Zionist
JF-Expert Member
- Dec 5, 2017
- 1,866
- 2,996
Habari wana JF,
Nimekua nikisikia kwamba barabarani Kuna vitimbwi vya mauza uza nikawa siamini, sasa ni juzi nilikua natoka Arusha kuelekea Kibaha. Nilifika sehemu jina silifahamu, ni kijiji baada ya kutoka Mombo.
Ni kwamba nikiwa kwenye mwendo alitokea mtu upande wa kushoto akawa anaingia barabarani Kama vile haioni gari nikapunguza mwendo na kupiga honi, nikitumaini jamaa atasimama ama kustuka, badala yake akaongeza spidi na kuliingia gari upande ule ule wa kushoto mimi na jamaa yangu tukasikia kishindo, side mirror ikavunjika ikaweka na kreki mbaya sana kwenye kioo cha mlango wa kushoto.
Nilisimamisha gari fasta tukashuka na kuangalia tunamuona yule mtu anakwenda tu kwa spidi ile ile, kama vile hakikutokea chochote. Tukawa tunashangaa basi yule mtu akaingia kama kwenye kichochoro Kati ya nyumba mbili, hii nyumba ya kulia Kuna jamaa alikua ameketi kibarazani amepaki pembeni gari aina ya vitz.
Tukamfuata jamaa yangu akamuuliza, Ndugu huyu mtu amekatiza hapa unamfahamu ? Maana tumemgonga na gari tumesimama ili tumtazame lakini cha kushangaza jamaa hakuanguka wala kuyumba ameelekea huku. Cha kushangaza tena, Jamaa akatuambia, nyie mpo salama? Tukamjibu ndio. Akasema basi shukuruni nyie endeleeni na safari. Nikamuuliza mbona hatuelewi?
Badala ya kujibu akabaki ametukazia macho jamaa yangu akanishika mkono na kunivuta tukaondoka. Lakini mpaka sasa hivi tumebaki na maswali vichwani mwetu.
Ni nini hasa kilitokea....
Asanteni