Kwa ‘madudu’ haya kwenye ripoti ya CAG, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa achia ngazi

Kwa ‘madudu’ haya kwenye ripoti ya CAG, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa achia ngazi

Cosovo

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2018
Posts
667
Reaction score
1,810
Ripoti hii ya CAG imeacha Serikali uchi na Waziri Mkuu kiongozi wa shughuli za kila siku za Serikali na msimamizi wa shughuli za Serikali za kila siku anapaswa aachie ngazi mara moja.

Ni aibu kwa madudu haya mpaka sasa upo ofisini, unafanya nini? Ona aibu mwenyewe uchukue hatua kwa heshima yako.

Nashangaa Mawaziri wanavyokuwa na makamera kuwajibisha vidagaa, wakuu wa shule kisa milioni 2 haikufanya manunuzi sahihi na huku mapapa wanakula watakavyo.

Kassim Majaliwa must go
 
Waziri Mkuu na Kamati Ya Usimamizi Wa Serikali (PAC) ya bungeni yote, wanatakiwa wajiuzulu haraka sana kwa maslahi ya taifa letu. Hii ni kashfa kubwa haijawahi kutokea nchini tokea tumepata uhuru.

Hata kashfa za Richmond/Dowans/Escrow hazijafikia kiasi hichi, hizo kashfa zote za ufisdai hata ukizionganisha pamoja hazijafikia hii ya safari hii.

"SPEAKER JOB NDUGAI" akumbushwe CAG Prof Assad alifanya ukaguzi wa mahesabu ya serikali, na aligundua huu ushenzi na madudu yote yaliofanyika... Ila aliposema kweli na kuweka wazi report yake, alikua mkali na kiherehere namba moja kumkashifu, kumwekea tamko la kutokufanya nae kazi, na kumdhalilisha kwa kumvua mkanda mpaka viatu siku anaingia bungeni.

Sasa, CAG Kichere nae ameongea yale yale aliosema mwalimu wake CAG Prof Assad. Na yeye weka zuio la kufanya nae kazi bungeni!!!
 
Mimi na fikiri ni wakati sasa bunge likandika historia ya kuwajibisha baadhi ya walikua wasaidizi wa mwenda zake. Kumlenga PM ni kurudia yale yanayo itwa makosa pale ya bandarini. Kuwa huko nyuma waliwajibishwa wa chini hadi cheo cha cf.

Hii tunataka bunge limuwajibishe mpaka aliye kuwa ni boss wa PM kwa madudu haya tunayo aminishwa. PM asiwe bangusilo. Aliye kuwa boss wa PM ajitathimini mwenyewe.
 
Kama haya mambo ya mikataba wataendelea kuachiwa CCM peke yao wayafanye, nina hakika kuna siku litatokea kubwa zaidi ndio akili zetu zitakaa sawa, nionavyo sasa hivi hii issue ya ripoti ya CAG imepokelewa kwa ushabiki zaidi watu badala wajadili namna ya kumaliza tatizo wanapoteza muda wote kumshambulia marehemu, wameshasahau system iliyomuweka marehemu madarakani bado tunayo mpaka sasa na ndio hiyo hiyo bado inatuwekea viongozi mpaka leo kwa sababu ya ubovu wa Katiba yetu.

Kila mwaka kila awamu CAG hutoa ripoti za aina hii, japo sasa wanajiliwaza huu ufisadi uliotokea haujawahi kutokea kabla, ni kama vile wanasema na wamekubali bora waibiwe kidogo kuliko kuibiwa sana, lakini hata kama hayo madudu hufuniliwa kila mwaka, wahusika huchukuliwa hatua gani? mara zote hulindana, ila bado tunapoteza muda mwingi kushangilia mambo ambayo hujirudia kila mwaka badala ya kutafuta solution ya tatizo angalau ya muda mfupi.

Nachojifunza kwenye hili sakata la ripoti ya CAG, ni kama vile watu walikuwa na chuki binafsi na mwendazake na sio chama chake au system iliyomuweka madarakani, na lakushangaza zaidi hao wapiga filimbi wengine ni "plastic opposition fans" wanaosikia mdundo wa ngoma lumumba, wao wanakata mauno mtaa wa tatu.

