Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Kwa yanayoendelea mataifa ya kiarabu na sasa habari inayovuma ni Uvamizi wa kijeshi wa taifa la Urusi Kwa Taifa la Ukraine ni dhahiri kuwa Waafrika hawana namna ya kufanya zaidi ya kuwa Vibaraka.
Sisi ambao hatujawahi kushika nafasi za juu katika nchi tunaweza kuwalaumu hawa ndugu zetu lakini nimrjaribu kufikiria Kwa upande wa pili nimegundua kuwa ndugu zetu hawana jinsi, hawana chaguo zaidi ya aidha kukubali kuwa kibaraka au kupokea vipigo ambavyo huwa vya Aina Aina.
Viongozi wote niliokuwa nawashambulia Kwa kweli mnisamehe tuu.
Nilifikiri kibinafsi bila kuvaa viatu vyenu. Sasa nimetambua jinsi msivyokuwa na chaguo zaidi ya kuwalamba Wababe wa Dunia viatu.
Ukweli ni kuwa usipomlamba viatu Mchina, basi utawalamba nchi za Magharibi na Marekani au Kanada.
Ubabe wa Dunia upo na utaendelea kuwepo,
Hakuna cha mzalendo wala ndugu yake uzalendo,
Tupo katika nyakati za kutawaliwa, inabidi tuwe wapole huku tukiwekeza kwenye elimu Kwa watoto wetu, hasa elimu ya kujitambua na elimu ya Mazingira.
Hii elimu ya kujifanya mzalendo ukiwa hauna Cheo ni uongo mtupu, wengi wakipewa uongozi hukuta kinyume na Yale waliyoyadhania.
Kwa mfano;
Tutafute mtu yeyote anayejiona mzalendo, alafu apewe nchi, utashangaa ndani ya miaka miwili mitatu ananyosha mikono na kujiunga katika kundi la Vibaraka.
Nini KIFANYIKE;
1. Elimu ya utambuzi na mazingira itolewe
2. Dini zote za kuja zifutwe na kama Hilo litakuwa gumu kutokana na kuwa Vibaraka bado ni wengi katika Dini hizo, basi elimu itolewe kuwa Dini ni elimu tuu ya maadili ya kumfanya mtu awe mwema ndani ya jamii.
Lakini hazina uhusiano wowote na MUNGU.
3. Neno Demokrasia lipatiwe maana nyingine kulingana na Mila na desturi ya taifa na jamii zetu.
4. Serikali iratibu mzunguko wa uzalishaji, na kuandaa matajiri wenye asili ya Tanzania ambao kwenye top 50 wawe zaidi ya Asilimia 80.
5. Serikali ianzishe Karakana kubwa kila kanda za kuzalisha Vijana wenye ubunifu na Teknolojia.
6. Serikali isiogope kuwa na Sera za Uvamizi na kutanua mipaka ya Nchi Kwa kuangalia maslahi ya watu wake. Hili kila siku nalisema.
Acha nipumzike kwanza