Kwa manufaa ya Taifa, Serikali izihamishie pengine zile taasisi za kidini Kurasini kupisha Bandari

Kwa manufaa ya Taifa, Serikali izihamishie pengine zile taasisi za kidini Kurasini kupisha Bandari

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Pale ilipo TEC na Pentecost pale kurasini zinatatiza sana kazi za bandari ya Dar es salaam.

Kuna ubaya gani serikali ikafanya mazungumzo kama ikivyofanya na wakazi wengine kuzihamisha zile taasisi pale zilipo kwa manufaa ya bandari?

Malori ya mzigo yanakosa maegesho kwakuwa hakuna nafasi ya kutosha.

Inaweza kuwa ngumu kutokana na uwekezaji ulifanywa pale na taasisi zile lakini Tanzania ni kubwa kuliko taasisi. Kama Kipawa na Kurasini walihamishwa kupisha Airport na Bandari haitashindikana kwa taasisi hizi pia.

Tuwaombe na kuwashilikisha kwenye sababu na manufaa ya wao kuhama eneo ile kama vile watu walivyoombwa kuhama Kipawa, Kurasini na waliopisha ujenzi wa yanakopita mabomba ya gesi na mafuta ya uganda au wale waliopisha upanuzi wa barabara Kimara. Kusiwe na ubaguzi wa huyu ni nani na yule ni nani tunafanya maamuzi kwaajili ya taifa.
 
Wazo zuri sana, lakini waizrael wa Buza kwa Rulenge watasema umeletea udini wakati ulichoongea ni kweli kabisa tena kwa maslahi ya taifa.
 
Back
Top Bottom