Kwa maisha wanayoishi ndugu zake Harmonize halafu nikimuona anatoa mil 9 kwa wengine, inaniuma sana

Kwa maisha wanayoishi ndugu zake Harmonize halafu nikimuona anatoa mil 9 kwa wengine, inaniuma sana

Hakuna watu wanafki kama ndg, afadhali kidoogo wa tumbo moja, ngd wengi watakuona wa maana ukiwa nacho ukiwa huna hawana muda na ww utapigwa majungu mpaka basi yan, ndg mkubwa ni mama yako tuu alafu wengine ata ukiwasaidia hawasaidiki
 
Kwa wanaowafahamu ndugu zake na Konde boy Mtwara halafu Dogo akifika Dar anagawa Pesa kwa wengine inaniuma sana hata kama siyo ndugu zangu! Ingefaa dogo aanze kuwasaidia ndugu zake kwanza wote watoke kimaisha, ndipo umwage pesa ovyo ovyo kuliko kufanya hivi wakati ndugu zake walio wengi tunaowafahamu bado wanapambana na hali zao kwa kulima mhogo huko Mtwara

Kwa watu wa Mtwara mtaelewa ninachokisema na kukimaanisha hapa, tofauti na wanaume wa Dar
Mtoa mada umenigusa sana, mimi napafahamu anapoishi mama yake mzazi njia ya kwenda Kijichi kutokea mbagala mission, tena ni bondeni kwenye mkondo wa maji. Watu wanatafuta umaarufu kwa nje wakati nyumbani shida ziko hadi mlangoni. Mungu atusaidie tujitambuwe.
 
Ywewe ndugu zako walivyo na shida hivi yaani unanunua bundle na kumsema huyu kijana. Bora hiyo pesa ya bundle ungewasaidia nduguzo.

Kweli, hii pesa ya bundle bora angewanunulia kandambili wadogo zake kijijini wanatembea pekupeku.
 
Ni kweli mkuu...Mimi mwenyewe huyo
"Mayonnaise" ni mtoto wa shangazi lakini hajawahi kunipa hata mia mie nateseka hapa kijijini na biashara yangu ya majeneza.! Nilishamwambia anisaidie japo kupata masoko ya bidhaa zangu huko Dar lakn wapi.!
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Nimecheka balaa.!
 
Kwa wanaowafahamu ndugu zake na Konde boy Mtwara halafu Dogo akifika Dar anagawa Pesa kwa wengine inaniuma sana hata kama siyo ndugu zangu! Ingefaa dogo aanze kuwasaidia ndugu zake kwanza wote watoke kimaisha, ndipo umwage pesa ovyo ovyo kuliko kufanya hivi wakati ndugu zake walio wengi tunaowafahamu bado wanapambana na hali zao kwa kulima mhogo huko Mtwara

Kwa watu wa Mtwara mtaelewa ninachokisema na kukimaanisha hapa, tofauti na wanaume wa Dar
Si juzi tu hapa alitoa msaada wa fimbo nyeupe kwa watu wenye ulemavu wa macho au sio huyu unaemzungumzia
 
Daaah, thanks my mama. Matatizo kibao yamenikuta lkn mama yupo upande wangu. Naumwa hadi demu wangu na ndugu hawataki kuja kunitembelea. Nikipona utaskia ndugu ushuzi wanaanza unajua yule kijana wangu kamaliza form six ila hana mkopo. Tusaidie basi hata ada. Ndugu ni Wanafiki wakubwa. Yule aliye pembeni yako kwenye matatizo msaidie, ila wengine Piga chini.
 
Hata we we hiyo buku 2 ya bando unayotumia kufuatilia maisha ya wenzio kwenye mitandao ingeweza kabisa kumlisha mlo wa siku nzima au kununua panadol kwa ndugu yako huko kijijini kwenu.. So acha ujinga ishi maisha yako na upambane na halo yako.. Period!

Wewe ndiyo mjinga, wazungu wanasema charity begins at home.
 
Hao ndugu zake kijijini ni walemavu??? kwanini wasipambane na hali zao

Umeambiwa wanalima NA wako hai, inamaanisha wanajitahidi. Huyu ndugu H angeweza kuwasaidi kuwekeza kwenye hicho kilimo chao, kuwanunulia trekta NA kuongeza mashamba, hiyo familia ingebadilika kimaisha.
 
Kwa wanaowafahamu ndugu zake na Konde boy Mtwara halafu Dogo akifika Dar anagawa Pesa kwa wengine inaniuma sana hata kama siyo ndugu zangu! Ingefaa dogo aanze kuwasaidia ndugu zake kwanza wote watoke kimaisha, ndipo umwage pesa ovyo ovyo kuliko kufanya hivi wakati ndugu zake walio wengi tunaowafahamu bado wanapambana na hali zao kwa kulima mhogo huko Mtwara

Kwa watu wa Mtwara mtaelewa ninachokisema na kukimaanisha hapa, tofauti na wanaume wa Dar
Unaweza kuta hao ndugu zake walikuwa wanapambana usiku na mchana asifanikiwe
 
Kama umetoboa kimaisha,ukitaka ndugu nao wafanikiwe uwatie hasira ya kupambana na maisha,ukianza kuwagawia hela kaa ukijua unawatengenezea umaskini
 
Wakati mwingine watu maarufu hufanya hivyo(kutoa pesa au misaada) kwa ajili ya kujenga majina yao. Sio kama wana upendo wa kweli kwa hao wanaowasaidia, bali ni kwa kuangalia jinsi inavyoweza kuwatangaza.
They call it STUNTS
 
Back
Top Bottom