Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,443
- 4,006
Kwa hicho ulichokiandika unamwonea waziri mkuu.Ripoti hii ya CAG imeacha Serikali uchi na Waziri Mkuu kiongozi wa shughuli za kila siku za Serikali na msimamizi wa shughuli za Serikali za kila siku anapaswa aachie ngazi mara moja....
Waziri wa fedha kwa kipindi husika, Tamisemi, Mwenyekiti kamati PAC/Local governmanet, makamu wa Rais kipindi husika, mwanasheria mkuu wa serikali kipindi husika, mawaziri na makatibu wakuu katika wizara na idara kwa kipindi husika na ripoti ya kukaguliwa CAG nayo iwekwe bayana.
Wote waliowahi kuhudumu katika serikali na mashirika ya umma kwa kipindi husika kwenye nafasi ya utangaji sera na maamuzi.
WAJIUZULU
1. Wanasiasa-Uchaguzi mpya uitishwe.
2.Watendaji-ajira zisitishwe na uchunguzi wa kijinai ufanyike kisha hatua za kisheria zichukue mkondo wake;
3. Ipigwe kura ya kutokuwa na imani na serikali iliyopo kwa kuanza kuwalaghai wananchi kana kwamba hawakuwemo kama sehemu ya ubadhirifu na upotevu wa mali ya umma.
4. Rais iliyepo anaonesha kwa uwazi kabisa alikuwa na nongwa na hayati ila wakati wa uhai wake aliifichakwa sababu anazozijua mwenyewe.
Wananchi wanafahamu vizuri hatua kwa hatua ni kilitokea baada ya kutoka kufungua mradi wa polisi huko Kurasini, kujisikia vibaya, kukimbizwa muhimbili kisha kuhamishiwa hospitali ya Mzena hadi mauti.
Viongozi wa kisiasa, watendaji wa serikali, mashirika ya umma, wafanyabiashara na viongozi wa kidini (sio wa kiroho) ACHENI kuonesha chuki na VISASI vyenu dhahiri kwa umma dhidi ya hayati na wateule wake huku mkijua milkuwa sehemu ya hali hiyo. Kwa sasa hata mkichafua namna gani hayati Magufuli hao wananchi wa chini ambao ndio wapiga kura hawawezi kuwaelewa kwa vyovyote vile. Mlitakiwa msubiri muanze kuonesha mabadiliko halisi badala ya maneno matupu.
Kwa sa Tanzania itakuwa na historia ya uongozi wa kisiasa kwa ngazi ya Rais kwa kipindi kimoja tu kutoka ichama tawala hadi cha upinzani hata kama hakuna katiba mpya. Mnaweza kuleta ubishi kwamba watumia dola, hilo haliwezekani na somo halisi mtafundishwa muda mchache ujao.
Kuna chama cha upinzani kitashika madaraka pamoja na kwamba walikuwa wakosoaji wakubwa na kuzusha hofu kwamba wanaweza kuhatarisha amani ya nchi, itakuwa kinyume chake, hatafanya visasi, hatadharau jitihadi za viongozi waliotangulia na watachochea maendeleo ya kweli na kuaminiwa sana.
Kesho inaijua Mungu pekee hakuna mwenye hati na dhamana ya pumziko la wajibu.