Mtanganyika
JF-Expert Member
- Jul 18, 2007
- 1,601
- 955
FJM,
Sijui kwanini unapoteza muda kujadiliana na Mtanganyika wakati kimsingi yupo upande wako wa hoja. Mnapopishana ni kwamba "mlinzi wa kweli wa muuungano ni vifaru na mizinga, sio wananchi". Vinginevyo ukimsoma, anakiri kwamba umma wa zanzibar na Tanganyika una kiu kubwa sana ya Tanganyika. Sasa kujadiliana na mtu wa aina hii inakuwa haina maana, ingekuwa na maana pale tu angekuwa anasema kwamba wananchi hawataki Tanganyika, huku yeye na makada wenzake ndani ya chama wakiachia mchakato uwe fair and transparent to prove that.
Hawa watu wanaweweseka, serikali tatu itawaathiri sana kimadaraka na vibaraka wao waliopo ambao hawapo tu CCM bali Chadema. Tunavyozungumza, they are indecisive kuhusu kugombea urais wa Tanganyika au Muungano, na nilishamwambia Mtanganyika kwenye mjadala wetu ule wa gharama za muungano, kwanini serikali tatu inawapa wakati mgumu sana. Hawana nia yoyote njema kwa wananchi, ni madaraka yao tu ndio yanawasumbua kwani yatayumbishwa sana na serikali tatu. Isitoshe, serikali tatu inapeleka madaraka karibu zaidi na wananchi kuliko serikali mbili. Wao wanataka madaraka yakae mbali kabisa na wananchi, hata ikibidi wayazuie na vifaru na mizinga.
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mchambuzi mimi nadhani nitakuwa wa mwisho kuchukua kadi ya CCM baada ya Mboe kuchukua then mimi, mimi naangalia uhalisia na najikita kwenye kusoma wakati. Nadhani kufanya dhana kwamba tutaona serikali ya tatu, hilo jambo nadhani halina nafasi katika bunge hili. Hivyo mimi mpenda serikali moja tuu ama ya Tanganyika au Tanzania siwezi kupata ninachokitaka na Wewe, Warioba na wengine wapenda serikali tatu sidhani kama hilo litawezekana kwa sasa, labda 2015 "Labda". Hivyo, wote tupo kwenye boti moja.
Nimefanya mchanganuo kwenye post moja hapo awali kwamba CCM ni asilimia 48% ya Bunge, Upinzania ni 18% na hawa "undecided" ambao wamechaguliwa na CCM ni 35%. Ili hoja ya Tanganyika ipite inabidi upate 100% of undecided, 100% of Upinzani na 41% ya CCM. Umeona hapa jinsi tunavyotofautiana kwenye kuelewa uhalisia? Kuwapata CCM hata 10% inabidi usukume ardhi na mbingu, na hii ni sababu ya strategic advantage ambayo CCM wanayo. Ndio maana kwenye mandiko yangu nikasema kama mchezo ni Last Card, basi CCM wana majoka yote manne. Lakini ili CCM washinde na idea zao wanatakiwa kupata wabunge 130 tuu kutoka kwenye hawa undecided. Na ukitazama muundo wa Tanzania 60% ya wananchi wanaelemea CCM. Hivyo technical CCM inatakiwa kubadili mioyo ya wabunge 20 tuu kwenye wale undecided.
Mimi nadhani hapa umegeuza script kuhusu wanaotaka Tanganyika na serikali mbili zaidi hao ndio wapenda madaraka. Kaka kama unadhani kwamba tukiongeza Tanganyika basi ndio tutaondoa CCM kwenye madaraka basi nadhani kweli tunatofautiana imani. Ukiwapa CCM Tanganyika watachukua na kuongoza, wataweka bunge la watu 300 (sababu wao ndio wataandika Katiba ya Tanganyika), Wataongoza muungano sababu wao ndio majority na watajaza watoto wao kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Ni ukweli usio fichika kwamba kama miujiza ikatokea Tanganyika ikazaliwa basi ni walewale watakao ongoza Tanzania Muungano na Tanganyika, ila sasa wataweka watu wao kwenye either Tanzania au Tanganyika. Lakini, ukiacha hayo yote kwa nini tupoteze muda kuanzisha kitu ambacho mimi na wewe wote tunajua kitakufa? Wazanzibar watakuja na kusema wanachangia serikali ya tatu lakini hawawezi kupata raisi sababu ya population, hivyo watataka kujitoa moja kwa moja. why waste time?
Ndio maana mimi nasema bora tulirudie hili jambo wakati wananchi wa Tanzania wakiwa na ufahamu.