Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Rais Donald Trump wa Marekani amenajisi misingi imara ya demokrasia nchini humu kwa dhana potofu kwamba labda yuko juu ya sheria. Kwa kitendo cha wafuasi wake kuvamia bunge la nchi hiyo kwa nia ya kusimamisha shughuli halali za bunge hilo kama alivyowaamuru, amevuka mstari usiovukwa. Dunia ina mengi ya kujifunza kuhusu taifa hilo na hatua ambazo sasa lazima zichukuliwe kwa wahusika wote bila kujali vyeo wala nafasi zao katika jamii.
Marekanai, taifa la watu huru, taifa la watu waliomwaga damu kudai uhuru, taifa la watu waliozikimbia nchi zao za asili kuepukana na tawala za kiimla, lazima liwashughulikie watu kama Rais Trump ili kuwa mfano kwa watu wake na dunia kwa jumla. Kaeni mfuatilie na kushuhudia jinsi taifa hilo litakavyoonesha kwa nini taifa hilo tofauti na mataifa mengine kama Urusi, China, Korea Kaskazini na hata Tanzania, madaraka yako kwa wananchi na si viongozi.
Hapa chini anaonekana Trump na baadhi ya wasaidizi wake wakiwashawishi wafuasi wao kuvamia Capitol Hill...