Nionavyo, ni bora sasa hii mikataba inayoingia serikali iwekwe wazi kila mwananchi aione, iwe ni kutangazwa kwenye magazeti ya serikali au pengine popote, muhimu mikataba iwekwe wazi watu waisome waichambue kabla ya kusaini na hayo makampuni, kuendelea kushangilia madudu yanayotangazwa na CAG kila mwaka tutadumaa kama taifa, ama sivyo tutaendelea kuchezeshwa ngoma na CCM kila wakati.
 
Ndugai aliyetumia bilioni 17 kujitibu fangus india asingeweza kumkemea jiwe.wote hao wana ukwasi wa kutisha.ndugai.jiwe.kigwangala.makonda na majaliwa ni mabilionaire
 
Uko sawa Mkuu cosovo kuna mengi ya kujiuliza , Mkuu wa shule anasimamishwa kazi kwa million mbili tatu na kwa mbwembwe kubwa atupishe ameshindwa kuendana na kasi ya awamu ya tano lakini kuna mawaziri na wengine wametumia mabilioni wapo wanadunda mitaani na mvx.

Wakati huo huo kuna watumishi wa umma hawajaongezewa mishahara wala kupanda madaraja kwa zaidi ya miaka mitano lakini kuna wasanii na vituo vya redio na TV wamelipwa mamillion ya shilingi za walipa kodi wa nchi hii.

Wakati huo huo kuna watumishi wa umma wanakamuliwa na board ya mikopo ya elimu ya juu hadi retention fee. We have long way to go
 
Mimi na fikiri ni wakati sasa bunge likandika historia ya kuwajibisha baadhi ya walikua wasaidizi wa mwenda zake. Kumlenga PM ni kurudia yale yanayo itwa makosa pale ya bandarini. Kuwa huko nyuma waliwajibishwa wa chini hadi cheo cha cf.

Hii tunataka bunge limuwajibishe mpaka aliye kuwa ni boss wa PM kwa madudu haya tunayo aminishwa. PM asiwe bangusilo. Aliye kuwa boss wa PM ajitathimini mwenyewe.
hahaha wewe unafikiria, hujui kama ni serikali ya ccm hii, ongea na kamati kuu ya ccm watakusikiliza. Tatizo lenu hujulipua kama mmekatwa kichwa,
 
Hata Namungo Fc inatakiwa ichunguzwe namna inavyojiendesha
 
Ripoti hii ya CAG imeacha Serikali uchi na Waziri Mkuu kiongozi wa shughuli za kila siku za Serikali na msimamizi wa shughuli za Serikali za kila siku anapaswa aachie ngazi mara moja.

Ni aibu kwa madudu haya mpaka sasa upo ofisini, unafanya nini? Ona aibu mwenyewe uchukue hatua kwa heshima yako.

Nashangaa Mawaziri wanavyokuwa na makamera kuwajibisha vidagaa, wakuu wa shule kisa milioni 2 haikufanya manunuzi sahihi na huku mapapa wanakula watakavyo.

Kassim Majaliwa must go
Tuandae online petition nn watu wasign, PM aondoke. Lengo ni uwajibikaji ili next time watu wajifunze.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Inatakiwa kuanzia Samia na cabinet yake yotete na bunge zima waachie ngazi kumwandama majaliwa peke yake ni kumuonea MPANGO awaeleze wananchi
 
Ripoti hii ya CAG imeacha Serikali uchi na Waziri Mkuu kiongozi wa shughuli za kila siku za Serikali na msimamizi wa shughuli za Serikali za kila siku anapaswa aachie ngazi mara moja.

Ni aibu kwa madudu haya mpaka sasa upo ofisini, unafanya nini? Ona aibu mwenyewe uchukue hatua kwa heshima yako.

Nashangaa Mawaziri wanavyokuwa na makamera kuwajibisha vidagaa, wakuu wa shule kisa milioni 2 haikufanya manunuzi sahihi na huku mapapa wanakula watakavyo.

Kassim Majaliwa must go
Kwa walio kuwepo wote waachie au yeye tu
 
Back
Top Bottom