Kwa majibu haya ya daktari nina hofu na afya yangu

Kwa majibu haya ya daktari nina hofu na afya yangu

100byte

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
220
Reaction score
61
Wiki iliyopita nilikwenda hospitali ambayo ni private, ni baada ya kutojisikia vizuri kiafya, baada ya maelezo yangu ilionekana nipime Malaria (BS) pia dr akaandika na kipimo kingine kilichosomeka Correctol katika karatasi lao. majibu yalipotoka, kwenye BS ilikuwa NIL lakini hiki kipimo kingine kiliandikwa POSITIVE. na niliambiwa hicho ni kipimo cha Typhoid. nikahoji hiyo Typhoid iko ngapi? wakasema haionyeshi ni ngapi na nikitaka kujua ni ngapi ni mpaka vipimo vikae masaa 24. Naombeni msaada kwa wanaojua haya mambo Napata hofu isije kuwa ni POSITIVE ya HIV na pengine nimedanganywa tu kuambiwa ni Typhoid ASANTENI
 
Pole mkuu..
Sidhani kama dr kakudanganya, kwa faida gani labda?

Basi nenda sehemu nyingne kapime..
 
Pole mkuu..
Sidhani kama dr kakudanganya, kwa faida gani labda?

Basi nenda sehemu nyingne kapime..

Labda hofu yake ni dokta kutokuwa muwazi kwamba anaambiwa anapima taiford lakini namna ya ujaji wa majibu,,,,, maana taiford huwa inaandikwa let say 1/180 ,,,,,,lakini hapa wamemwaandikia neno Positive tu bila nyongeza,,,,, ni mtazamo wangu tuuu,,,
 
+postive ni magonjwa ya zinaa
kama yepi mkuu? maana nina zaidi ya mwaka sasa niko peke yangu, je inawezekana kwa muda wote huo kuja kuonekana sasa huo ugonjwa wa zinaa?? nisaidieni tafadhali.
 
Acheni kwenda zahanati za vichochoroni.

Mkuu hii hospitali niliyokwenda ni kubwa kubwa tuu sema huwa wanapenda sana kuajiri cheap labaour hawana hata maadili ya kazi zao hapa nilipo sina amani natafakari sijapata majibu
 
Mkuu pole sana kwa kupata na hofu.. Nenda hospitali nyingine kupata uhakika wa Afya yako ili uishi kwa amani.. Hofu imenikuta kama ww lakini nilipoenda hospital mambo yalikua safi kabisaa

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
sijawah skia test inaitwa correctol

na screening test for typhoid ni widal test

majibu yakiwa negative unapewa majibu yako yakiwa positive ina bid wafanye titration

sasa wew hyo correctol ungemuuliza ni nn hasa
 
Hizi hofu zitatuua, kwa kweli leo hii nimeshindwa kuvumulia, nimetembelea ma dr zaidi ya 3 ambao nina uhakika nao, wameniambia kwamba hosp nyingi hazina kipimo cha taifiord, wanachofanya wao ni ku generalize vipimo, kama kuna bacteria wanaandika in general kwamba ni positive bila kusema ni bacteria wa ugonjwa gani, kinachotokea huwa hawataki kukubali kwamba hawana kipimo hicho,
 
sijawah skia test inaitwa correctol

na screening test for typhoid ni widal test

majibu yakiwa negative unapewa majibu yako yakiwa positive ina bid wafanye titration

sasa wew hyo correctol ungemuuliza ni nn hasa
1, yaani kwenye karatasi yao iliandikwa chorestol kama sijakosea spelling, na mbele ya hicho kipimo ndipo kuliandikwa hilo jina la widal test na majibu yakaja kwa jumla jumla kwa eti POSITIVE, na niliuliza hiyo positive ni ya nini kwa kweli hakuwa na jibu la maana sana sana alisema nikitaka majibu ya taiford iko ngapi mwilini nisubiri mpaka masaa 24 yapite
 
Ni kweli, Mara nyingine huwa hicho kipimo kinachukua Massachusetts 24.
 
