Kwa mahojiano haya ya Deo Bonge na Ayo, atakuwa 'amefinywa'? Asema aachwe apumzike, analiamini Jeshi la Polisi kufanya kazi yake

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Millard kafanya mahojiano na bonge kueleza kwa undani kilkchotokea. Tunamjua Millard🌚🌚... mnasemaje wakuu?

Wazee wa kusoma kuread between the lines na kuangalia body language, ukiangalia maswali ya Ayo TV na majibu ya Bonge, unapata conclusion gani?

Naomba pia ujikumbushe kwenye uzi niliweka juzi (nimeanza kuwa kama Pascal Mayalla kwarudisha nyuma kiintelijensia tuunge dots😀😀): Utekaji kuhusishwa na uhasama wa kibiashara ni namna ya kuwaepusha wahusika halisi kuwajibika? Tukio Dar24 limeishaje?

Deo amenza kwa kumshuru Mungu na Watanzania walioguswa na tukio lile na kupaza sauti zao, ameuhakikishia umma kuwa yupo salama kabisa. Pia amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kumpa ushirikiano wa hali ya juu toka tikio lilipotokea mpaka sasa, bado ana imani na jeshi la polisi kuwa watakamilisha kazi yao ili haki iweze kupatikana.

Deo amesema tuliamini Jeshi la Polisi kuwa watafanya kazi yao kwa weledi na kwamba yeye hawezi kuzungumzia lolote kuhusu lile tukio kwasababu linafanyiwa uchunguzi na jeshi la polisi, uchunguzi huo ukikamilika watatoa taarifa zaidi.

Mwandishi kamuuliza kuhusu tukio hili kuhusika na siasa kwa kuandika kwenye mitandao kuhusu siasa ama kuigusa serikali kwa namna yote; akijibu swali hili Deo amesema hapana, tukio lile halina itikadi ya siasa sababu yeye siyo mwanasiasa au ‘mtu wa kuandika andika mtandaoni’, mwandishi akauliza tena kwahiyo tukio lipo zaidi kibiashara… Deo akajibu kama nilivyosema siwezi kuliongelea zaidi, tuache Jeshi la Polisi wafanye kazi yao.

Kuhusu watu kutofanya lolote na kuacha apambane mwenyewe, Deo amewaasa watanzania kuongeza umoja na kushirikiana unapoona mwenzako amepata tatizo, leo linaweza kuwa kwake siku nyingine likatokea kwako msomaji. Unaweza usiingia kuanza kushikana na watekaji lakini ukahoji kinachoendelea na kupaza sauti apate usaidizi.

Mwandishi amemuuliza kama anaona kuna mwanga kwenye ufuatiliaji wa Jeshi la Polisi kama haki itapatikana, Deo amejibu ana imani Jeshi la Polisi litafanya kazi yake.

Deo ameongeza kuwa baada ya majohinao haya na Ayo TV tuache Jeshi la polisi lifanye kazi yake, ameshatoa taarifa kuwa yupo salama, basi vyombo vya habari vimuache apumue, uchunguzi ukimalika na Jeshi la Polisi likitoa taarifa yake labda hapo ndio ataweza kuongea tena.

Mwandishi akamwambia atuhadithie kidogo ilivyokuwa mpaka akaweza kujinasua, Deo amesisitiza tena kuwa maelezo mengine yatatolewa na Jeshi la Polisi.
 
Mbona izi videos za humu JF zinakuaga ngumu sana kufunguka haijalishi mtandao wangu una kasi kiasi gani au shida ipo kwangu tu? Badala yake huwa nalazimika kuzidownload kitu ambacho hakichukui hata dakika
Screenshot_20241115-074318.png
 
Siyo Ayo bali Deo Bonge kaambiwa asifunguke kwa vyombo vya habari..

Ndani ya siku mbili mwili umeisha.
Soma between them lines Mkuu (Ayo anasifika kwa nini? Wanagpi wametekwa hajaenda kuwahoji? Kwanini Bonge? Maswali anayomuuliza na conclusion ya Bonge)
 
Wakuu,

Millard kafanya mahojiano na bonge kueleza kwa undani kilkchotokea. Tunamjua Millard🌚🌚... mnasemaje wakuu?

Wazee wa kusoma kuread between the lines na kuangalia body language, ukiangalia maswali ya Ayo TV na majibu ya Bonge, unapata conclusion gani?

Naomba pia ujikumbushe kwenye uzi niliweka juzi (nimeanza kuwa kama Pascal Mayalla kwarudisha nyuma kiintelijia tuunge dots😀😀): Utekaji kuhusishwa na uhasama wa kibiashara ni namna ya kuwaepusha wahusika halisi kuwajibika? Tukio Dar24 limeishaje?

View attachment 3152607
Huyo ana misala yake usiyo ya kisiasa tatizo chadema wanataka wamtumie kama millage
 
Wakuu,

Millard kafanya mahojiano na bonge kueleza kwa undani kilkchotokea. Tunamjua Millard🌚🌚... mnasemaje wakuu?

