Kwa majina haya ya wateule, vijana jiajirini mpate fedha mtateuliwa kwa hadhi za familia zenu

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Nipo mjini Dsm zamani waliliita jiji la Dsm. Nimekuja na ndege iliyonunuliwa awamu iliyopita na nimepanda madaraja mawili ya awamu ya Tano. Nilipita MFUGALE nikaiona Buguruni kwa chini ikiwa bado chakavu na yenye foleni ya malori. Baadaya nikatoka posta kwenda kunywa kahawa mlimany city nikasema wakati narudi hotelini nipite daraja la mzalendo Kijazi.

Kwa kweli ubungo imependeza na watu napishana kwa raha na hii nimpongeze Hayati Magufuli.

Lakini nikiwa Mlimani City kwa takriban masaa manne nikiwa napitia PDF ya ma Ras nikawasikia vijana wanaijadili. Kwa ujumla huku mtaani kila msomi inaonekana anamini nimteule wa Rais anayesubiri kuteuliwa.

Vijana hawa wengi wanaonekana ni wasomi wa masters na PhD au niwakufunzi wa UDS, wanachojadili nikwanini flan kaachwa, mara mkuu usiofu bado nafasi zipo,mara fulani ajasoma mbona kateuliwa, mara GPA nk Hawa ndio wasomi wa dar wanaowaza kuteuliwa badala yakuwaza kutafuta fedha.

Unapokuta vijiwe kama Mcity watu wamekaa kimakundi KUJADILI teuzi unabaini kazi hazifanyiki na vijana wameacha kujishighulisha wanasaka ajira za uteuzi.

Na Mimi kweli nilipoona Hadi Balozi Batilda anarudi kwenda kuwa DAS nimesikitika sana, Ni udhalilishaji wa hadhi ya ubalozi. Lakini pia inavyoonekana watumishi wengi ambao ni wateule wa Rais hawana kazi mbadala zakufanya. Namwangalia Chogello anakwenda kuwa DAS najiuliza seniority kwenye mfumo wa nchi ipo?

Kwamba hawa watu ndio wasimamizi wa makatibu kata wa mkoa, kwamba leo Batilda akaandike minutes za kamati ya mkoa? Kutoka waziri,balozi hadi DAS?

Pamoja na kwamba ajira ni ngumu ila haimaanishi taifa limekosa watendaji Hadi tukawachukue retired nakuwapa kazi za vijana.

Mfumo wa uteuzi uangaliwe upya, RC awe na exposure kuliko DAS lakini tunapowashurutisha senior officers ma RC watashindwa kufanya kazi na ndo tunazalisha migogoro.

Nanyi vijana subirini mzeeke ila mzeeke mkiwa na fedha au exposure ndo mtapata uteuzi
 
Du! umenistua kidogo... Batrida kawa RAS kutoka uwaziri then Ubalozi hadi huku chini tena jamani............ kweli wanasiasa hawanazo kichwani yaani kashindwa hata kuanzisha foundation mtu ambaye tayari ana exposure ya uwaziri na ubalozi ili ajiri vijana...
 
Alipaswa kutoa ajira na hizo foundation.
 
Inashangaza sana, ina maana hakuna wasomi wapya, kila siku majina yale yale....Batrida Buriani n.k wameshakula kodi za watanzania hadi basi lkn kila siku ndio wanateuliwa
 
Mweh mama ataniona kwel jamen?najiandaa kuacha kazi nikajiajiri tu.

Ngoja niwape siri moja ya mafaniko nyie vijana wa leo. Kitu kimoja nilichokigundua kwa vijana wa leo ni kwamba wana tamaa na kutaka vitu vingi vya starehe upesi upesi. Sasa kama ni hivyo ; kazi yeyote ya kuajiriwa haiwezi kukidhi mahitaji yako hivyo utajikuta unakuwa mwizi na mbadhirifu na mwishowe utaishia jela!!

