Kwa leo acheni tu niwape heshima zao wanawake wote:

Kwa leo acheni tu niwape heshima zao wanawake wote:

AMINATA 9

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2011
Posts
2,120
Reaction score
642
ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza anakuelewa anakusamehe halafu anasahau na anaendelea kukupenda!!!
...
UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana. Anakuchukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni kuchukiwa atachukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!

UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI:Anakuwa na hofu kwa kuhofia usalama wako,Ukirudi anafurahi, Anakukaribisha vizuri, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.
...
UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi,supu n.k. (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!

CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hufanyi maandalizi yoyote unamuumiza.Ukishamaliza bila kujali kama mwenzako naye karidhika unageukia pembeni na kuanza kukoroma.
Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza tokea hii; hana kinyongo!

UNAJIANDAA KWENDA KIBARUANI: Unaamka,Unakuta tayari kakuandalia viwalo, suruwali imenyooshwa kama ya askari trafiki, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi!
Ulichomuudhi jana keshasahau na kukusamehe! anakutakia kazi njema kwa pendo!!!

UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!

Na mengine meeeeengi sana wanafanyiwa hawa watu lakini WANASAMEHE, WANAVUMILIA,WANAENDELEA KUWAPENDA!

Kwa leo acheni tu niwape
heshima zao wanawake wote:

LOVE WOMEN!

GOD BLESS WOMEN!!!!!!"
 
upendo wa mwanamke hauwezi kulinganishwa na upendo wa mwanamme katika mapenzi mana wanawake hua wanapenda sana kuliko wanaume katika mahusiano.....................just love ur woman plzzzzzzzzzzz kama hukufanya 2011 just try again 2012 mana hujachelewa bado kustart afresh
 
umesomeka, ila ngoja tusubirie upande wa pili wa shilingi
 
Kuna point hapo zingine zinaonyesha si kupenda bali ni ujinga walio nao....Haswa hio ya kumfumania mme wake, halafu bado anaendela kuishi na mme wake.

Any way nice thread.
 
mamie this z awesome, kaz ni kwao hope watalipata somo.
wanawake oyeeee.
 
I will always remember my beloved wife, I KNOW ONE DAY YOU WILL FORGIVE ME! I LOVE YOU
 
wako juu kama mawingu siku zote
ndo wanaofanya finishing ya kujaza dunia
unafikiri mchezo hapo!
 
upendo wa mwanamke hauwezi kulinganishwa na upendo wa mwanamme katika mapenzi mana wanawake hua wanapenda sana kuliko wanaume katika mahusiano.....................just love ur woman plzzzzzzzzzzz kama hukufanya 2011 just try again 2012 mana hujachelewa bado kustart afresh
unawezaje kugeralized and you have never been a man ?
 
Kuna point hapo zingine zinaonyesha si kupenda bali ni ujinga walio nao....Haswa hio ya kumfumania mme wake, halafu bado anaendela kuishi na mme wake.

Any way nice thread.

Sio wote wasameheo na kuendelea kuishi na waume zao baada ya kuwafumania ni kwa ajili ya ujinga......chunguza tu ndugu yangu!!!
 
Sio wote wasameheo na kuendelea kuishi na waume zao baada ya kuwafumania ni kwa ajili ya ujinga......chunguza tu ndugu yangu!!!
sio wote ila ktk 100% nakuambia 78% wanasanehe na kukaa na waume zao
 
unawezaje kugeralized and you have never been a man ?
m
mweh! kwani mpaka niwe man ndio naweza kujua kuhusu mwanaume ana filiaje ndani ya moyo wake ...............mbona ww mwanamme ila wajua sana kuhusu wanawake kwani ulishawai kuwa mwanamke??????????
 
Back
Top Bottom