Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
MZALENDO au NDUMILA KUWILI?
Tuwangalie kwa jicho angavu
Ni tatizo tusilolijua
Pande mbili za mheshimiwa na tusiyoyakumbuka
Wanajamvi tutakuwa na sehemu I-III kuhusiana na mwenyekiti wa bunge la katiba, tukimwangalia alipotoka alipo na aendako.
Kwa mwenendo wake wengi tunajiuliza kama keshakata tamaa na sasa anahitimisha safari yake ya kiasiasa
Sehemu ya I
Mwenyekiti wa bunge la katiba(BMLK) Mh Samwel Sitta ni mwanasiasa asiyeleweka kwa wengi. Amejaliwa kipaji cha kuongea,busara na kujenga imani kama mmoja wa Wazelondo wa nchi hii.
Historia yake ni ndefu katika umri wa miaka 71. Sitta ni msomi wa sheria akiwa mhitimu kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaa. Alianza masomo yake mwaka 1964 na kumaliza mwaka 1971.
Miaka 7 chuoni UDSM haikuwa rahisi, naye kama walivyo wanasiasa wengine aliwahi kufukuzwa chuo mwaka 1966 katika ule mgomo wa kujiunga na JKT.
Mgomo huo uliitingisha nchi lakini si mwalimu Nyerere. Wanafunzi wa chuo kikuu walimpa mwalimu ‘ultimatum' kuhusu madai yao. Hatimaye wakajikuta uso kwa uso na mwalimu na ndipo walipokabiliana na nguvu ya hoja na nguvu za dola.
Wengine waliokuwepo ni akina Warioba na viongozi wengine.
Samwel Sitta amelihudumia taifa katika ngazi ya serikali na chama akiwa waziri, katibu wa chama, mkurugurenzi mtendaji wa mashirika ya umma n.k.
Hiyo pengine ni pamoja na kuwa na diploma katika mambo ya utawala kulikompa nafasi zaidi
Kwa haraka haraka Sitta anaonekana kama miongoni mwa wanafunzi watiifu wa Nyerere. Hata hivyo muda umetueleza bila kificho akina nani walikuwa watiifu na wepi walikuwa na woga wakiwa wanafunzi wanafaniki.
Sitta ilichomoza akiwa miongoni mwa wapiga debe wakubwa wa EL katika chaguzi za mwanzo. Tunakumbuka jinsi Mwalimu alivyomuangalia EL kwa jicho la hofu na uhalifu.
Pamoja na hayo sitta alikuwa mstari wa mbele kumuunga mkono
Sitta alikwenda mbali kupingana na Nyerere dhidi ya uteuzi wa mh EL.
Hata pale wenzake akina JK, Lukuvi, Seif khatibu walipoonekana kunywea, Samwel alisimama kidete na Swahiba yake EL.
Harakati zake zilifika mwisho ndani ya NEC pale mwalimu alipomtaka Sitta kama waziri wa sheria asome faili la EL na kuwaeleza wapi alikuwa anaonewa.
Hapo hakuwa na ujanja bali kuahirisha harakati zake.
Samwel Sitta ni mmoja wa wanamtandao ambao si tu walinyanyasa watu wengine bali pia waliwadhalilisha baadhi ya viongozi kwa kutumia nafasi zao. Mtandao huo uliundwa ili kuwabomoa wazee kama akina Malecela na wengine, Sitta akiwa mshiriki.
Matarajio ya Samwel Sitta kuchukua nafasi yalizidi pale Nyerere alipohitimisha safari ya EL. Ikumbukwe mtandao uliendelea na harakati hadi chaguzi zilziomwingiza JK magogoni.
Sitta akatumia fursa hiyo kunyemelea kiti cha uwaziri mkuu kwa vile tu EL alishachafuka na hivyo hakuwa chaguo tena siku za mbeleni.
Katika hali isiyotarajiwa na akiongozwa na vigogo wa mtandao wenye nazo, JK alijikuta akimchagua EL. Jambo hilo halikuwa habari njema kwa Sitta .
Hata hivyo Sitta akiwa mwanamtandao akatunukiwa nafasi ya Uspika.
Zipo habari za yeye kuomba msafara kama kiongozi mkuu.
Hilo likakataliwa ndipo nyongo na chuki zikaanza, mtandao ukaanza kumeguka kidogo kidogo.
Ilipotokea nafasi ya Richmond, Sitta hakusita kuitumia vema na mzee wa Monduli akajikuta kaangukia pua.
Sehemu itaendelea..........
Richmond na viporo alivyofunika
Posho za wabunge na alivyowageuka wananchi
n.k