Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Huduma ya afya ni haki ya msingi kwa kila mtanzania. Ni wajibu wa serikali kuweka utaratibu wa kuwezesha kila mtanzania anapata haki hii ya msingi. The Healthcare must be easily accessible and affordable to every tanzanian.
Huko nyuma hadi mwaka 1998 huduma hii ilikuwa inatolewa bure na serikali kupitia bajeti ya serikali. Mwaka 1999 serikali iliweka utaratibu wa wagonjwa kuchangia kiasi kidogo cha gharama ya matibabu yao ie cost sharing. Kiasi hicho cha mgonjwa kuchangia kikawa kinaongezwa kila mwaka hadi kuwa kikubwa sana. Ikawa tena siyo cost sharing but full cost. Sana sana mchango wa serikali ukabaki ni kulipa tu mishahara ya watoa huduma. Hadi sasa watanzania walio wengi (takribani robo tatu au zaidi) hawana uwezo wa kupata huduma hii. Our health care is no longer affordable to the majority of our people. Leo hii watu wengi matumbo yao yakijifunga (bowel obstruction) wanakufa kwani gharama ya kuyafungua kwa operesheni ni malaki kama siyo mamillioni ya pesa. Leo hii matibabu ni kwa wale pesa, wale wengine wamebaki wakihangaika kwa miti shamba na tiba mbadala. They have been denied access to our health care.
Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) ulianzishwa kwa ajili ya watumishi wa serikali ili kutatua tatizo hili. Baadaye serikali iliruhusu mtu ye yote kujiunga na mfuko huo. Lakini gharama za kujiunga na mfuko huo imekuwa kubwa sana hususana full bundle ni TSh 1.5 milioni kila mwaka, kitu ambacho watanzania wengi hawawezi. Matumaini yao yalikuwa kwenye uanzishwaji wa mfuko wa Bima ya Afya kwa Wote. Walitegemea utakuwa kweli kwa wote lakini gharama ya kujiunga na mfuko huo ilipopendekezwa na serikali kuwa Tsh 350,000 kwa mwaka, matumaini yao yaliyeyuka.
Serikali inabidi ikubali kwamba watanzania wengi (over 70%) ni wanyonge ambao kipato chao kwa siku hakizidi dollar moja ya kimerikani. Na kwamba mfuko huu wa Bima ya Afya kwa Wote ni kwa ajili ya hawa wanyonge. Tungeweza kuuita Mfuko wa ya Afya kwa Wanyonge.
Mapendekezo.
1. NHIF: iendelee kwa wale wenye ukwasi wanaohitaji fast track service au private service au VIP service. Mchango wake ubaki huo wa TSh 1.5 millioni kwa mwaka. Watumishi wa umma waendelee na mfuko huu kwa kukatwa mishahara yao na kiasi kinachobaki kwenye hiyo 1.5 milioni kulipwa na serikali kwenye mfuko huo. Kwa wale VIP iwe TSh 3.0 milioni kwa mwaka. Makampuni binafsi na watu binafsi wenye uwezo washawishiwe kujiunga na mfuko huu. Wenye bima hii wataweza kutibiwa hata kwenye private hospitals. Hizo bando ndogo ndogo kwenye mfuko huu ziondewe, ibaki full package na vip.
2. Bima ya Afya kwa Wote.
Baada ya zoezi la kisasa la sensa kukamilika, sasa tuna takwimu zote zinazohitajika kukokotoa kiasi cha kila familia au kaya tunachotaka wachangie kujiunga na mfuko huu. Tatizo hadi sasa National Beural of Statistics hawajaweka wazi mchakato mzima wa matokeo ya sensa. Hivyo nilizotumia hapa ni maoteo.
- Kwa mjibu wa sera yetu, wazee wa umri wa miaka zaidi ya 60, watoto chini ya miaka 5 na akina mama wenye mimba matibabu yao ni bure.
Serikali iwalipie Sh 30,000 kwa kila mzee, mtoto na mjamzito kwa mwaka kwenye mfuko huu wa bima kwa wote. Hivyo hivyo kwa kila kaya za TASAF. Nimeotea kundi hili litakuwa na watu au kaya million 5. Hivyo kwa mwaka serikali italipa kwenye mfuko huu Sh 30,000 × 5,000,000 = Sh 150 billion.
Hili ni jukumu ambalo serikali lisilikwepe.
- Kaya za wanyonge nimeotea kuwa ziko 15 millioni. Nimegawa hiyo population ya 61 million kwa 4. Hawa nao walipe Shs 30,000 kwa kila kaya kwa mwaka. Hivyo watalipa kwenye mfuko huu
Sh 30,000 × 15,000,000 = Sh 450 billion.
- Hivyo jumla ya Sh 600 billion kwa mwaka zitalipwa kwenye mfuko huu kwa ajili ya matibabu ya magonjwa yo yote watakayopata wanyonge hawa katika hospitali na vituo vyote vya serikali. Bima hii si kwa kutibiwa kwenye vituo vya binafsi. Kwa kiasi hiki cha sh 30,000 kwa mwaka, kuna uhakika wa karibu kaya zote kuweza kulipa bima hiyo kwa hiari bila shinikizo wala tozo. Sh 600 bilioni zitaweza sana kugharimia au kuchangia gharama za dawa, vifaa tiba, vipimo na operesheni zo zote watakazopatiwa.
Tusisahau kuwa population kubwa ya Tanzania (90%) ni la vijana na hivyo ni wachache sana (<10%) watakaougua na kuhitaji matibabu. Ndiyo maana hata mlipuko wa ugonjwa wa corona haukutusumbua maana sisi ni young population. Tuking'ang'ania kuwachangisha malaki hawa wanyonge nina uhakika hatutaweza kukusanya zaidi ya sh 10 billion na tatizo la ku deny access to health care to our people litaendelea. Mfuko huu lazima uwe full package na kusiwe na ubaguzi au unyanyasaji wo wote kwa wale wenye kadi ya mfuko huo kimatibabu.