Kwa mambo haya mnataka tuoe kweli?

Kwa mambo haya mnataka tuoe kweli?

Hiki kisa nimekichukua FB asee

Mimi ni mama wa watoto 2 mimi na mume wangu tulikua vizuri shida ni huyu mwanaume ambaye niko naye. Nimfanyakazi mwenzangu na ni mume wa mtu.

Mwanzo mahusiano yalikua ya kawaida tu tunafurahiana lakini baadaye nikajikuta naanza kumpenda nikabeba mimba yake na ndiyo huyu mtoto wangu wa pili.

Haikua shida ila mwaka jana mwishoni mke wake alijua, katika kuongea nilimtukana sana huyo mpaka akaondoka akarudi kwao. Alipoondokja nilipata uhuru wa kukaa naye zaidi nikawa natumia muda mwingi kwake mpaka mume wangu akagundua.

Kwa ushawishi wa huyu Kaka aliniambia nimuambie ukweli wangu ili tuachane kwani yeye kashaaachana na mke wake hivyo anataka tuishi pamoja.

Kweli nilimuambia mume wangu nikamuambia na kuwa mtoto mdogo si wake, mume wangu alikasirika sana basi akaniacha na kuondoka, alichukua kila kilichochake na kwenda kupangisha nyumba nyingine.

Hii nyumba na mume wangu tulijenga pamoja ingawa ina majina yake lakini aliniachia kila kitu yeye alichukua nguo tu. Baada ya mume wangu kuondoka huyu mwanaume alichukua vitu vyake na kuhamia kwangu kwani alikua kapanga tu.

Shida inakuja hivi, mwanaume hahudumii kwa chochote, anafanya kazi na anamshara mzuri lakini hatoi hata hela ya kula, mimi ndiyo namhudumia kila kitu, nikimuuliza matumizi anadai hana hale, tunagombana sana, shida yoyote ananiambia nimuombe mume wangu.

Mwanzo mume wangu alikua ananihudumia kwani alijua naishi mwenyewe, lakini baada ya kuwa namsumbua aligundua naishi na huyu mwanaume hapa, alikuja na kuchukua mtoto mkubwa ambaye ndiyo wakwake akampeleka kwa Mama yake, tangu siku hiyo hatoi chochote na hahangaiki na mimi.

Sababu ya kuja kwako ni hivi, huyu mwanaume anataka kwenda kuchukua watoto wake 3 ambao alizaa na mke wake , si hivyo tu, kuna wengine wawili alizaa huko nnje ananiambia anataka kuishi nao kwani nyumba kubwa, nawaza kama huyu mmoja hahudumii je akileta hao wengine itakuaje.

Kaka najuta kwanini nilimuacha mume wangu, kipindi cha mahusiano huyu Kaka alikua anahudumia, anajali hela yake naiona lakini sasa hivi nimemuacha mume wangu hanihudumii kwa chochote, nimechoka nataka kumuacha lakini hata sijui naanzia wapi naomba ushauri wako nifanya nini kaka?
Hatukuletwa duniani kuwajali wasiotujali.
 
Kumbe simulizi, ndio maana Kama Haina uhalisia.
 
1)Hii ni hadithi iliyotungwa kusapoti Ushoga wa kukataa ndoa.
2)Hata kama ingekua ya kweli still haitoshi kuwa sbb ya kukataa ndoa sbb haya aliyoganya huyu mwananamke yashafanywa toka enzi za mabibi ila still mababu hawakukataa ndoa.
3)Watu wa upinde mtahangaika sana ila marijali wataoa kama kawa.
4)KATAA NDOA kama wewe ni shoga

Punguza dharau na matusi.
Sio lazima mtu afanye lile utakalo WEWE
Sio lazima mtu aseme lile uonalo WWE kuwa sahihi.

Yaani watu kufikiria tofauti na wewe unavyofikiria ni sahihi.

Hata wewe una mengii unafikiria tofauti na wengine na UPO SAHIHI KABISA.

Jifunze kuyakubali mawazo ya wengine na kama huyataki basi jibu HOJA kwa HOJA.

#YNWA
 
Stori imetungwaaaa, mpaka ikafika mahali ikabidi yenyewe ikatae kutengeneza uongo

Iddi Makengo anawapotosha sana wanawake ..

Iddi makengo huwaga una story za kipuuzi na za uongo uongo za kuwateka wanawake

Sent using Jamii Forums mobile app

Stori za uongo hizi mnatunga

Watu siku hizi wakiwa bored wanatunga story kama hii..... Zipo nyingi sana.

Kwahiyo wajuba "NILIYOWAKUSANYA" mnaikataa ndoa kwasababu haijaenda ile "direction" muitakayo?

Kwahiyo wajuba, kwakuwa tu amesema tofauti na mawazo yenu BASI KAWA MUONGO.

Kwahiyo wajuba, mnataka Dunia iende VILE MTAKAVYO NYIE.

Kwahiyo wajuba, huwa hamuwezi ku "defend" point zenu zaidi ya kutoa maneno ya kashfa kama ""mashoga nyie, mmelelewa na familia mbovu, mnamalezi mabovu N.k""

Kwahiyo wajuba, wakati mnasoma mashuleni kwenu ""Si mlikuwa na debate?"" Kwahiyo nyie mlikuwa na kazi ya kutukana wale waliowapinga, HAMKUFUNDISHWA KUITETEA MADA YENU KWA KUJENGA HOJA?

USHAURI WANGU KWENU.
ndugu zangu wakubali Ndoa, ni kweli ndoa ni Bora sanaa "KWENU" ila si kitu chochoteee kwetu.

Na ni kweli ndoa ni jambo lisilo na maana kwetu, ila ni jambo jema kwenu.

Sasa iko hivii...

Tukiwa tunajadili "HILI/HAYA" hebu tufungue akili zetu.

Tusitake Dunia na watu wotee waamini "Kile tuaminicho ni sahihi pia kwao"

Hebu Jenga hoja na sisi WAKATAA NDOA tutajenga hoja.

Ikifika point huoni usahihi wangu na cha kuandika huna basi "JUST AGREE TO DISAGREE" na ishia hapo.

Huna haja Tena ya kutoa maneno mabaya (negative words) kama "Wewe ni shoga" "Umemelewa na wazazi sijui wakoje"

Just shut up and move on.

sophy27 hebu njoo uwaelekeze wenzako hili nililosema.

Asanteni wotee MNAOITAMANI NDOA na nyie wengine Mungu awaongoze kwenye ndoa ZENU mzidi kuishi kwa kuvumiliana, ila sisi wengine MDOMO TU WA MWANAMKE TUMESHINDWA VUMILIA.

Nawasilisha;

Mr. Liverpool
Raisi wa KATAA NDOA duniani.

Nakala:-
dronedrake
Katibu Mkuu wa Chama - Kwa utekelezaji

#YNWA
 
Back
Top Bottom