SPACE CADET
JF-Expert Member
- Dec 15, 2022
- 2,280
- 3,555
Hiki kisa nimekichukua FB asee
Mimi ni mama wa watoto 2 mimi na mume wangu tulikua vizuri shida ni huyu mwanaume ambaye niko naye. Nimfanyakazi mwenzangu na ni mume wa mtu.
Mwanzo mahusiano yalikua ya kawaida tu tunafurahiana lakini baadaye nikajikuta naanza kumpenda nikabeba mimba yake na ndiyo huyu mtoto wangu wa pili.
Haikua shida ila mwaka jana mwishoni mke wake alijua, katika kuongea nilimtukana sana huyo mpaka akaondoka akarudi kwao. Alipoondokja nilipata uhuru wa kukaa naye zaidi nikawa natumia muda mwingi kwake mpaka mume wangu akagundua.
Kwa ushawishi wa huyu Kaka aliniambia nimuambie ukweli wangu ili tuachane kwani yeye kashaaachana na mke wake hivyo anataka tuishi pamoja.
Kweli nilimuambia mume wangu nikamuambia na kuwa mtoto mdogo si wake, mume wangu alikasirika sana basi akaniacha na kuondoka, alichukua kila kilichochake na kwenda kupangisha nyumba nyingine.
Hii nyumba na mume wangu tulijenga pamoja ingawa ina majina yake lakini aliniachia kila kitu yeye alichukua nguo tu. Baada ya mume wangu kuondoka huyu mwanaume alichukua vitu vyake na kuhamia kwangu kwani alikua kapanga tu.
Shida inakuja hivi, mwanaume hahudumii kwa chochote, anafanya kazi na anamshara mzuri lakini hatoi hata hela ya kula, mimi ndiyo namhudumia kila kitu, nikimuuliza matumizi anadai hana hale, tunagombana sana, shida yoyote ananiambia nimuombe mume wangu.
Mwanzo mume wangu alikua ananihudumia kwani alijua naishi mwenyewe, lakini baada ya kuwa namsumbua aligundua naishi na huyu mwanaume hapa, alikuja na kuchukua mtoto mkubwa ambaye ndiyo wakwake akampeleka kwa Mama yake, tangu siku hiyo hatoi chochote na hahangaiki na mimi.
Sababu ya kuja kwako ni hivi, huyu mwanaume anataka kwenda kuchukua watoto wake 3 ambao alizaa na mke wake , si hivyo tu, kuna wengine wawili alizaa huko nnje ananiambia anataka kuishi nao kwani nyumba kubwa, nawaza kama huyu mmoja hahudumii je akileta hao wengine itakuaje.
Kaka najuta kwanini nilimuacha mume wangu, kipindi cha mahusiano huyu Kaka alikua anahudumia, anajali hela yake naiona lakini sasa hivi nimemuacha mume wangu hanihudumii kwa chochote, nimechoka nataka kumuacha lakini hata sijui naanzia wapi naomba ushauri wako nifanya nini kaka?