Kwa kutokuwepo Ujasiri wa Kujiuzulu, Uongozi ni Fursa

Kwa kutokuwepo Ujasiri wa Kujiuzulu, Uongozi ni Fursa

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Tuna nchi ambayo viongozi hawawajibiki kwa wananchi wala hata kwa kauli zao.

Tafsiri halisi ya kuwa uongozi kwao ni fursa wala si dhamana.

Kama fursa viongozi hawa wamejihakikishia marupurupu ya kufa mtu wawapo ofisini na hata wasipokuwapo:

IMG_20220107_150403_525.jpg

Yapo mengi ya kujiuliza. Mfano:

Kwanini waziri Mkuu hakujiuzulu kumpisha mama Samia kuunda serikali upya kwa uhuru baada ya Magufuli mwaka jana?

2. Kwanini waziri Mkuu anasubiri ikibidi afurushwe hata baada ya Mama Samia kuonyesha kukereka mno na uwepo wa vita vya chini kwa chini ndani ya serikali?

Au ni yale yale ya kutaka kutuaminisha wao na marupurupu yao mpaji ni Mungu?

Katiba mpya yenye kuweka tafsiri zote za msingi upya ndizo zenye kuweza kuliokoa taifa hili.

Marupurupu na ukomo katika ajira au baada yasiachwe mikononi mwa wanufaika kujipangia.
 
Wanajua wameshajitengenezea himaya yao hata wakitikiswa mambo yao yatabaki mazuri tu, and on top of that bado kuna kinga ya kushtakiwa kisheria, hawa sio wenzetu.
 
Wanajua wameshajitengenezea himaya yao hata wakitikiswa mambo yao yatabaki mazuri tu, and on top of that bado kuna kinga ya kushtakiwa kisheria, hawa sio wenzetu.

Hili la vyama vya siasa kupoa na kujivua uanaharakati, litatugharimu kwa muda mrefu sana.

Kwanini CCM wanatuita SACCOS?

DP ya Mtikila kwenye zama zake isingekaa kimya. Nini kimebadilika DP si ingalipo?

Pumzika kwa amani Mchungaji Mtikila.
 
Wanajua wameshajitengenezea himaya yao hata wakitikiswa mambo yao yatabaki mazuri tu, and on top of that bado kuna kinga ya kushtakiwa kisheria, hawa sio wenzetu.

Hivi lets say kiongozi akifariki marupu rupu yanaendelea?
 
Back
Top Bottom