JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mtangazaji wa Wasafi FM, Ricardo Momo amenukuliwa katika session yake redio akidai kuwa wale wazee wa klabu waliozungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa watashitaki kwa Rais Samia Suluhu kuhusu klabu yao kuonewa, wamefanya hivyo kwa kuwa kuna kiongozi wa Serikali ambaye yuko nyuma ya pazia.
Momo hajataja jina la klabu lakini wote tunajua kuwa anamaanisha Yanga, kwani hao ndiyo ambao walifanya ‘press’ mara mbili, kwanza na Haji Manara na Hassan Bumbuli pamoja na ile ya wazee wa Yanga, anadai kuwa kuna kiongozi mwenye nguvu Serikalini ndiyo anawakandamiza Yanga.
Momo amerukaruka katika maelezo yake pasipo kutaja majina, na inavyoonekana kuna huyo kigogo wa Serikalini ni shabiki au mdau wa upande wa pili (inawezekana anamaanisha Simba), ndiyo maana Yanga wameanza kuwa na wasiwasi kuwa wanaweza kukandamizwa katika mbio zao ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la Azam Federation msimu huu.
Unadhani Momo yuko sahihi na kwa nini Yanga wanakuwa na wasiwasi wakati wanaongoza ligi tena kwa pointi nane na cha mwisho unadhani huyo kiongozi anayemzungumzia Momo ni nani?
Tujadiliane ndugu zangu!