Wiki iliyopita nilikwenda hospitali ambayo ni private, ni baada ya kutojisikia vizuri kiafya, baada ya maelezo yangu ilionekana nipime Malaria (BS) pia dr akaandika na kipimo kingine kilichosomeka Correctol katika karatasi lao. majibu yalipotoka, kwenye BS ilikuwa NIL lakini hiki kipimo kingine kiliandikwa POSITIVE. na niliambiwa hicho ni kipimo cha Typhoid. nikahoji hiyo Typhoid iko ngapi? wakasema haionyeshi ni ngapi na nikitaka kujua ni ngapi ni mpaka vipimo vikae masaa 24. Naombeni msaada kwa wanaojua haya mambo Napata hofu isije kuwa ni POSITIVE ya HIV na pengine nimedanganywa tu kuambiwa ni Typhoid ASANTENI

Acha uoga na acha kucrame kila kinachokuwa positive ni ukimwi na negative huna acha ufilawimbi ww alaaah mm nishawahi kwenda hospitali ya Missionary nilikuwa naumwa tumboni nilikuwa naskia vichomi na tumbo kuwaka moto upate wa kulia nilipoenda hiyo hospital nikapima typhoid nikakutwa sina, ndipo nikapimwa kipimo chengine kuangaliwa bakteria nikaandikiwa positive yaamanisha nilikuwa na bacteria wanaosababisha kupata vidonda vyatumbo nikapewa dawa sasa niko fresh sasa ww unaogopa nini au mzinzi ww ushakula papuch hadi za wauza mwili sasa unajishtukia
 
sijawah skia test inaitwa correctol

na screening test for typhoid ni widal test

majibu yakiwa negative unapewa majibu yako yakiwa positive ina bid wafanye titration

sasa wew hyo correctol ungemuuliza ni nn hasa

titration ndiyo nini mkuu nijuze tafadhali!!
 
Acha uoga na acha kucrame kila kinachokuwa positive ni ukimwi na negative huna acha ufilawimbi ww alaaah mm nishawahi kwenda hospitali ya Missionary nilikuwa naumwa tumboni nilikuwa naskia vichomi na tumbo kuwaka moto upate wa kulia nilipoenda hiyo hospital nikapima typhoid nikakutwa sina, ndipo nikapimwa kipimo chengine kuangaliwa bakteria nikaandikiwa positive yaamanisha nilikuwa na bacteria wanaosababisha kupata vidonda vyatumbo nikapewa dawa sasa niko fresh sasa ww unaogopa nini au mzinzi ww ushakula papuch hadi za wauza mwili sasa unajishtukia

Teh! japo umechonga sana lakini umenisaidia kuwa na uhakika zaidi ya usalama wa afya yangu, maana na mimi nimefuatilia zaidi ndicho niilichoambiwa kwamba bacteria yoyote wao wanaandika positive, pia kati ya watu ambao siyo wazinzi mimi niko 3 bora. asante.
 
Teh! japo umechonga sana
lakini umenisaidia kuwa na uhakika zaidi ya usalama wa afya yangu, maana
na mimi nimefuatilia zaidi ndicho niilichoambiwa kwamba bacteria yoyote
wao wanaandika positive, pia kati ya watu ambao siyo wazinzi mimi niko 3
bora. asante.

ahaaaaaa 3bora nimecheka thana mm ni mbili bora
 
Naona kuna vitu vinanichanganya hapa.

Wewe uliona nini hasa..chorrectol au chorestol? Maana umetumia maneno yote mawili interchangably. Maana kama huna hakika na nini hasa kilichokuwa kwenye hilo karatasi,huna sababu ya kumlaumu huyo dr wako..maana pengine alialichoandika kiko sahihi ila wewe ndiye uliona vibaya.

Pili umesema hospitali hiyo inatumia cheap labours.Inanipa shida kidogo kujua ni busara gani ilitumika kwenda kule ilhali unaelewa kuwa hakuna cha maana kinachoweza kufanyika na cheap labours..na hayo ndiyo uliyategemea.

Mimi nadhani tunapokuwa tunamlaumu huyo dr wako,ni vema pia na wewe ukajitathmini uhusika wako katika kadhia hii.
 
Back
Top Bottom