu Dkt Samia.
Tatizo mnalinganisha miaka ya 1961 na mwaka 2023. Unadhani mazingira ya Mwalimu yalikuwa sawa na ya Samiah?. Tuache ujuaji kwenye mambo tusiyoyajua.
 
Kwani huyo alie andika Huwa hawazipitii kuhakikia [emoji706][emoji706][emoji706][emoji706]Shida sana hii kama hiyo paragraph umeizungushia ...

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Hapo wanamuandikia beberu??
Naona aamemtukana na Magufuli sijui amewakosea nini????
Ok msalimieni Beberu sipati picha anavyosoma kwa kucheka
 
Nape hawezi kuandika kiingereza kibovu, kwanza kasoma India na Uk kwenye vyuo vikuu vya maana kama oxford na university of London. Kwa hiyo hiyo barua ni feki
Sawa mh tumekusikia
 
Kiswahili wanachokimudu wanakibeza, Kingereza wasicho kimudu wanakitukuza,matokeo yake Kingereza kinawabeza wao
 
Kama waziri hajui jina la wizara anayoisimamia, je, anatosha?
 
Mimi nadhani tujadili zaidi kukamatwa kwake ni halali? Yamkini wanatuchanganya tusiwe na muda wa kujadili suala hilo
 
Kwa akili yako timamu unafikiria kiswahili kinaweza kutumika ku address issue serious nje ya Tanzania?? Putin anafahamu Kiingereza na Kijerumani ila hata sikumoja hawezi kwenda kutoa hotuba kwa lugha hizo kwa sababu anauhakika ni lazima wafanya maamuzi wamsikilize katika lugha yake ya Kirusi na watafsiri kwa lugha watakazoelewa kwa maana anayoongea yana TIJA. Sasa unategemea Hotuba yenye TIJA kutoka kwa mtu ambaye bado nchi yake inakopa pesa ijenge vyoo vya shule? ni dhahiri changamoto zake bado ni za zama za mawe hana mchango wa maana kwenye ulimwengu wenye changamoto za dunia ya kwanza?? Tuwe serious
Sasa Nape akiongea Kuswahili hituba yake itakosa tija kwasababu ya kuongea Kiswahili? Jaribu kuendana na hadhi ya JF٬ the home of great thinkers.

Sasa nchi kuwa na changamoto za kizamani zinazuia nchi hiyo kuongea Kiswahili na kusikilizwa? Hivi hao waliompa ruhusa ya kuongea Kiswahili hawalijui hilo ila wewe ndo unalijua? Hivi kweli wewe unajua unachozungumza?

Nakushauri: Sio kila mtu anaweza kuzungumza au kuandika. Ukiona mada imekuzidi bora ukae kimya; jizuie.
 
Sasa Nape akiongea Kuswahili hituba yake itakosa tija kwasababu ya kuongea Kiswahili? Jaribu kuendana na hadhi ya JF٬ the home of great thinkers.

Sasa nchi kuwa na changamoto za kizamani zinazuia nchi hiyo kuongea Kiswahili na kusikilizwa? Hivi hao waliompa ruhusa ya kuongea Kiswahili hawalijui hilo ila wewe ndo unalijua? Hivi kweli wewe unajua unachozungumza?

Nakushauri: Sio kila mtu anaweza kuzungumza au kuandika. Ukiona mada imekuzidi bora ukae kimya; jizuie.
Unafahamu ulichouliza, mimi sifahamu hata ninachoongea mkuu, nasubiri jua lizame nikapate mbege mkuu BTW Karibu
 
Back
Top Bottom