Zionist
JF-Expert Member
- Dec 5, 2017
- 1,866
- 2,996
- Thread starter
- #21
Hii dunia Kuna vingi hatuvijui mkuuMshukuru Mungu kwa kuwa upo salama mkuu
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii dunia Kuna vingi hatuvijui mkuuMshukuru Mungu kwa kuwa upo salama mkuu
Inawezekana kwa sababu si kwa ukauzu ulepoleni sana,au huyo Jamaa mliyekuwa mnamuliza kilikuwa kitu chake
Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana mkuu, ila Dunia imejaa hatari kila konaMkuu pole sana, mshukuru Mungu kwa kila jambo maana yeye hujua kila wazo, tendo na kusudi chini ya jua.
Sent using Jamii Forums mobile app
Alishikwa na bumbuwazi , katika hali hiyo angeeleza nini ? Ni vitu visivyoelezeka.--ngoja nifupishe,
Nakumbuka kuna siku 2012 nimepanda basi ya kampuni ya Satelite kutoka tanga kuelekea dar nikiwa nimekaa siti za karibu na mbele niliona dereva amepiga mabreki mengi gari ikayumba na tukasikia mlio mkubwa kwenye eneo la engine,a ila akaimudu na kuiweka sawa na akaweza kupaki pembeni ya barabara.
Wadau tukamgeukia dereva , "kulikoni unataka kutumwaga ?"
Akatujibu kuwa alikua ameona Kanga (ndege jamii ya kuku) na akamgonga ndio yule tulisikia kwenye engine,
Tukashuka na eneo la mbele la engin likafunguliwa, hatukukuta damu, manyoya wala dalili zozote za kugongwa kitu ila kitu pekee tulichokikuta ni fan belt iliokatika.
Tukajaribu kukagua huku na kule hatukukuta kitu chochote na safari yetu ikawa ndio mwisho mpaka ilipoletwa basi nyingine kutuchukua.
Mpaka leo hii sijaweza kujua ni kitu gani kilitokea japo dereva alikomalia msimamo wake
Kama una roho nyepesi ndio mwisho wa kuendesha masafa marefu [emoji851][emoji851]Jamaa yangu alikuwa kwenye spidi kubwa maneneo ya Mikumi,akatokea mtu anakuja kwa kasi kuelekea kwenye gari,alikuwa na mwenzake kwenye gari akamwambia mgonge usifunge beak,jamaa akanyoosha,walisikia kishindo na mtu alieogongwa amepita kwenye kioo cha mbele kuelekea nyuma,hawakusimama walipofika Mikumi kwenye mji wakasimama na kuchukua chumba,kesho yake wanaangalia gari halina mchubuko wala taa iliovunjika,kufika Dar jamaa akaamua kuuza gari...
Kwa sisi tunaoenda safari ndefu, tunaambiwa hao ni majini wasumbufu tu.Kuna siku ilikuwa 2007. Nikitoka Arusha kwenda Dar saa Saba Nane usiku nilikuwa napita maeneo ya kwedikwazu. Kuna mahala Barbara imenyooka Sana Basi nikawa natembea speed 100-120.
Kuna mrembo mmoja mdada akawa anasimamisha gari akiomba lift. Nikapiga taa kubwa kumwona vizuri mrembo haswaa, sikusimama nikanuoosha goti, huku najiuliza huyu anaenda Wapi saa hizi,. Bwana ile nampita kwa speed ile alinipiga busu Mara tatu hapo dirishani. Maana sikuwa nimefunga madirisha ili nipigwe upepo nisilale. Nilifika dar Sina raha kutwa nzima.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo sijawahi mkuuIvi nyie mlishawahi kuona ziwa (lake) barabarani.?
Kwa sasa hivi napumzika kidogo nisahau ile issueUsiku una mengi sana. Mnaoendesha mna mioyo ya akajabu. Ikishafikaga saa sita usiku niko safarini sikai kwa amani kabisa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Duuh mkuu aliweza kuja dirishani huku upo speed hyoo?Kuna siku ilikuwa 2007. Nikitoka Arusha kwenda Dar saa Saba Nane usiku nilikuwa napita maeneo ya kwedikwazu. Kuna mahala Barbara imenyooka Sana Basi nikawa natembea speed 100-120.
Kuna mrembo mmoja mdada akawa anasimamisha gari akiomba lift. Nikapiga taa kubwa kumwona vizuri mrembo haswaa, sikusimama nikanuoosha goti, huku najiuliza huyu anaenda Wapi saa hizi,. Bwana ile nampita kwa speed ile alinipiga busu Mara tatu hapo dirishani. Maana sikuwa nimefunga madirisha ili nipigwe upepo nisilale. Nilifika dar Sina raha kutwa nzima.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, now ushakuwa mzoefuM
Mimi huwa nanyoosha goti tu sikwepi kitu mwaka 1993 nilimkwepa mbuzi nikajikuta niko mtaroni hata mbuzi simuoni tena LEYLAND la watu likiwa chakari cabin imebonyea ila sikuumia