Unaonekana mwelewa na asante..
1. Hasara ya ATCL inatokana na Break Even point ama upya wa biashara yake na corona...
Unaweza kukubaliana na hilo?
Asante sana mkuu, hakika una hoja za kuchangamsha kuchwa kuliko wengine. Sasa twende pamoja,
Sikatai kwamba, Corona Virusi ni sababu moja wapo ilioakisi hasara ya ATCL na mashirika mengine ya ndege duniani, ila Corona sio sababu ya kusababisha
Beyond Margin Loss kutoka 2015 - 2021 kwa Air Tanzania.
1) Corona Virus ilianza mwaka 2019 (Covid-19). Hasara ya ATCL ilianza 2015 mpaka 2021. Kuna utofauti wa miaka 4 hapo ambayo Corona haikuwepo na haiwezi kutumika kama sababu kuu.
2) Air Tanzania route zake nyingi ni za ndani ya nchi, kila siku. Kwa Tanzania, Corona haijawahi kusababisha route za ndege kusimamishwa (Hakuna Lock Down) wala biashara kufungwa. - Ingekua Air Tanzania route zake zote ni za nje ya nchi, basi ningekubaliana na wewe.
3) Air Tanzania ndio ilikua kitovu cha serikali ya magufuli kuuwa mashirika ya
FAST JET na
PRECISION AIR ili shirika liweze kufanya
MONOPOLY YA BIASHARA YA ANGA. Na ilifanikiwa kuwakandamiza mahasimu wake kibiashara.
4) Shirika la ndege la Air Tanzania lilianzishwa mnamo mwaka 1977 (Kama Sijakosea) baada ya kufa kwa EAC, hivo shirika la Air Tanzania sio
GENI/JIPYA kibiashara ya maswala ya ndege na anga. Sikatai halikuwa na ndege na mengineyo mengi:
Maswali;
A) Swala la upya wa biashara kwa shirika lenye umri zaidi ya miaka 44 inakuja akilini kweli??? Kwa muda wote huo hawaijui biashara ya ndege na utendaji wake kazi???
B) Upya wa biashara au kufufua biashara
unachukua zaidi ya miaka 5 tena kwa shirika lenye kukingiwa kifua na dola na lililo na msamaha wa kodi???
C) Corona imeathiri vipi biashara ya Air Tanzania, wakati shirika linategemea route za ndani ya nchi (Geita, Mwanza, Dar n.k) ambazo hazikufungwa kwasababu ya Corona???
KUMBUKA: Magufuli alituaminisha shirika la ATCL linaendeshwa kwa faida, na kufikia kutoa gawio kwa serikali la faida kwa kutumia vyombo vya habari -
HII NAYO IMEKAAJE MKUU???