Kinyonyoke
JF-Expert Member
- Oct 4, 2016
- 3,498
- 13,138
Hapa siizungumzii Manchester City, la hasha nawazungumzia manchester united, mabingwa wa kihistoria kunako ligi ya uingereza, naam ni manchester united ama mashetani wekundu ukipenda.
Man U kama wadau (mashabiki wa soka) wengi wanavyopenda kuifupisha, kwa sasa wanaenda kwa mwendo wa hobela hobela kama jeshini ni ile chenja maarufu iimbwayo "mdogo mdogo we mwendo tunayeya mdogo mdogo we mwendo tunayeya". ndivyo exactly mambo yanavyoendelea huko OLD traford.
Ole Gunnar Solskjaer amewasha moto Uingereza na barani ulaya kwa ujumla, na tayari wababe kadhaa wameshakiona cha mtema kuni,Wababe wa nguvu PSG wana habari yake,Toteinham, Chelsea, Arsenal tayari wote hawa amewagaragaza.
klopp baada ya kumpa kichapo kibaya Mourinho na kuhitimisha rasmi kibarua chake, aliingia kichwa kichwa kwa Baby faced assasin OGS kabla ya kuponea chupu chupu kwenye tundu la sindano.
Mzee mzima Pep Guardiola anakuna upara tu kwa sasa, OGS waliyemchukulia poa sasa anawanyima usingizi.Ole Gunnar Solskjaer Kila akijitazama kwenye kioo anaiona taswira ya Sir Alex Ferguson na si vinginevyo, ni kama vile Sir Alex anaishi ndani ya Ole Gunnar Solskjaer.
Nauona mwisho mzuri wa msimu huu kwa man U, Manchester united ambayo itaondoka na kikombe cha FA,itafika nusu fainali na pengine fainali ya Uefa, huku ikimaliza ligi katika nafasi nne za juu hususani nafasi ya tatu.
Wakati huo Ole Gunnar Solskjaer ametulia tuli kitini akisubiri tu kwenda mapumzikoni na kurejea kwa ajili ya msimu mpya 2019/2020.
Ni swala la muda tu.