Mbona inaonekana mkurupukaji ni wewe.
Usiangalie tu upatikanaji wa hela. Hata jambazi huua, hupora, na kisha hupata hela. Na anaweza kuitumia pesa hiyo kuchangia arusi na kwenye misiba.
Asilimia kubwa ya hawa waliotoa hiyo pesa, wameporwa. Wamekubali kununua uhuru wao kutokana na kushindwa kuhimili maisha ya mateso yaliyopo magerezani. Wengi wamesoteshwa mahabusu za magerezani kwa zaidi ya mwaka mzima ili kuwalazimisha wakubali.
Walitengenezwa makosa, wakasoteshwa mahabusu kwa muda mrefu, DPP alikosa uthibitisho wa kuwatia hatiani kwa mujibu wa sheria. Wamelazimika kulipa ili wawe huru, wakaungane na familia zao. Na Jiwe alisema watakaokataa kukiri na kutoa pesa, wasoteshwe mahabusu bila huruma!!
Kufurahia unyama ni kushiriki ushetani. Mungu wa haki, asimame na wale walionewa, na awalipie kisasi kwa aliyewaonea. Waliokuwa na makosa, hao ni haki yao kulipia makosa waliyoyafanya. Lakini tunajua kuwa wengi wao wameonewa, ndiyo maana DPP alishindwa kuwasilisha ushahidi mahakamani.
Sent using
Jamii Forums mobile app