Pamoja na kujipitisha mashuleni kutuomba kura za huruma, mie nimeamua kura yangu sitampa mgombea wa ccm kama nilivyofanya 2015 hii ni kutokana na mambo 10 niliyoyaona kipindi hiki cha miaka mitano
Babia Ndonga Shokoloo, hauko peke yako na wala si waalimu peke yao wameathirika katika kipindi hiki cha miaka mitano, walioathirika ni wengi lakini kwa kipindi chote hicho hawakuwa na pa kusemea kwani uhuru huo walinyang'anywa na utawala wa kiimla usio na uvumilivu, usio na upendo, usio na subra, usio na hekima, usio na busara wala huruma.
Kulianza kujengeka tabia ya viongozi wetu kudhani kwamba wako juu ya sheria na kwamba haki zozote tulizo nazo ni kwa hisani zao na wanaweza kuzipoka wakati wowote wakitaka. Ilifikia hata wakajiaminisha kwamba hata haki yetu wananchi ya kuishi wanaimiliki wao na hivyo wakati wowote wakitaka hiyo haki wanaweza kuichukua.
Taifa lililosifika barani Afrika na duniani kote kama kisiwa cha amani ghafla wananchi wake wakaanza kuishi kwa hofu huku wakiwindwa kama nguchiro ndani ya nchi yao. Si wakulima, si wafanya biashara, si wafanya kazi, si wanafunzi...wote maisha yetu na mali zetu zikafungwa luku na kauli zetu zikatiwa kufuli, ole wako ukohoe!
Ametokea mkombozi kwa jina akiitwa Mh. Tundu Antiphas Lissu na katika kipindi kifupi cha miezi miwili tu ameweza kutukumbusha wajibu wetu kama wananchi huru. Katika muda huo mfupi, ameweza kutufungua macho na kutuondolea woga katika kuwakumbusha viongozi hawa kwamba madaraka waliyo nayo yanatoka kwetu wananchi;
nasi tunaweza tukayapoka wakati wowote.
Nakuunga mkono
Babia Ndonga Shokoloo, kumpigia kura mgombea wa CCM ni sawa na kujihukumu maisha ya hatari, maisha ya dhiki, maisha ya chuki, maisha ya ubaguzi...hapana, tarehe 28/10/2020 ni siku ya hukumu. Mateso ya miaka hii mitano sasa basi.