Kwa maana waalimu mpaka leo hawajui kutumia vishikwambi? Mbona wana hang nazo mitaani?

Tajiri wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2022
Posts
1,079
Reaction score
2,947
#HABARI: Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI (Elimu), Dkt. Charles Msonde amewataka Maafisa Elimu Kata (MEK), kuwasimamia na kuwasidia Walimu namna kutumia vishikwambi walivyopewa kuwezesha ufundishaji na ujifunzaji, ili kuinua ubora wa elimu nchini.
.
Dkt. Msonde ametoa maelekezo hayo wakati akifunga Mafunzo endelevu ya walimu kazini (MEWAKA), kwa Maafisa elimu kata 1,209 yaliyofanyika katika chuo cha Ualimu Klerruu mkoani Iringa, ambapo ameendelea kusisitiza kuwa watumie vishkwambi hivyo kwa kuingia kwenye Maktaba Mtandao na Mfumo wa Kujifunza (LMS) wa Taasisi ya Elimu Tanzania ili kujipatia vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na mbinu mbalimbali za ufundishaji.
.
“Kupitia mafunzo haya ya MEWAKA mmefundishwa namna mnavyopaswa kutumia vishikwambi katika ufundishaji na ujifunzaji, hivyo nitoe rai kwenu kuhakikisha vinatumika ipasavyo kuinua ubora wa Elimu nchini” - Dkt. Charles Msonde
 
wao wanajua kote internet inashika sio!!???
 
Back
Top Bottom