Kwa kweli Kiswahili ni kigumu

Kwa kweli Kiswahili ni kigumu

deonova

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2013
Posts
742
Reaction score
419
Bado unasema Kiswahili ni lugha nyepesi eti kwa kuwa tunaelewana tu!!!?Tazama.......
KIINGEREZA------KISWAHILI
Device-------------Kitumi
Photocopier------Kinukuzi...
Duplicating Machine --Kirudufu
Resistor-----------kikinzani
Power Saw-------Msumeno oto
Sensor-----------Kisimbuzi
Lap Top---------Kipakatalishi
ICU--------------Kisadaruki
Microwave-----Tanuri ya miyale
Memory Card-----------Kadi sakima
SIM card----------Kadiwia/mkamimo
Scratch card------------Kadi hela
Business card-----Kadikazi
Identity card----Kitambulisho
ATM---------- -Kiotomotela
Nutrients ----- -Virutubisho
Starch---------- ---------Nisha
Stigma--------- ----------Ntwe
Nectar---------------Mbochi
Humus---------------Mboji
Germ cell----------Celizazi
Femur---------------Fupaja
Green house-------Kivungulio
Esophagus--------------Umio
Sunflower---------------Alizeti
Weevil-------------Fukusi/dumuzi
Distillation--------Ukenekaji
Evaporation-------Mvukizo
Dissolve ----------Uyeyushaji
Stagnant----------------Tuame
Synthesis---------Uoanishaji
Monitor-----------Muwazi
Processor---------Kichakato
Computer Virus-----Mtaliga
Floppy Disk-------------Diski tepetevu
Mouse-----------Kipanya/kisakura
Slot----------------Upenyu
Flash Disk--------------Diski mweko
Scanner-----------------Mdaki
Keyboard-------Kicharazio
Force of Gravity-------Kani ya mvutano
Certificate-----Astashahada
Diploma--------Stashahada
Degree------------Shahada
Masters----------------Uzamili
Phd----------------Uzamivu
Sausage---------------Soseji
Kebab-------------Mshakiki
Crisps--------------Kaukau
Chips-------------------Vibanzi
Juice---------------Sharubati
Password--------------Nywila
Zebra Crossing-------Kivuko milia

Afadhali kuchanganya lugha kwa kweli, tukiongea Kiswahili bila kukopa maneno hatutaelewana kabisa.
 
Lakini inabidi tukitumie sasa vizuri, ili hivyo vitu visiwe vigeni kwetu. Ni kigumu kwa vile hatukitumii.Tujivunie lugha yetu jamani, tunaiua hivihivi.
 
Hicho kiswahili cha hayo maneno ni kigumu kwa mtu asiyeshughulika na fani ya hayo maneno mathalan mkata tikiti wa Ubungo Bus Terminal. Kwa mtu anayeshughulika na mambo ya kompyuta na mitandao kwa mfano, hasa waalimu na wanafunzi wao hayo maneno(istilahi)wanaitumia na kuyakumbuka vizuri.
 
Hapo kiswahili ni kigumu zaidi ya kiingereza, kiswahili kama vipi kiwe kwa wanaokitaka ndio wakisome
 
Ila hii ya nywila nimewahi kuiona kwenye simu yenye kiswahili....umekosea nywila yako
 
aliyetafsiri icho kiswahili ni wakenya au wale ndugu zetu wa pale udsm? kama wakenya basi icho sio kiswahili, ni kikenya.
 
Ila huku ni kama kulazimisha tu, kama kitu hakina neno moja kwanini tunalazimisha? Ata kiingereza au kiarabu baadhi ya vitu hawana neno moja ni lazima waunganishe, ukija kiswahili tunalazimisha tu ilimradi na sisi tuenalo, sasa KISADARUKI ndo neno gani?
 
Back
Top Bottom