Wazee wa kusoma kuread between the lines na kuangalia body language, ukiangalia maswali ya Ayo TV na majibu ya Bonge, unapata conclusion gani?

Naomba pia ujikumbushe kwenye uzi niliweka juzi (nimeanza kuwa kama Pascal Mayalla kwarudisha nyuma kiintelijia tuunge dots😀😀): Utekaji kuhusishwa na uhasama wa kibiashara ni namna ya kuwaepusha wahusika halisi kuwajibika? Tukio Dar24 limeishaje?

View attachment 3152607
Ukiona hivyo itakuwa yeye ndio ana jambo na angependa huruma upande ule. Ndio maana anafukia katika hali ya kawaida huwezi hata kushindwa kueleza tukio lilikuwa je anasema Jeshi la Polisi litaeleza wakati mwenye tukio ni yeye ni ajabu kabisa.
 
Mbona izi videos za humu JF zinakuaga ngumu sana kufunguka haijalishi mtandao wangu una kasi kiasi gani au shida ipo kwangu tu? Badala yake huwa nalazimika kuzidownload kitu ambacho hakichukui hata dakika
View attachment 3152613
Kama umenotice kipindi hiki telegram na JF kumekuwa na shida kiasi kuingia tofauti na mitandao mingine..... tunaenda kwenye uchaguzi Mkuu, jiongeze.... hakikisha hukosi VPN kwenye simu yako...... incase wakikaza zaidi kama kipindi kile ikafikia mitandao yote hutakuwa unakosa taarifa
 
Wakuu,

Millard kafanya mahojiano na bonge kueleza kwa undani kilkchotokea. Tunamjua Millard🌚🌚... mnasemaje wakuu?

Wazee wa kusoma kuread between the lines na kuangalia body language, ukiangalia maswali ya Ayo TV na majibu ya Bonge, unapata conclusion gani?

Naomba pia ujikumbushe kwenye uzi niliweka juzi (nimeanza kuwa kama Pascal Mayalla kwarudisha nyuma kiintelijensia tuunge dots😀😀): Utekaji kuhusishwa na uhasama wa kibiashara ni namna ya kuwaepusha wahusika halisi kuwajibika? Tukio Dar24 limeishaje?

Deo amenza kwa kumshuru Mungu na Watanzania walioguswa na tukio lile na kupaza sauti zao, ameuhakikishia umma kuwa yupo salama kabisa. Pia amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kumpa ushirikiano wa hali ya juu toka tikio lilipotokea mpaka sasa, bado ana imani na jeshi la polisi kuwa watakamilisha kazi yao ili haki iweze kupatikana.

Deo amesema tuliamini Jeshi la Polisi kuwa watafanya kazi yao kwa weledi na kwamba yeye hawezi kuzungumzia lolote kuhusu lile tukio kwasababu linafanyiwa uchunguzi na jeshi la polisi, uchunguzi huo ukikamilika watatoa taarifa zaidi.

Mwandishi kamuuliza kuhusu tukio hili kuhusika na siasa kwa kuandika kwenye mitandao kuhusu siasa ama kuigusa serikali kwa namna yote; akijibu swali hili Deo amesema hapana, tukio lile halina itikadi ya siasa sababu yeye siyo mwanasiasa au ‘mtu wa kuandika andika mtandaoni’, mwandishi akauliza tena kwahiyo tukio lipo zaidi kibiashara… Deo akajibu kama nilivyosema siwezi kuliongelea zaidi, tuache Jeshi la Polisi wafanye kazi yao.

Kuhusu watu kutofanya lolote na kuacha apambane mwenyewe, Deo amewaasa watanzania kuongeza umoja na kushirikiana unapoona mwenzako amepata tatizo, leo linaweza kuwa kwake siku nyingine likatokea kwako msomaji. Unaweza usiingia kuanza kushikana na watekaji lakini ukahoji kinachoendelea na kupaza sauti apate usaidizi.

Mwandishi amemuuliza kama anaona kuna mwanga kwenye ufuatiliaji wa Jeshi la Polisi kama haki itapatikana, Deo amejibu ana imani Jeshi la Polisi litafanya kazi yake.

Deo ameongeza kuwa baada ya majohinao haya na Ayo TV tuache Jeshi la polisi lifanye kazi yake, ameshatoa taarifa kuwa yupo salama, basi vyombo vya habari vimuache apumue, uchunguzi ukimalika na Jeshi la Polisi likitoa taarifa yake labda hapo ndio ataweza kuongea tena.

Mwandishi akamwambia atuhadithie kidogo ilivyokuwa mpaka akaweza kujinasua, Deo amesisitiza tena kuwa maelezo mengine yatatolewa na Jeshi la Polisi.
Hauna jipya, usilazimishe tuandike vyakusadikika, subiri jeshi la polisi lifanye kazi yake.
 
Back
Top Bottom