Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
- Thread starter
- #41
SITTA ABADILI MSIMAMO, AKUBALI KATIBA YA CCM IJADILIWE
SITTA HAJALI NCHI TENA, SASA NI KIU YA URAIS NA 'BORA KATIBA'
Mswada wa sheria ya rasimu ulipopingwa bungeni, bunge la JMT liliupitisha kwa idadi ya wajumbe 100, chini ya 2/3 inayotakiwa. Hilo lilifanywa kwa nguvu ili kushinikiza mswada.
Mh Sitta akiwa mbunge na waziri alikuwepo ndani ya bunge.
Hakukemea kwasababu lilikuwa na mafao kwa CCM
Juzi wabunge wa UKAWA walipotoka nje ya ukumbi wa BMLK mh Sitta alisema majadiliano yataendelea kwavile akida imetimia ambayo ni 2/3 ya CCM na Mh Mrema.
Akidi ipi wakati kuanzia huko nyuma hakukuwa na suala la akidi mzee Sitta?
Ni sitta huyo huyo aliyeshindwa kukemea mswada uliopitishwa na watu 100 lakini akatumia wingi wa CCM bunge la katiba kuhalalisha kikao. Kwa wale msiomjua mzee huyu na undumila kuwili hya ni baadhi ya tu ya mambo ya mzee.
Mzee huyu alipofanya mbinu za kumnyanyasa Warioba kwa kumtanguliza mbele ili aadhibiwe na JK alisema busara zilimuongoza kwamba Rais azungumze baada ya Warioba.
Inashangaza kuona mzee huyo huyo ameshindwa kutumia busara kutambua kuwa katiba ni suala la nchi na si la chama.
Hadi sasa anachokifanya ni kuandika katiba ya CCM akitarajia kuwa katiba inayoandikwa itamwezesha kuteuliwa au kuwa Rais wa nchi hii.
Mzee Sitta anashindwa kutumia busara kubaini kuwa matatizo ya katiba anayoiandika na CCM si ya watu wa nje, ni ya watoto na wajukuu zake ambao huenda siku moja nyaraka hiyo hiyo ikaja kuwahukumu kama raia.
Na katika kuonyesha undumila kuwili na busara chache za mzee wetu, Sitta amependekeza muda zaidi wa kuchambua katiba.
Tunachojua ni kuwa anahitaji muda zaidi ili kuweza kufumua rasimu ya Warioba kwasababu muda uliopangwa hautoshi. Hilo mzee Sitta halioni kama gharama na upotezaji wa muda.
Ni upotezji wa muda kwasababu katiba ya CCM itafumuliwa pengine miaka chini ya 5 ijayo.
Je, hiyo ndio busara ya Sitta kwa kizazi hiki?
Katiba ya CCM inayoandaliwa inaweza kuzua vurugu nchini. Je, ndio busara za Rais mtarajiwa Sitta?
Ingawa anatumika kuhujumu wananchi kwa mategemeo ya Urais, Sitta atambue kuwa matendo, usaliti wa umma na undumila kuwili umeshahitimisha ndoto hizo kabla ya kuziota.
Tusemezane