Kwa kujaribu kuitingisha misingi ya demokrasia nchini Marekani iliyodumu kwa miaka zaidi ya 300, Trump aliamsha dude!

Mag3

Platinum Member
Joined
May 31, 2008
Posts
13,413
Reaction score
23,592
Rais Donald Trump wa Marekani amenajisi misingi imara ya demokrasia nchini humu kwa dhana potofu kwamba labda yuko juu ya sheria. Kwa kitendo cha wafuasi wake kuvamia bunge la nchi hiyo kwa nia ya kusimamisha shughuli halali za bunge hilo kama alivyowaamuru, amevuka mstari usiovukwa. Dunia ina mengi ya kujifunza kuhusu taifa hilo na hatua ambazo sasa lazima zichukuliwe kwa wahusika wote bila kujali vyeo wala nafasi zao katika jamii.

Marekanai, taifa la watu huru, taifa la watu waliomwaga damu kudai uhuru, taifa la watu waliozikimbia nchi zao za asili kuepukana na tawala za kiimla, lazima liwashughulikie watu kama Rais Trump ili kuwa mfano kwa watu wake na dunia kwa jumla. Kaeni mfuatilie na kushuhudia jinsi taifa hilo litakavyoonesha kwa nini taifa hilo tofauti na mataifa mengine kama Urusi, China, Korea Kaskazini na hata Tanzania, madaraka yako kwa wananchi na si viongozi.

Hapa chini anaonekana Trump na baadhi ya wasaidizi wake wakiwashawishi wafuasi wao kuvamia Capitol Hill...

 
Mimi sina maneno mengi! Naomba ninukuu maneno ya mwana Congress Karen Bass:

Every single person that broke into the Capitol should be arrested.

Every single person that scaled the Capitol with rope should be arrested.

Every single person that broke into Speaker Pelosi’s office should be arrested.

Every single person that broke into the Senate Chamber should be arrested.

When this is all over, we will respond and our response will be forceful.

This is the United States of America and this will not stand.

(Mwisho wa kunukuu!)
 
Subiri waje wayahudi weusi akina zedudu humu tusikilize maoni yao
 
Mimi sina maneno mengi! Naomba ninukuu maneno ya mwana Congress Karen Bass:

Every single person that broke into the Capitol should be arrested....
House members na Senators baada ya kuona kilichokuwa kinatendeka huko nje (kumbuka wakati wa uvamizi walikuwa wamejifungia hawajui kinachoendelea huko nje) wamepigwa butwaa! Wanajiuliza kama kweli hali kama hii inaweza kutendeka ndani ya taifa lao. La kwanza walilofanya wote kwa pamoja ni kumpitisha Joe Biden kama mshindi wa Urais kwa kupokea na kuhesabu kura za electors: 306-232

Dunia itapata nafasi ya kushuhudia uzuri wa kuwa na taasisi imara katika utawala wa demokrasia unaofuata sheria. Marekani haina utani linapokuja swala la sheria, kanuni na taratibu.
 
#BREAKING: Facebook & Instagram are blocking President Trump from using their services indefinitely and for at least the next two weeks until the peaceful transition of power is complete, CEO Zuckerberg says. https://t.co/L3Xxiw9zlg
 
Hii issue ya Capitol imemu-isolate sana Donald Trump. Mpaka sasa maafisa na washauri wake kadhaa wamejiuzulu nyadhifa zao na wengine pia wanafikiria kufanya hivyo hivi karibuni.
 
Russian and china are laughing aside let it broke into pieces
Ngoja wacheke lakini wao hawana cha kujivunia kwani ni wao Trump anajaribu kuwaiga naye awe kama wao, above the law. Hali kama hii ingetokea Russia au China idadi ya watu ambao wangeuawa si haba. Kwa miaka minne Trump amekuwa na free ride hadi kuitumbukiza Marekani katika hali tunayoishuhudia akizijaribu taasisi zake kama ni imara!

Yesterday's events were an unprecedented attack on the very core of American democracy - incited by a sitting president. The president has long disregarded and diminished the rule of law and the constitution. Yesterday, that culminated in violent sedition against the US Congress for the purposes of overturning a legally recognized and valid election.

Matokeo ya huu uasi ukiongozwa na Rais Trump hayatakuwa mazuri kwake na kama nilivyosema hapo juu ameliamsha dude na sasa baada ya kulikoroga awe tayari kulinywa pamoja na machungu yake. Kama alivyowahi kuonya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere; mtoto akililia moto mpe umchome pale pale na Trump kweli kalilia moto...
 
Hii dili nahisi Mrusi alikuwa na nia ya kulipiza kisasi yale ya Gorbachev nao wakamweka trump
Kilicho wasaidia US ni mifumo yao ya Kiutawala ipo Imara
 
Wahenga walinena: Mzaha mzaha!.........

..........Mbuzi kampanda mama yake.

Trump anawapa uhalali madikteta wa kiafrika, anawapa waminya demokrasia cha kujitetea. Katika yote aliyofanya hili litatuathiri sana waafrika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…