Ili uweze kuwa na gari na nyumba nzuri ; nidhahiri hivi vitu havipatikani kwa upesi kama utakuwa mtu wa kutegemea mshahara!! Hapa ni lazima uwe mtu mwenye nafasi ya fedha ndio uweze kuvimudu na njia peke ya kupata utajiri ni kujiajiri mwenyewe!!! Matajiri wote duniani ni watu waliojiajiri hakuna tajiri hata mmoja anayeajiriwa hata akiwa mwizi wa aina gani hawezi kuwa tajiri kwa kuiba. Vijana mkitaka kuwa matajiri pigeni kazi kwa kujituma kwenye maeneo mnayoyapenda na kuyamudu mtafanikiwa.
 
Amesema Antony Mtaka " kujiajiri ni kazi kubwa sana mimi nawaheshimu sana sector binafsi ambao watu wake wamejiajiri maana kuna watumishi wa serikali wanalipwa mshahara hadi 12M lakini wameshindwa kujiari" mwisho wa kunukuu

Kwenye mada yako...tatizo kwenye uteuzi wa Rais ndio kwenye maslahi makubwa mnooo na hadhi kubwa sana sasa nani aangaike na kazi ndogondogo ...!! TATIZO MFUMO SIO MZURI.
 
Du! umenistua kidogo... Batrida kawa RAS kutoka uwaziri then Ubalozi hadi huku chini tena jamani............ kweli wanasiasa hawanazo kichwani yaani kashindwa hata kuanzisha foundation mtu ambaye tayari ana exposure ya uwaziri na ubalozi ili ajiri vijana...
Kujiajiri ni kipaji kikubwa mno Ndugu sio kitu rahisi na kama ingekuwa rahisi watumishi wenye mishahara 5M+ wote baada ya miaka mitano tu wangeacha kazi wajiajiri. TATIZO MFUMO NA ELIMU.
 
Du! umenistua kidogo... Batrida kawa RAS kutoka uwaziri then Ubalozi hadi huku chini tena jamani............ kweli wanasiasa hawanazo kichwani yaani kashindwa hata kuanzisha foundation mtu ambaye tayari ana exposure ya uwaziri na ubalozi ili ajiri vijana...
Njaa Haina haiba yeyote. Ukiona aibu wakati account haisomi kila mwezi at least hizo milioni 3, itasaidia nn? Wanasiasa Wana njaa na tamaa sana.
 
Amesema Antony Mtaka " kujiajiri ni kazi kubwa sana mimi nawaheshimu sana sector binafsi ambao watu wake wamejiajiri maana kuna watumishi wa serikali wanalipwa mshahara hadi 12M lakini wameshindwa kujiari" mwisho wa kunukuu

Kwenye mada yako...tatizo kwenye uteuzi wa Rais ndio kwenye maslahi makubwa mnooo na hadhi kubwa sana sasa nani aangaike na kazi ndogondogo ...!! TATIZO MFUMO SIO MZURI.
Well said
 
Ngoja niwape siri moja ya mafaniko nyie vijana wa leo. Kitu kimoja nilichokigundua kwa vijana wa leo ni kwamba wana tamaa na kutaka vitu vingi vya starehe upesi upesi. Sasa kama ni hivyo ; kazi yeyote ya kuajiriwa haiwezi kukidhi mahitaji yako hivyo utajikuta unakuwa mwizi na mbadhirifu na mwishowe utaishia jela!!

Ili uweze kuwa na gari na nyumba nzuri ; nidhahiri hivi vitu havipatikani kwa upesi kama utakuwa mtu wa kutegemea mshahara!! Hapa ni lazima uwe mtu mwenye nafasi ya fedha ndio uweze kuvimudu na njia peke ya kupata utajiri ni kujiajiri mwenyewe!!! Matajiri wote duniani ni watu waliojiajiri hakuna tajiri hata mmoja anayeajiriwa hata akiwa mwizi wa aina gani hawezi kuwa tajiri kwa kuiba. Vijana mkitaka kuwa matajiri pigeni kazi kwa kujituma kwenye maeneo mnayoyapenda na kuyamudu mtafanikiwa.
Point sana
 
Balozi Batilda anarudi kwenda kuwa DAS nimesikitika sana,
 
Back
Top Bottom