Kuna kitu kimoja ambacho ninakuunga mkono kwa asilimia zote katika bandiko lako hili ni ushauri wako ulioutoa kwa watu wa Geita kuwa wasimpe kura hata moja Lissu,kwa kuwa anapinga uwanja wa ndege kujengwa nyumbani kwake Chato na kuhamishia mbuga ya wanyama kijijini kwake Chato.
Bonge la ushauri wako huu uwafikie pia wananchi wa mikoa mingine ambao Magufuli hajawafanyia kitu chochote nyumbani kwao wahakikishe hawampi Magufuli hata kura moja.
Nafikiri watu wengi hawajamuelewa mheshimiwa Lissu
Hata siku moja hajawahi kupinga maendeleo ya geita wala chato
Ila anahoji kulikoni pajengwe uwanja wa kimataifa kijijini ambako hakuna ndege inaenda isipokua ndege moja tu?
Pia kulikoni mkandarasi awe mume mwenza wa pombe??
Pia kulikoni mabilioni hayo ya pesa yaidhinishwe na mtoto wa dadake pombe bila hata kuhusisha yeyote serikalini?
Kama pangejengwa chuo kikuu au hospitali ya rufaa hata sisi tunaokaa geita ingetunufaisha
ufisadi wakati mwingine mafisadi wanatafsiri ni maendeleo